Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 180 - NIMEFIKAJE HAPA

Chapter 180 - NIMEFIKAJE HAPA

Dakika kumi ziliisha, Edrian akiwa amejifungia mle ndani, Derrick alipoona yule dada anapiga kelele sana akamfunga kitambaa mdomoni kisha akarudi alipomuacha kaka yake..

Akajaribu kufungua mlango akagundua ulifungwa kwa ndani, akamuita kaka yake

"Bro kuna shida, tafadhali fungua mlango"

Akasikia kitasa kikifunguliwa akasogea na hakusubiri afunguliwe akausukuma mlango. Ed alikuwa amepiga hatua kusogea kwenye kitanda ambacho kilikuwa na Aretha aliyelala na upande mwingine Charlz

Derrick hakuelewa nini kinaendelea akamwangalia usoni kumuuliza kaka yake ambae alikuwa akibofya simu yake na kisha akaweka simu sikioni. Alipoyatazama macho ya kaka yake yalikuwa kama moto mkali ulio katikati ya msitu, akameza mate na kushindwa kuuliza

"Hello Brianna naomba vyumba viwili kwa matibabu binafsi niko njiani nakuja" alipomaliza akamgeukia Derrick

"Muinue Charlz msaidiane kumleta nje kwenye gari." Ed akasema kisha akainama akambeba kwa uangalifu Aretha ambaye alikuwa amelala, akatoka mle ndani

"Fanyeni haraka nawasubiri msichukue chochote hapa kinachohusiana na Aretha wala Charlz ." Akaondoka

Derrick kwa haraka nae akamuinua Charlz ambaye alianza kufumbua macho kwa shida. Akamkamata vyema na wakapiga hatua kwenda nje huku Angie akihakikisha vile vitu vipo

Edrian akasaidizana na Derrick kumuingiza Charlz kwenye gari. Walipomaliza Edrian akamwambia Derrick

"Naomba karipoti tukio hili chuoni waambie tuliwatafuta Aretha na Charlz sababu hawakupokea simu ndio tukawakuta wamepoteza fahamu hapa kwenye hii nyumba. Nitakupigia simu baadae"

Akaingia kwenye gari na kuondoa gari huku akiwasha taa.

Derrick akafanya kama kaka yake alivyomwelekeza akatoa taarifa kwenye uongozi wa chuo. Kitendo cha uongozi kujua aliyehusika kuwapeleka wanafunzi hao hospitali ni Edrian Simunge, polisi walifika mara moja huku uongozi wa chuo ukitoa ushirikiano wa kutosha.

Ndani ya saa moja tayari walikamatwa wanafunzi sita akiwemo Bruno. Polisi wakagundua matumizi ya dawa za usingizi kwenye vitambaa ambacho walivikuta mle ndani na pia walibaini matumizi ya mihadarati. Yule dada alipofunguliwa na polisi kila walipojaribu kumhoji wakagundua alikuwa na tatizo la akili.

Watuhumiwa wote wakapelekwa rumande, nao polisi wengine wakaelekea kule hospitali.

************

Edrian aliketi pembeni ya kitanda huku kichwa chake kikiwa kimeinama.

"Rian" sauti dhaifu ya Aretha ikamshtua naye akainua kichwa kumuangalia

"Nimefikaje hapa?" akauliza huku sauti yake ikiwa na mikwaruzo akijaribu kuinuka

Edrian alipoona Aretha akimtazama akakwepesha macho yake na kuangalia nje

"Endelea kulala hivyo hivyo daktari anakuja sasa hivi" akainuka huku akibofya simu yake

"Brianna, amemka naomba uje tafadhali" akamwambia kisha akageuka kuelekea pale kitandani alipomwangalia usoni Aretha aligundua machozi yalikuwa yakitiririka pembeni ya macho ya Aretha.. Maumivu makali yakachoma moyo wa Ed kiasi cha kufanya machozi pia kuonekana ndani ya macho yake.

"Retha tafadhali, usilie. Unahitaji kupumzika sio kulia" akamwambia Aretha huku akijikaza hasira kudhihirika kwenye sauti yake.

"Rian sikumbuki chochote na nimejikuta nikiwa hapa hospitali nawezaje kujiona sawa?" akauliza huku akimuangalia usoni Edrian lakini yeye alikwepa kuyatazama macho yake..

Kabla Edrian hajajibu mlango ukafunguliwa na Dr Brianna akaingia akiwa amevalia koti lake jeupe

"Aretha, nafurahi kuona umeamka" Dr Brianna akampa tabasamu ambalo lilituliza kidogo hali ya Aretha

"Asante dokta" Aretha akajibu akijaribu kutabasamu macho yake yakihama kutoka kwake hata kwa Ed ambaye alimwangalia Dokta Brianna

Baada ya kumtolea dripu na kumuangalia, "nafikiri utakuwa salama kabisa na nakuruhusu"

"Una uhakika Brianna?" Edrian akamuuliza kwa wasi wasi

"Hahaha mimi ni daktari, Edrian she is okay" Dokta Brianna akamjibu huku akiachia kicheko chepesi kisha akamwambia

"Naomba tuongee nje mara moja" akachukua faili na akatoka akimtakia Aretha kupona haraka

Edrian akamuangalia mara moja Aretha kisha akampa ishara kuwa atarudi

Walipofika nje dokta Brianna akamgeukia Edrian ambaye alisimama makini kumsikiliza.