"Mwili wangu unakutaka" Ed akazungumza kwa taratibu huku akisikiliza mwitikio wa Aretha. Kimya cha sekunde kadhaa kikapita, lakini bado alisikia akihema
"Retha, mwili wangu ndio unaokutaka lakini akili yangu imenizuia kabisa. Ninajaribu kukimbia kujinusuru...mmmhh" akashusha pumzi huku akigeuka kitandani na kulala kifudifudi
"Rian" Aretha akaita kwa sauti dhaifu sana
"Mhm" akaitika Ed
"Na aahm.. Natamani kukubusu tena"
"What" Akainuka kwa ghafla Edrian na kuketi
Aretha aliposikia upande wa pili "Rian uko sa_"
"Niko sawa Retha, niko sawa kabisa" akarudi kujiegemeza kwenye ubao wa kitanda
" Emhhm.. Nilihofia labda umeanguka" Aretha akashusha pumzi
"Retha, unatamani nini hasa?" Akauliza
"Rian, aomba nikuache ulale. Kesho nitaenda chuoni" Hakumpa nafasi, Aretha akakata simu akimuacha Ed akishangaa.
"Hahhaha, basi sawa" akawaza huku akiinuka kuelekea kabatini akitoa pajama zake ya kulalia. Akarudi kwenye meza, akaketi huku akichukua kompyuta mpakato tayari kupitia taarifa ambayo Captain alimtumia.
"Afadhali Captain umerahisisha kazi yangu" akawaza baada ya kuelekea kwenye barua pepe zake..
Akasoma maelezo ambayo Captain aliyakusanya, kilichomshtua ni kwamba ile namba ilionekana kumpigia Aretha mara kadhaa. Akaamua kumuandikia ujumbe mfupi Aretha kujua kama kuna ile namba ilimpigia kweli
"TikTik"
"Hapana Rian." Akajibu Aretha.
Akatafakari kwa nini kulikuwa na namba ya Aretha kwenye orodha ile. Aliitambua kwa haraka kwa kuwa aliikariri kama maji.
Akachukua simu na kumtafuta tena Captain kutafuta majibu kwa kuwa hata mahali ilipokuwa ilionesha ipo katika chuo alichosoma Aretha. Majibu ya Captain yakampa ahueni kwani alimwambia ataifuatilia siku itakayofuata.
Alipotaka kufunga kompyuta akaona barua pepe iliyoingia. Alipotazama jina ilitoka kwa Martinez, "Huyu huu usiku anataka nini tena?" Akawaza huku akifungua barua pepe ile. Akaanza kuisoma lakini hakuendelea sana.
"Aaaargh unataka kujua mambo yote haya ikiwa bado hata wiki huna" akaacha kusoma akazima kompyuta yake na kuelekea kulala huku hasira zikiwa wazi usoni.
Alipojitupia kitandani ujumbe ukaingia kwenye simu.
"Rian, kesho nitatoka saa moja jioni, naomba nikuone. Usiku mwema mpenzi"
"Ooooh sasa naweza kulala" Ed akasema kwa sauti kisha akajibu ujumbe na kuizima simu yake, akalala.
**************
Aretha aliingia chuoni mapema siku iliyofuata. Mara alipoingia darasani nuso za watu zilimuangalia huku minong'ono ya hapa na pale ilisikika. Akaamua kutowafuatilia. Kipindi hiki kiliwaweka kwenye darasa la pamoja ambalo lilimfanya akutane na Charlz wakaketi pamoja.
"Aretha pole kwa yale yaliyokukuta jumapili" Charlz akamwambia huku uso wake ukionesha uhalisia wa huzuni aliyokuwa nayo..
Aretha akashtuka na kumuuliza "Nani alikwambia?"
Lakini kabla Charlz kujibu Aretha akawa ameshaelewa "Derrick bila shaka. Asante" akatoa daftari lake na kitabu akaviweka mezani
"Ila naamini big bro atawapata tu waliofanya hivyo" Charlz akamwambia
"Shhhhh Charlz unaongea kwa sauti" Aretha akampa ishara asiongee kwa sauti
"Hahaha kwa nini unawaogopa?" Akauliza Charlz kwa utani
"Hapana, siwaogopi ila sitaki tuzungumzie hayo" Aretha akamjibu kwa sauti ya chini, lakini hakujua nyuma kulikuwa na mtu akifuatilia mazungumzo yao
"Hutaki tujue ulivyo kiberenge kuiba mwanaume asiye wako eeeh" sauti ya kiume nzito iliwashtua Aretha na Charlz.. Lakini kabla hawajageuka nyuma alipiga hatua na kusimama pembeni ya kiti alichokalia Aretha
"Bruno nadhani hatujawahi kugusana hata kidogo" Charlz akasimama kumkabili kijana yule na mara hiyo macho ya watu yakawaangalia yakitaka kujua nini kinaendelea..
Aretha akamshika Charlz mkono kumpa ishara akae lakini hakufanya hivyo akabaki amemkazia macho Bruno..
" Hahahah Charlz unatafuta umaarufu kupitia mwanamke huyu, kiberenge ni kiberenge tu hakitakuwa treni hata siku_" kabla Bruno hajamaliza maneno yake, ngumi nzito ikashuka kwenye shavu lake la kushoto na kumfanya ayumbe kuangukia kwenye meza zklizokuwa zimekaliwa na watu
Bruno akainuka kwa haraka ili kumvaa Charlz kwa ngumi lakini sauti ya mkufunzi ikawastua