Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 176 - KULA NINI

Chapter 176 - KULA NINI

"Sijui baba, mimi niliandaa watu wangu wamteke Aretha lakini kabla hawajafanya hivyo purukushani ile ikatokea"

Lyn akainuka

"Watu wamteke? Wampeleke wapi? Ila njia zako huwa hufikirii kwa kiasi gani zinakugharimu?" Martinez akamuuliza binti yake

"Baba, wangemteka hata nisingemfanya chochote zaidi ya kumtisha tu, yule binti ni muoga sana"

"Umekosa njia nzuri ya kumrejesha Simunge hadi unaanza kuteka watu?" Baba yake akamuuliza akimwangalia kwa ukali

"Baba, yule binti nakwambia anahitaji kuti__" Martinez akanyoosha mkono akamkatisha binti yake

"Umechezea nafasi nzuri ambayo wengine waliitafuta. Nimekusaidia sana ila sasa tulizana kabisaaa, usije haribu mambo"

Lyn akamwangalia baba yake huku midomo yake akiivuta mbele kama mtoto mdogo, "baba lakini nitaachaje mwanamke mshamba kama yule anizidi akili kwa Ed"

Martinez akaweka karatasi aliyoshika mezani akamuangalia Lyn, "Kwa kusema hivyo umesahau lengo la kuwa na huyo Simunge. Au umempenda?"

Lyn akatikisa kichwa kukataa, baba yake akamwangalia kisha akarudisha macho kwenye karatasi na kuendelea kusoma. Lyn alivyoona hivyo akapiga hatua kuondoka pale sebuleni lakini mikono yake ikatuma ujumbe wakati huo huo katika simu yake. Akaelekea chumbani kwake huku akitabasamu

*************

"Rian, umefika salama?" Ujumbe uliingia kwenye simu ya Ed

Ed akatabasamu mara alipoegesha gari na kuusoma huku akiangalia idadi ya simu alizopiga Aretha ambapo mara mbili mfululizo zilizipigwa pasipo kupokea akiwa njiani.

"Niko salama princess, nitakupigia" akaandika na kumtumia Aretha.

Akashuka kwenye gari na akapiga hatua za haraka kuelekea chumbani kwake. Alipoingia akaelekea bafuni moja kwa moja na maji yakasikika yakimwagika mfululizo. Akiwa huko hakujua simu yake ilikuwa ikiita mfululizo

Ikamchukua muda wa dakika thelathini kabla ya kutoka huku akijikausha akaelekea ilipo simu yake. Akakutana na namba mpya ambayo ilimtafuta mara sita,

"Huyu ni nani tena" akajiuliza

Akaamua kuipiga namba kabla ya kumpigia Aretha, mara simu ilipopokelewa alisikia sauti ya kike iliyokuwa ikitoa kilio ikiomba msaada huku ikitaja jina lake

"Ed naomba uje unisaidie, aaaaah ananiumiza, niacheni"

Taulo iliyokuwa kichwani kwa Ed ikaanguka, alipojaribu kuita upande wa pili hakuna aliyeongea zaidi ya kuomba msaada. Akauliza ni nani aliyehitaji msaada wake, upande wa pili hawakujibu zaidi ya kelele za kuomba msaada na kisha simu ikakatika ikimuacha Ed katika mshangao. Akaangalia simu kwa muda kisha kama radi akakumbuka akapiga simu ya Aretha kwa haraka

"Rian" sauti ya Aretha ikaisika huku ikiwa imejaa wasi wasi

"Retha uko salama?" Swali la Ed likamshtua Aretha

"Mimi niko salama Rian lakini wewe ndio unanipa wasi wasi nini kimetokea?"

Ed akashusha pumzi kwa nguvu, "naomba dakika moja nitakupigia" akamwambia Aretha, lakini sauti ya Aretha ikamkatisha

"No...Rian kuna nini kwani?"

"Niko salama Retha nataka nimpigie mtu kazini mara moja kabla sijaongea nawe, tafadhali" Edrian akamsihi Aretha naye akaridhia akakata simu na kumpigia Captain

"Nakutumia namba naomba uniangalizie taarifa zake zote na simu ya mwisho iliyopigwa ilikuwa maeneo gani. Nijulishe haraka ukimaliza" alipomaliza akakata simu na kurudi kumpigia Aretha

"Retha samahani ila niko salama usihofu" Ed akaanza

"Umekula?" Akauliza Retha

"Kula nini?" Akamuuliza kwa mshangao huku akiuacha mshangao ule kwa Aretha

"Rian, ni. .Nilikuudhi? au kuna kosa nilifanya aan...nil____"

"Hapana Retha" Ed akatabasamu baada ya kumsikia Aretha akifinya finya maneno kisha akaendelea

"Kwa nini unadhani kuna kitu umeniudhi?"

Akauliza huku tabasamu likizidi usoni kwa Ed

"Eeeh" Aretha akashtuka

"Umenisikia Retha" akanyamaza akimsikiliza akaelekea kitandani, akaketi akiegemea kwenye ubao mkubwa wa kitanda

"Aaaah sababu aaaa...ni, Rian aaaargh kwa nini ulikataa kuingia ndani" Aretha akapata shida kueleza kwa kuwa alihisi Ed angempa maswali zaidi

"Retha" Ed akamuita kisha akameza mate na akaendelea baada kusikia sauti dhaifu ya Aretha ikiitika

"Mwili wangu unakutaka" Ed akazungumza kwa taratibu huku akisikiliza mwitikio wa Aretha