Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 175 - NAHITAJI KUOA

Chapter 175 - NAHITAJI KUOA

Edrian aliendelea kufumba macho akisubiria Aretha ampe busu alilolitamani kwa wakati huo. Alitabasamu akifikiri ni kwa namna gani mapenzi yake kwa Aretha yamembadilisha na kumfanya kuwa kama mtoto ambaye hutumia kila fursa kupata anachotaka. Kuna wakati alihisi mwili wake ulitaka kulipuka kwa matamanio juu ya binti huyu.

"Come on Retha, I need this" akawaza moyoni

Taratibu ulaini wa midomo ya Aretha ukagusa ile ya kwake. Akaamua kujizuia ampe nafasi Aretha kuweza kumshawishi kuzama katika busu zito. Akamuacha Aretha akambusu taratibu na alipoona ameacha

Akafumbua macho na kumtazama "Retha umenibusu au?"

"Eeeh" Retha akashtuka na kumwangalia Ed

"Rian... tuko ba_"

"Retha, busu kwanza" Ed akafumba macho tena. Aretha alipoona hakuna dalili za kubadili msimamo hakutaka kusita sita.

Ghafla Ed akashangaa mikono ya Aretha ikiwa shingoni kwake na midomo yake laini ikimbusu kitendo kilichomfanya ashindwe kujizuia na kumdaka Aretha. Katika siku ambayo Ed anakumbuka kumbusu Aretha sana basi leo ilishika rekodi.

"Rian" alishtuliwa na sauti dhaifu ya Aretha ambayo ilimrudisha kwenye hali kwenye ufahamu wake. Akaacha taratibu huku akimsikia Aretha akihema kwa nguvu akijaribu kurudisha hewa iliyopungua kwa busu lile.

Ed akashusha vioo kuruhusu hewa ya nje kuingia ndani, kisha akawasha gari na kuondoka.

Aretha macho yake yaliangalia nje huku akitabasamu kila alipotafakari lile busu. "Eewhh hili busu lina nini" akawaza maana kila alipolitafakari mwili wake ulimpa mwitikio wa kuhitaji tena..

Edrian hakuongea chochote aliendesha gari huku akiongeza mwendo. Muda mfupi baadae walisimama nyumbani kwao Aretha.

Aretha akamwangalia Ed huku macho yake yakiwa na wasi wasi akihisi huenda alikosea kumuita.

"Rian kuna k__" akakatishwa na mkono wa Ed uliomshika kwenye shavu.

"Nina njaa Retha" sauti ya Ed ikatoka dhaifu japokuwa tabasamu lake lilituliza wasi wasi wa Aretha

"Rian, twende ndani ukale tafadhali mama atakuwa na chakula" Aretha akamwambia kwa kujali huku akiweka mkono wake pale Ed alipoweka

"Ahm Retha nitakula nyumbani, nitakuona kesho, mwambie mama asante sana" akatoa mkono shavuni kwa Aretha na kubonyeza kitufe cha kufungua mlango.

Aretha akamwangalia akishtuka asielewe akidhani kama Ed alikasirika hata anakataa kwenda kuingia ndani

"Rian"

"Retha tafadhali nitakupigia nikifika" akamsihi kiasi cha kumfanya Aretha afungue mlango na kushuka. Alipomaliza kuufunga akafungua tena ambapo akamuona Ed ameegama kwenye usukani.

"Rian are you okay?" Akamuuliza

Ed alishtuka alipoona mlango umefunguliwa tena akainua kichwa na kumuangalia Aretha huku akitikisa kichwa

"Yes am okay Retha, worry not" akamhakikishia

Aretha akafunga mlango, Ed akamtazama alipoelekea getini hata alipoingia ndani akaondoa gari yake kwa mwendo wa haraka.

"Nahitaji kuoa hahaha" akacheka wakati akiendesha kuelekea nyumbani

****************

"Baba, naapa kabisa sio mimi niliyehusika na hizo picha" Lyn akamwambia baba yake aliyekaa sebuleni akipitia makaratasi ya mauzo ya hisa

"Natumai hujafanya chochote ambacho kitatuingiza mashakani. Tuko hatua za mwisho tunahitaji utulivu mkubwa tunapopanga" Martinez akamwambia binti yake

"Kwa hiyo baba unafikiri utaweza kuwashawishi wengine pia?" Akauliza Lyn

"Huniamini na wewe?" Akauliza Martinez akishusha miwani yake kwa chini

"Hapana baba, nakuamini. Najua mipango yako itakaa vizuri tu" Lyn akamwambia baba yake huku akisogea kuketi alipoketi

"Baba, huyu Aretha nataka nimkomeshe kidogo" Lyn akamwambia

"Mh. . Utamkomeshaje?" Akauliza Martinez huku akimwangalia usoni

"Aaaah baba, Nina njia nzuri na rahisi ya kumshughulikia"

"Hahaha utamuwezaje maana huyo Simunge amemwekea ulinzi"

"Hahahahah baba, nitamkomesha kule ambako Ed hatoweza kugundua. Maana kwenye onesho alinilaumu mimi lakini sio mimi. Tena nafurahi kumbe maadui wa huyo mwanamke tupo wengi" Lyn akamwambia baba yake huku akiinua miguu yake na kuiweka mapajani mwa baba yake.

"Kama sio wewe unadhani ni nani amehusika?" Akauliza

"Sijui baba, mimi niliandaa watu wangu wamteke Aretha lakini kabla hawajafanya hivyo purukushani ile ikatokea"