Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 165 - NITAKUJA KWAKO

Chapter 165 - NITAKUJA KWAKO

Aliingia kwenye chumba alicholazwa Aretha, kule kumuona amepumzika moyo wake ukatulia. Hakujua mama yake Aretha hakuwa amelala, alisikia hatua zake. Alipogeuka kuondoka sauti ya upole ikamuita,

"Mwanangu usiondoke"

Edrian akasimama pasipo kugeuka, mapigo yake ya moyo yaligonga kwa haraka akajikaza kiula na akageuka kumwangalia mama ambaye sasa aliinuka taratibu huku akimlaza Aretha ambaye alilala mikononi mwake.

Edrian akabaki amesimama pale pale mpaka mama alipomaliza, akasogea alipokuwa amesimama akampa ishara watoke nje.

Walipotoka nje, Ed akamsubiri mama aketi kwenye benchi ndipo naye akaketi. Li aliagizwa kumpeleka Frans nyumbani pamoja na kuchukua nguo na vitu vichache kwa ajili ya mama na Aretha. Mama aliomba Frans abaki nyumbani hivyo Li pekee ndie angerejea.

"Mwanangu najua unavyojisikia, naelewa hofu yako kwa binti yangu, lakini kuna kitu kimoja ambacho ninaamini hata sasa... " mama akaanza kusema mara tu walipoketi huku akiyaelekeza macho yake mbele kutazama ubao uliokuwa na matangazo ya hospitali.

Edrian alikaa kimya akisubiri kile ambacho mama huyu alitaka kumwambia. Moyoni alihofia isije ikawa ndio tamati ya kuwa na Aretha, lakini mara zote wazo hilo alilitupia mbali nyuma kabisa ya ubongo wake

"Nampenda Retha, najua ananipenda hii ni dhoruba ya muda tu, itaisha." Akawaza moyoni na kujitia moyo

Mama akaendelea, "Naamini mnapendana. Uvumilivu unahitajika kwenu nyote. Retha hajui dunia yako ilivyo na hajui michezo yake inavyogeuka kila siku. Anaogopa lakini hataki kukupoteza pia."

Edrian aliposikia hivyo moyo wake ukapata tulizo la ghafla na amani ikasafiri katika kila eneo la mwili wake hadi uso wake ukaathiriwa.

"Mama" Edrian akamuita

Mama akainua uso na kumuelekea Ed, akamsikiliza kama asikilizavyo watoto wake

"Naomba niseme hivi sikuwahi fikiri kumpenda mwanamke kama ninavyompenda Retha. Ninafanya kila niwezalo ajue namjali, nampenda na namthamini. Ninachotamani kwake ni kuniamini. Hiki kilichotokea kinaweza kuwa kigeni kwake lakini mimi najua. Nitafanya niwezalo mapema ili azidi kuwa salama"

Mama akashusha pumzi kwa nguvu kama mtu aliyeshusha mzigo mzito, "Asante mwanangu. Naomba ukapumzike, mpe muda wa kukuelewa. Kesho atakuwa bora zaidi."

"Usijali mama, nitapumzika hapa hapa" Ed akamuondoa shaka mama yake Aretha japokuwa alimshawishi aende nyumbani lakini jitihada zake hazikufua dafu...

Wakabaki pale wakimsubiri Li arejee, kwa upande wa Ed hakupata shida kufikiri wapi angepumzika sababu Dokta Ivan alimkaribisha ofisini kwake ambapo kulikuwa na chumba ambacho mara nyingi hukitumia kupumzika iwapo ratiba za upasuaji ziliisha usiku au kuanza usiku sana.

Majira haya ya usiku kulikuwa na baridi, Ed aliihisi ikipenya ndani yake sababu alibaki na ile shati huku koti akikumbuka kumfunikia Aretha wakati akiwa kwenye gari. Akamuaga mama huku akimuomba arudi chumbani kukaa na Aretha, yeye akaelekea kwenye gari kulifuata koti.

Njiani simu ya Captain ikaita, akapokea na kusikiliza kwa umakini kisha akakata simu na tabasamu laini likaonekana usoni kwake..

"I know BM. You have something to do with all that. Nitakuja kwako taratibu"

*********

Asubuhi ilifika Ed akiwa hospitali baada ya kumlazimisha Li aende nyumbani apumzike baadae aweze kumletea nguo za kubadilisha. Kile chumba ndani ya ofisi ya Dokta Ivan kilibeba huduma zote, hivyo Ed aliamka alfajiri japokuwa masaa aliyotumia kulala ni mawili tu. Alitumia muda mwingi kuangalia moja ya picha za CCTV ambazo zilitumwa kwenye simu yake.

Baada ya kuoga, akachukua nguo ambazo Li alimletea alfajiri. Alipomaliza akaelekea kwanza kuona hali ya Beruya ambaye sasa alikuwa amerejewa na fahamu zake. Alizungukwa na ndugu zake ambao walimsikiliza Dokta Damian ambaye ni mchumba wa Beruya akiwapa kwa ufupi tathmini ya hali ya Beruya..

Ed akaongea na Dokta Damian kwa muda mchache kujua kama kuna chochote kinachoweza kuhitajika kwa ajili ya kumsaidia Beruya. Katikati ya mazungumzo yake na dokta Damian, aligundua hali ya lawama kwa kile kilichompata Beruya kuweka kwa Aretha.

"Unajua kaka, Beruya angesikiliza ushauri wa rafiki yake"