Edrian alipotoka kumuona Beruya, moyo wake ulikuwa mzito na kiasi alimuonea huruma Aretha. Akawaza iwapo maneno haya angeyasikia Aretha basi hali yake ingekuwa mbaya zaidi. Akakumbuka jitihada zake kumsaidia Damian kuona kuwa tukio hili si kwa sababu ya Aretha bali ni mtu mwenye nia mbaya na sanaa ya picha, lakini hakuweza kumwelewa.
Akashusha pumzi mara aliposimama kwenye korido iliyoelekea chumba cha Aretha. Alipoangalia alimuona mama akiwa amekaa kwenye benchi na Frans. Akapiga hatua kwa haraka kuelekea walipokuwa, wakasalimiana.
"Mama mbona mko nje Dokta Brianna yuko ndani?" Akauliza
"Hapana mwanangu, mdogo wako ndio ameomba kuongea na Retha" mama akamwambia
"Linus?" Akauliza kwa mshangao
Mama akakubali kwa kutikisa kichwa. Edrian akashusha pumzi kisha akaketi kwenye benchi akijiuliza Li atakuwa anaongea nini na Aretha.
**********
Linus mara alipotoka ofisini kwa dokta Ivan akakusudia kumuona Aretha walau kuzungumza kile alichoamini kitasaidia kumtoa kaka yake katika hali ya huzuni aliyoiona jana.
Alipoingia chumba kile alicholazwa alimkuta dokta Brianna akiwa na Frans na mama yake Aretha. Baada ya dokta kumhakikishia Aretha kuwa anaweza kurudi nyumbani na kupumzika, Li alitumia nafasi hiyo kuomba kuongea na Aretha
"Li mazungumzo mafupi yasiyo na hisia kali" Dokta Brianna alimnong'oneza Li wakati wanatoka nje kumpa nafasi ya kuongea na Aretha. Li akatabasamu maana alimfahamu daktari huyu
Aretha alimwangalia Li huku akijaribu kuonesha kutokuogopa lakini ukweli ni kwamba, mapigo yake ya moyo yaligonga kwa nguvu sababu ya wasiwasi wa kile ambacho Li alitaka kuongea nae.
"Aretha, nakuomba kwanza 'relax' usifikiri nina jambo zito la kusema nawe, ni mambo ya kawaida kabisa" Linus akamwambia huku akivuta kiti na kuketi karibu na Aretha ambaye sasa aliketi kitandani huku miguu yake ikining'inia chini..
Aretha akatabasamu "niko sawa kaka Li"
"Najua matukio yaliyotokea yanakufanya ujione mwenye hatia, lakini tambua wewe huwezi kudhibiti tabia ya mtu iwapo atakusudia kufanya ubaya. Mambo mawili ya kuwa makini nayo, moja, usiruhusu kujilaumu kwa mambo ambayo hungeweza kuyadhibiti na la pili usiwalaumu watu ambao wao pia wasingeweza kudhibiti kile ambacho wewe umeshindwa kukidhibiti." Li akamwangalia Aretha ambaye alimsikiliza kwa makini
"Ninajua maisha ya kaka yana changamoto nyingi, lakini nachagua kuamini kuwa unaweza kukabiliana nazo. Unahitaji kujipa nafasi kuelewa yanayoendelea na ujifunze kutoruhusu hisia zako kuingiliwa na matendo ya watu wengine. Usipofanya hivyo utawapoteza watu muhimu ambao wamejitoa kuwa nawe"
Li akainuka, "Najua utafanya kilicho sahihi kwa faida yako Aretha. Sikulazimishi ila pia sipendi kuona maumivu yakizaliwa tena kwenye moyo ulioanza kuchipua pendo"
Akasimama kabla ya kupiga hatua kutoka mle ndani, lakini kabla ya kushika kitasa cha mlango swali lilifuata nyuma yake
"Kaka Li, Rian yuko wapi?" Aretha akauliza huku akifinya vidole vyake!
Li akatabasamu na kumjibu huku akageuka "Nadhani atakuwa amemaliza kujiandaa na anashuka kuja kukuona."
Aretha akamwangalia kisha akamwambia "Asante kaka Li, ukimuona mwambie naomba nimuone kabla sijaondoka."
"Atakuwa tayari mlangoni anataka kujua ninaongea nini muda wote huu na__" kabla ya kumaliza maneno yake mlango wa chumba kile ukafunguliwa taratibu, Edrian akaingia
Li akamwangalia kisha akamgeukia Aretha, "nilikwambia uvumilivu umemshinda...Asante Aretha. Mazungumzo mema" akageuka na kutoka akimuacha Ed asielewe nini Li alimaanisha lakini kumuona Aretha akiwa na uchangamfu ule ulimfanya ajisikie farijiko la ndani.
"Rian..am sorry" Aretha akasema huku macho yake akiyatazamisha chini
"Retha, unaendeleaje?" Edrian akajifanya kubadilisha mada kwa kuwa hakutaka kuongelea tena jambo lile lililopelekea kuwepo hapa hospitali.
Aretha akainua uso na kumwangalia Ed ambaye alisogea lakini akiacha nafasi kati yao na kuvuta kiti akaketi.
"Naendelea vyema, dokta Brianna amenipa ruhusa niende nyumbani"
"Aaaaah vizuri. Huko utapumzika vizuri zaidi. Utakubali niwapele__"
"Rian" Aretha akamuita Ed
"Ahhmmm" Ed akaitika
"Please, I am _"