Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 158 - MNAFAHAMIANA?

Chapter 158 - MNAFAHAMIANA?

"Aretha uko salama?" Akauliza Coletha huku akimpa maji pale alipoketi. Aretha akayapokea na kunywa kimya na alipomaliza akarudisha chupa kwa Coletha.

Macho yake akayainua kuangalia kule picha zilipokuwa, machozi taratibu yakaanza kumtoka.

Wakati huo huo Derrick alikuwa akizungumza na Yassin meneja wa Beruya ambaye naye alikuwa amechanganyikiwa kwa kile ambacho kilifanyika kwenye picha zote pale ukumbini. Watu wengine walianza kutoka, malalamiko yaliendelea kusikika hapa na pale wengine wakimfuata Yassin kutaka kujua hatma ya onesho hilo.

Edrian akarudi kwa haraka kwa Aretha ambaye hakuongea chochote zaidi ya kumwangalia tu usoni na kulia.

"Retha please don't be hard on yourself, it's goin to be okay" akajaribu kumbembeleza, lakini sauti ya kipaza sauti ikawashtua

"Mabibi na mabwana naomba usikivu wenu"

Edrian hakujaribu kuinua macho kumwangalia aliyeongea, alimuweka Aretha kifuani kwake huku machozi yakilowanisha shati yake na kumfanya kusikia ubaridi ukifikia ngozi yake. Sura yake ilibeba mfano wa bomu lililokuwa tayari kulipuka

Ukumbi ulipopata utulivu akaendelea kuongea, "kuna wakati vitu huwa vinatokea nje ya matakwa yetu, lakini haimaanishi kuwa hakuna wema tunaoweza kuuvuna." Akaangalia mahali alipokuwa Aretha na Ed lakini wao hawakumuona sababu walimtega mgongo...

Akaendelea, "Hizi picha zinazoonekana kuchanwa katikati zinabeba hadithi ambayo mimi nataka niinunue kwa gharama yoyote" Derrick na Yassin wakashtuka baada ya kusikia maneno yale. Derrick akamkumbuka mtu yule lakini kwa kuwa bado akili yake iliwaza kilichotokea hakujali sana maana aliona amewasaidia kuokoa jahazi lililoelekea kuzama! Yassin akaachia tabasamu la matumaini.

Edrian aliposikia maneno yale akageuka amuone aliyeongea, ghafla sura yake ikabadilika lakini akajikaza akiendelea kumkumbatia Aretha ambaye aliificha sura yake kifuani kwake.

Watu waliokuwa ukumbini wakageuka na kuangalia zile picha huku minong'ono ikiibuka hapa na pale maana ilikuwa ni vigumu kuona uzuri. Ni wazi kabisa aliyechana alitumia kisu kikali na kwa kila picha alichana alama ya X katikati ya picha.

"Nitanunua picha tano za Aretha ambaye ni mchoraji chipukizi ili kutomkatisha tamaa na tatu za Beruya ambaye najua atainuka tena. Kuna yeyote anayeweza kuniunga mkono? Karibu" Akamaliza huku mwanaume huyu ambaye muonekano wake uliwafanya watu waliokuwa ukumbini kumsikiliza.

Yassin aliposikia maneno yale akaelekea aliposimama mwanaume huyu ambaye macho yake yalielekea kule alipokuwa Aretha, " Nashukuru sana BM kwa kuunga mkono juhudi za Beruya. Picha hizi zote mpaka muda alipoondoka Beruya zilikuwa salama. Hatujui kilichotokea. Lakini nina uhakika hatutaruhusu tukio hili liwe sababu ya kutuzuia kuendelea. Tutafuatilia kujua nani alihusika. Kwa atakayetaka hizi picha anaweza kuonana nami au mwenye beji ya mauzo" Yassin akamaliza

Aretha aliposikia jina la BM likitajwa akashtuka na akajitoa kifuani kwa Edrian kisha akainuka na kutazama jukwaani. Wakati huo BM alianza kushuka ngazi kuelekea alipokuwa Aretha.

Derrick alipoona muelekeo wa BM akasogea kwa haraka alipokuwa Aretha na wakati huo Edrian alisimama pembeni yake.

Edrian alipoona Aretha akijaribu kutabasamu huku akimuangalia BM, akahisi ngumi nzito ya wivu ikigonga moyoni mwake. Akainama kwenye sikio la Aretha akamuuliza taratibu japokuwa Derrick aliyekuwa amesimama karibu naye alisikia

"Mnafahamiana Retha?"

"Aaaaahm" akashangaa na kutaka kumjibu Ed lakini alichelewa maana tayari BM alikuwa mbele yao..

"Mr Simunge sikuwahi kujua unavutia na sanaa hii ya picha!" BM akamtania Ed huku akinyoosha mkono kumsalimia

"Mmmmmm" Edrian akaguna lakini akanyoosha mkono wake kumsalimia

"Aretha pole kwa kilichotokea, lakini nataka nitunze kumbukumbu ya huu mwanzo wa safari yako" BM akamwambia Aretha huku akitaka kumgusa begani, lakini Edrian akamvuta ubavuni kwake

Derrick akaingilia kati baada ya kuona hali ya kaka yake ikibadilika

"Asante kwa kujitolea kununua picha za Aretha, hayuko vizuri kwa sasa, naweza kuongea nawe, mimi ni meneja wake"

"Ooooh ni sawa" BM akamjibu Derrick kisha akamgeukia Aretha