Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 159 - SIJUI NIA YAKE

Chapter 159 - SIJUI NIA YAKE

"Ooooh ni sawa" BM akamjibu Derrick kisha akamgeukia Aretha na kumwambia

"Aretha, nanunua picha zako zote na nitakuwa tayari ikiwa utahitaji msaada wangu"

Edrian aliyekuwa amenyamaza huku mkono wake umemshika begani Aretha akataka kumjibu, lakini hakuendelea maana alisikia sauti ikimuita na kumfanya aangalie mbele yake.

Mwanaume mwingine aliwasogelea ambaye mavazi yake yalimfanya aonekane kuwa hakuwa mmoja wa watu waliokuwamo ukumbini. Alivaa pensi aina ya jeans na fulana huku chini akiwa amevalia makobazi

"Oooh BM" akaachia tabasamu alipomuona BM ambaye alimpa ishara ya kumsalimia kwa kumpungia mkono, kisha akamwangalia Edrian ambaye kwa muonekano wake ulimfanya mwanaume huyu kuondoa tabasamu lake usoni na kuvaa sura ngumu

"Brother, am sorry! Nafuatilia kujua nini kilitokea" akamsogelea Edrian

"Tobby nafikiri kwa hili tunahitaji kuongea. Naliacha mikononi mwako leo kesho nitakuja" Edrian akamwambia na wakati huo akageuka aliposimama Frans na Coletha na kuwapa ishara wamfuate.

Aretha ambaye muda wote alinyamaza ubavuni mwa Edrian akasita kupiga hatua.

"Retha" Edrian akamwangalia kutaka kujua nini kilimfanya asite

"Rian, nahitaji kumshukuru BM" akaongea taratibu

"Kwa nini umshukuru?" Akauliza Edrian huku macho yake yakimulika kwenye yale ya Aretha

"Rian, are you okay!" Aretha alishtuka aliposikia swali lile

Edrian akashusha pumzi kama mtu aliyebeba kitu kizito kisha akamwambia Aretha "Sioni umuhimu wa kwenda kumuaga sababu sijui nia yake Retha"

Aretha akamwangalia kujaribu kumuelewa, akakumbuka hakuwa amemwambia kama alikutana na BM kwa mara nyingine. Bado nafsini mwake aliona ni vizuri kumshukuru mtu aliyeamua kununua picha zilizoharibika

"Rian kumshukuru hakuhitaji kujua nia yake nadhani ni_"

"Mr Simunge naweza kuongea na Aretha mara moja?" BM akamsogelea Edrian huku nyuma akifuatiwa na Derrick ambaye alimuangalia kaka yake kwa mashaka

Edrian akamgeukia BM ambaye alimpa tabasamu huku macho yake yakimuelekea Aretha

Kabla hajajibu Aretha alipiga hatua pembeni akijinasua mikononi mwa Edrian

"Pia nilitaka kuongea nawe" Aretha akamwambia huku macho yake ya aibu yakijaribu kuyakwepa yale ya BM

"Retha" Edrian akamuita kwa wasi wasi lakini Aretha alimuangalia kwa jicho lililobeba ujumbe wa 'niamini'

Derrick akasogea pamoja na Aretha kuongea na BM. Edrian alipoona Aretha ameamua kumsikiliza BM yeye akasogea mahali Tobby aliendelea kuhoji watu wa ulinzi. Kwa sasa ukumbi ulibaki na watu wachache, Yassin alifanya kazi ya kuwahakikishia watu mahali pale kuwa litaandaliwa onesho lingine. Na mara waandishi wa habari

Tobby alipomuona Edrian akisogea alipokuwa akawaza ishara walinzi watoke na yeye akapiga hatua kumfuata.

"Mr Simunge"

"Mmmmmm" Edrian akaguna kisha akamuuliza..

"Yule ni nani?"

Wakaelekeza macho aliposimama BM na Aretha, Tobby akamjibu kwa kuuliza "unamaanisha BM?"

"Mm"

"Humfahamu Bon" Tobby akauliza kwa mshangao!

"Ningemfahamu nisingekuuliza brother" Edrian akamjibu pasipo kupepesa macho yake ambayo hayakutoka hata sekunde kumwangalia Aretha..

"BM au Bon ni moja kati ya wawekezaji katika eneo la burudani. Anamiliki lebo na wasanii wengi ambao wanafanya vizuri" Tobby akamwambia Edrian

"Mmmmm, Tobby nini nimetokea hapa?"

"Brother hata mimi sikujua nimepigiwa simu ndio kufika hapa. Polisi watakuja hapa muda si mrefu nimeshawajulisha. Nimehoji walinzi waliopo na kuhakikisha hakuna anayeondoka. Na waliolala wamepigiwa simu kuripoti hapa ili kuwarahisishia polisi" Tobby akamueleza Edrian

"Okay, nitakuja hapa kesho tuongee" Edrian akaanza kupiga hatua kuelekea alipo Aretha, Derrick, Frans na Coletha wakimsubiri..

"Brother lakini huyo binti atatakiwa kubaki sababu mwenzake yuko hospitali, tutahitaji mtu wa kuelezea tukio lote" Tobby akamjulisha mara alipoona akiondoka

Ed akageuka na kumwambia "Yassin na Derrick watatoa maelezo nadhani kwa sasa anahitaji kupumzika" kisha akageuka na kuondoka.

Alipofika waliposimama akampa maelekezo Derrick kisha wakatoka, lakini Aretha alisisitiza waelekee hospitali kujua hali ya Beruya ikoje. Edrian hakubishana nae bali aliondoa gari