Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 154 - HAKUMBUKI

Chapter 154 - HAKUMBUKI

Asubuhi ya siku ya onesho Edrian alichelewa kuamka, kwa kuwa alirejea usiku sana akiwa na uchovu mwingi.

Kwa upande wa Aretha aliamshwa asubuhi na simu kutoka kwa Victoria ambaye alipewa jukumu na Edrian la kuhakikisha anaweka watu mahiri watakaompa muonekano unaofaa kwa tukio la leo.

"Aretha kuna mtu namwagiza kukuchukua nataka twende Spa mara moja halafu tutamalizia mambo mengine hapo nyumbani...nipe maelekezo!"

Aretha aliposikia akakurupuka pale kitandani na kuinuka, akampa maelekezo ya kumfikisha hapo nyumbani alipomaliza akakimbilia bafuni na kujiandaa. Alipoangalia simu yake hakukuwa na dalili yoyote iliyoonesha Ed alimtafuta. Akaanza kupiga simu lakini kabla ya kuita akakata

"Acha apumzike atakuwa alichoka sana" akawaza Aretha akatoka na kuelekea jikoni apate kifungua kinywa lakini alipofika sebuleni akakumbuka jana alipitiwa na usingizi mara alipoingia kwenye gari ya Edrian, lakini namna gani alifika chumbani kwake hakumbuki

"Unawaza nini maana umekuja mbio halafu ghafla umesimama" akauliza mama aliyeketi kwenye kochi huku akitabasamu

"Ah mama, shikamoo" Aretha akamsalimia mama yake huku akili yale ikijaribu kuunganisha matukio lakini akaamua kuacha

"Mama yule mtu wa 'make up' amenipa maelekezo niende naye Spa. Baadae tutarudi naye hapa" akamwambia mama yake na kuelekea kwenye meza ya chakula akachukua kikombe na kumimina maziwa kidogo, akachukua na vipande viwili vya mkate, akaanza kula

Wakati huo simu yake ikaita alipoangalia ilikuwa ni namba mpya, akapokea na kusimama huku akimalizia maziwa

"Hellow" akaitikia,

Upande wa pili ukampa taarifa kuwa ni dereva aliyeagizwa kuja kumchukua. Akatoka kwa haraka huku akimpa maagizo mama yake,

"Mama nikarudi muwe tayari naomba"

Mama yake akatabasamu na kuinuka huku akimuangalia kupitia dirisha lililoelekea getini.

"Uwe salama binti yangu" akasema kwa sauti ya chini na mara uso wake ukawa na huzuni.

Aretha akiwa amevalia gauni fupi rangi ya kijivu na viatu vya kamba, alipofika nje aliona gari ndogo yenye mchirizi wa kijani ikiwa imesimama karibu na geti. Akasogea kumsalimia dereva ambaye alishusha kioo baada ya kumuona..

"Aretha eeh" akauliza dereva, Aretha akamuitikia na kuingia kwenye gari kiti cha nyuma. Wakaondoka.

Njiani Aretha akaamua kumpigia Edrian baada ya kuona ukimya ulizidi kwenye simu yake. Simu ya Edrian ikaita kwa muda mpaka ikakata. Aretha akajawa na wasi wasi akajilaumu sababu hakupata nafasi ya kumuuliza kama alifika salama au la! Akiwa kwenye mawazo hayo, mara simu yake ikaita na alipotazama akapokea kwa haraka

"Rian" akaita

Upande wa pili Ed alikuwa ametoka bafuni kuoga, taa ya simu yake ilimulika mulika kuonesha kuna ujumbe au simu ambayo haikupokelewa. Mara aliposhtuka kitandani alielekea moja kwa moja bafuni kuondoa uchovu wa usingizi aliokuwa nao

Alipoona ni Aretha aliyempigia, akampigia mara hiyo hiyo huku akielekea kuketi kwenye kochi

Kabla simu haijaita sana tayari alisikia sauti ya Aretha ikimuita, akatabasamu

"Habari ya asubuhi princess" akamsalimia baada ya kusikia namna alivyomwita kama mtu mwenye wasi wasi

"Aaah salama Rian... samahani sana.. Mungu wangu...aaah hivi ulifika salama?" Wasi wake ulikuwa wazi katika mtetemo wa sauti yake!

"Niko salama Retha, wewe je, umelala vyema" Edrian akatabasamu mara alipokumbuka namna Aretha alituliakwenye mikono yake na namna alivyosema "I love you Rian" akiwa katika usingizi mzito...

"

Nimeamka salama Rian" Aretha sasa sauti yake ilianza kurudi kawaida, lakini ndani yake alitamani amuulize alifikaje chumbani.

"Uko barabarani?" Edrian akauliza baada ya kusikia kelele za magari barabarani..

Aretha akampa maelezo ya namna Victoria alivyoweka ratiba hii.

"Nitakuja kukufuata!" Edrian akamwambia Aretha japokuwa hakumaanisha kweli, lakini Aretha angekubali angeenda

"Hapana Rian, naomba upumzike, uje kama ulivyoahidi" Aretha akamsihi Ed

"Oooh basi sawa princess nadhani una mambo yako na V hamtaki niyafahamu" Edrian akajifanya kulalamika

"No eewh Rian simaanishi hivyo naomba unielewe" Aretha akajaribu kumuelewesha japokuwa Ed alifurahi tu kumsikia anavyomjali.