Ulipofika muda wa jioni Edrian aliondoka na Li kuelekea nyumbani. Njiani alimtumia Aretha meseji kumjulisha kuwa alimaliza mkutano na alikuwa akielekea nyumbani kupumzika. Mara alipotuma ujumbe ulijibiwa kwa haraka na Aretha...
"Hongera sana Rian. Naweza kupiga nikusikie?" Ujumbe wa Aretha ukamfanya Edrian atabasamu kwa furaha.
Linus aliyekuwa akiendesha gari alipoona tabasamu usoni kwa kaka yake, naye akatabasamu kitu kilichomfanya Edrian kumshangaa na kumhoji
"Vipi mbona unatabasamu"
Li akashindwa kujizuia akacheka, "Hahahha bro nimefanya kile ulichofanya, kuna shida hapo?"
Edrian akamwangalia Li akatikisa kichwa na kurudi kwenye simu yake ambapo hakujibu meseji ya Aretha akampigia simu,
"Hello princess" akamuita Aretha upande wa pili mara simu ilipo pokelewa huku akimwangalia Li ambaye alijaribu kubana kicheko kilichokuwa karibu kumponyoka.
Akaongea na Aretha kwa dakika chache akijibu maswali ya Aretha ambaye alionekana kujali. Akakubaliana nae atampitia baadae kuelekea Southern Pole kupeleka picha kwa ajili ya onesho lake na Beruya.
Akacheka taratibu mara aliposikia msisitizo wa Aretha kuwa akalale walau masaa matatu.
"Sawa Retha, nitafanya kama ulivyosema" wakaagana na akakata simu.
Li aliyekuwa amejibana muda wote wa maongezi akaachia kicheko, "my brother, my brother"
Edrian akaguna na kugeukia dirishani huku akitabasamu.
"Huyu Aretha aliyebatizwa Retha ana miujiza ya haraka sana" Li akamwambia Edrian ambaye sasa aligeuka na kumwangalia
"Miujiza tena!" Akauliza kwa mshangao
"Eeeh bro, amemgeuza mtu asiyependa maisha yake kuwa wazi hadi kuwa mtu asiye na hofu watu wajue au wasijue daaah"
"Hahahahha Li, mbona unanishambulia mapema sana" akacheka Edrian
"Hujui tu siku kama hizi zinavyotupa furaha kila tunapokuona" Li akamwambia
"Kweli eeh?" Akauliza Edrian
"Kila mara tulihofia maisha yako ya mapenzi na hasa mama" sasa kulikuwa na hisia za kumaanisha kile alichokiongea Li
Edrian akamsikiliza mdogo wake kisha akauliza, "Li kwani nilipokuwa na Joselyn kuna tofauti yoyote na Retha?"
"Mmmmhm.....Bro unataka nikwambie ukweli?" Li akamuuliza kaka yake
"Eeehhhhm" akaitika Ed
"Tofauti ya wakati ule na sasa sio kubwa ila athari yake ni rahisi kuonekana. Sio kwamba Joselyn hakufanya tuone tofauti la hasha! Bro una 'enjoy' na hutaki kujificha kabisa, umekuwa na furaha"
"Hahahhaa kumbe naonekana eeeh!" Edrian akacheka
"Sana bro hahaha" Li akajiunga na kaka yake kucheka
Safari yao ikaishia nyumbani ambapo alikutana na taarifa ya mlinzi iliyomfanya abadilike
"Kwa hiyo Joselyn alikuja hapa?" Li akauliza baada ya kuona Edrian amekaa kimya
"Ndio ila hakuingia ndani, kama mkuu alivyonielekeza nilimzuia." Mlinzi akampa maelezo Li wakati huo Edrian akaondoka pasipo kusema neno jingine.
Baada ya Li kumsikiliza mlinzi naye akaondoka kuelekea ndani akitaraji kumkuta Ed pale sebuleni ili kuongea nae, lakini hakumkuta.
Akaelekea chumbani kwake na kumgongea, Edrian akafungua akiwa ametoa shati kuonesha alikuwa katika maandalio ya kuingia bafuni
"Vipi bro uko poa?" Li alimuuliza japo wasi wasi wake ulianza kumuisha sababu sura yake ilionesha kutokuwa na hasira
"Niko poa Li, nataka nilale kidogo. Vipi una shida?" Edrian akauliza huku tabasamu lake likiwa wazi usoni
Li akacheka taratibu na kuanza kuondoka, "Sina shida bro, nilikuwa naangalia kama unafuata ushauri uliopewa. Pumzika sasa"
Edrian akarudi chumbani akicheka, "Am not allowing you to change my mood" akawaza huku akielekea bafuni.
Baada ya dakika 15 alikuwa tayari kitandani akiutafuta usingizi, akachukua simu yake na kumtumia ujumbe Aretha huku akitabasamu.
"Nalala sasa, i love you Retha"
Akasubiri sekunde chache, kabla hajapitiwa na usingizi ujumbe ukaingia kwenye simu yake, akatabasamu na kusoma
"Usingizi mwema Rian. Nitakusubiri mara ukiamka"
Taratibu akapitiwa na usingizi
**********
Beruya alishangazwa na wageni wa ghafla waliomtembelea pale ukumbini,
"Samahani Bei, najua uko kwenye "Final touches" za onesho, Huyu anaitwa Joselyn ni rafiki wa Mr Simunge anahitaji msaada wako" Melissa akamwambia Beruya