Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 144 - NOT YOUR ENEMY

Chapter 144 - NOT YOUR ENEMY

"Kuna maadui gani wanakutafuta?" Akamuuliza

"Maadui? Wa wapi hao Retha" akauliza Ed ambaye sauti yake ilikuwa na mshangao mkubwa

Aretha alipoona namna Edrian alivyoshangaa akawa kama ameshikwa na kigugumizi

"Retha unawaza nini" Edrian akamuuliza baada ya kuona kimya kimetawala kidogo

"Aaaah. .naona unavyonisisitiza kuwa mwangalifu unanipa maswali Rian" Aretha akajitahidi kujieleza

"Oooh ni kawaida kukutaka uchukue tahadhari, nilikwambia tangu mwanzo kuwa nina maadui ambao wananich_" kabla ya kuendelea sauti ya mlango uliogongwa upande wa Edrian ulikatisha maongezi yaliyoendelea, alipotaka kuendelea Aretha akawahi kumwambia

"Rian tutaongea hata baadae, tafadhali endelea na majukumu yako" Aretha akamsihi

"Retha ni mimi ndio nimepiga simu hahaha" Edrian akamtania huku akimruhusu aliyegonga kuingia

"Sawa Rian lakini uko kazini" Aretha akajitetea

"Nitakupigia baadae Retha. Love you" akakata simu bila kusubiri jibu la Aretha.

Aretha akatabasamu baada ya Edrian kupata simu, "afadhali amenisikiliza"

Kabla ya kuendelea na kupanga vifaa vyake simu yake ikaita tena, alikuwa ni Derrick aliyempigia. Akapokea.

******************

"Nitakupigia baadae Retha. Love you" Edrian akakata simu bila kusubiri jibu la Aretha na akageuza vyema kiti chake kumwangalia mgeni aliyesimama mbele ya meza yake.

"Samahani Mr Simunge, sikukusudia kukatisha maongezi yako" akasema Renatha asijue akae au aendelee kusimama

"Hujayakatisha Renatha, ni mimi nimekata simu ilinikusikilize." Edrian akamwangalia akiwa tayari kumsikiliza

Renatha ambaye kwanza alishtushwa na kumsikia Edrian akiita jina la Retha na zaidi sana kusikia akimwambia "love you". Alitamani kumjua huyo mtu ni nani maana mpaka sasa alimfahamu Joselyn na vituko vyake.

"Renatha" Edrian akamtoa kwenye mawazo yake

"Aaahm" Renatha akashtuka

"Samahani, Mr Simunge nimepata taarifa mna mkutano wa bodi" Renatha akazungumza huku akisogea kilipo kiti akae..

"Mmmmm" Edrian akaguna na macho yake yakamwangalia kwa ukali Renatha kiasi cha kumfanya mwili wake kusisimka

"Àaaaaah inaonekana haukupenda niju__"

"Renatha" Edrian akamkatisha

Renatha alipomwangalia Edrian baada ya kuita jina lake, kidogo ageuke na kukimbia

"Yes boss" akaitika kwa kukaza sauti

"Unataka nikusaidie nini?" Edrian akauliza kwa sura ya kikazi ambayo ilimfanya Renatha ashikwe na kigugumizi

"Mr Simunge, ninaweza kupata kibali cha kupitia tathmini ya upatikanaji wa maeneo mapya ya uchimbaji?" Renatha akajikaza na kumwambia Edrian

"Kwa nini?" Akauliza Edrian huku akimkazia macho Renatha ambaye naye hakujaribu hata kupepesa macho ili asionekane kutishwa na hali iliyokuwa mbele yake

"Nafikiri kuna kitu naweza kufaidia SGC" akajibu Renatha

"Kwa nini unataka kutusaidia Renatha?" Akauliza Edrian huku akiweka mikono yake miwili juu ya meza.

"Na kwa nini nisiwasaidie kama ninaona naweza kufanya hivyo?" Renatha akarudisha swali kwa Edrian, akaketi huku akimtazama

Edrian akanyamaza kwa sekunde chache akiendelea kumwangalia Renatha. Akashusha pumzi na kuegama kwenye kiti

"Renatha, why are you here" akamuuliza tena uso wake ukiwa na muonekano ule ule..

"Mr Simunge, nimeomba kuona tathmini ya maeneo mapya mnayoyaandaa kwa ajili ya operasheni. It's a request and not an order sir" Renatha akamjibu

"Hapana, hilo eneo si sehemu ya kazi yako Renatha" Edrian akamwambia

"Basi sawa bosi. Ila ukiona umuhimu wa msaada wangu usisite kunijulisha" Renatha akainuka huku akitabasamu

Edrian akamwangalia sana Renatha akishangaa ni nini hasa kilimsukuma kufikiri juu ya maeneo mapya.

Renatha akapiga hatua kutoka, lakini alipofika mlangoni akageuka na kumwangalia Edrian,

"I am not your enemy boss" akatabasamu na kutoka mle ndani akimuacha Edrian katika kutafakari nini kinaendelea ndani ya binti yule.

"Kwa ujasiri tu nakukubali lakini siwezi kukuamini katika hili" akawaza taratibu Edrian.

Akaendelea na kazi huku akitupia jicho kwenye saa yake, akatabasamu alipokumbuka maneno ya Aretha alipomuuliza kama amekula.

"Japokuwa muda umeenda lakini ngoja nile walau hata matunda" akawaza na kisha akainua simu kumuagiza Loy