Chapter 145 - BM

Aretha aliwasili akiwa na Derrick katika ukumbi Southern Pole,

"Retha, umekataa nisikuite shemeji eeeh?"Derrick akamtania Aretha ambaye aliinama kwa aibu huku akicheka

"Hapana Derrick, niite Aretha au Retha"

"Na wewe unanikataza kama Bro tu!" Derrick akajifanya kukasirika. Maneno haya yakamshtua kidogo Aretha

"Bro?" Akauliza kwa mshangao

Derrick akajibaraguza ili asimtaje Edrian, maana siku waliyotoka kuongea na akina Beruya, kaka yake baadae alimwambia asijaribu kumuita "shem" Aretha.

"Bro Li...hahahha au ulidhani namaanisha Big bro eeh" Derrick akaendelea kumtania

"No... sikumaanisha Ria...Ee..Big bro!" Aretha akashikwa na kigugumizi wakati akijaribu kujitetea

"Hahahha relax Retha, just kidding" Derrick akasema mara walipokaribia mlango wa kuingilia ukumbini.

Macho ya Aretha yalivutiwa tena mandhari safi iliyokuwa mle ndani. Tangu siku ya kwanza alipoingia humu leo aliona kama aotaye ndoto.

"Waaaoooh hii ni nzuri " akasema Aretha ambaye alivutiwa na rangi iliyopakwa now ndani.

"Uzuri wako ni zaidi ya humu ndani" sauti ikamsemesha nyuma yake. Mwanzoni alidhani ni Derrick lakini akashangaa kumuona yule mwanaume ambaye alimuona akiwa na Edrian, wakati wakitoka ukumbini hapo.

"Habari" Aretha akamsalimia huku mashaka yakiumbika moyoni, maneno ya 'usisahau kuwa mwangalifu' yalimiminika akilini mwake

"Salama Aretha, naona umevutiwa na muonekano wa ukumbi au nimekosea?" Akamuuuliza huku akipiga hatua kusimama karibu sana naye, Aretha akapiga hatua kurudi nyuma ili kujihami kama alivyoelekezwa na Edrian

Yule bwana akatabasamu, akanyoosha mkono wake ili kumsalimia Aretha...

"Samahani naona nimeingilia muda wako lakini natamani tusalimiane tu."

Aretha ambaye bado alikuwa katika mshangao akanyoosha mkono na akamsalimia kwa haraka kisha akatoa mkono wake.

"Naitwa BM, unaweza niita Bon" akajitambulisha

"Naweza kujua ulinifahamu vipi?" Aretha akamuuuliza

Lakini kabla ya kujibu Derrick alisogea pale akitokea maliwatoni ambapo alielekea mara tu walipoingia ukumbini mle. Alipoona Aretha akiwa katika mashaka na kurudi nyuma akapiga hatua haraka kuelekea walipokuwa wamesimama!

"Aretha are you okay?" Akamuuliza na kumfanya huyu Bon asimalizie kujibu swali.

Aretha akaitika kwa kutikisa kichwa chake.

Derrick akamgeukia

"Naitwa Derrick, sijui mwenzangu ni nani?"

"Ooooh Derrick Simunge, nimefurahi hatimaye kuonana nawe" Mr Bon kama alivyojitambulisha akaunyoosha mkono wake kumsalimia Derrick ambaye bila kusita alimpa wa kwake na wakasalimia.

"Tulishawahi kuonana?" Akauliza Derrick

"Aaaaah hapana ila niliwahi kusikia baba yangu akiwazungumzia watoto wa marehemu Simunge. Leo nimefurahi kuonana nawe" akajibu

Derrick alipomuangalia alikubali kwamba alikuwa ni mtanashati mwenye mavazi nadhifu ya kuvutia. Alivaa shati ya mikono mifupi iliyokuwa mistari, chini akivaa suruali ya rangi nyeusi. Kwa muonekano alikuwa ni mtu ambaye pesa haikuwa tatizo kwake maana saa aliyovaa, Derrick alifahamu bei yake ingeweza kununua saa tatu za gharama ya kati.

"Nafurahi kuonana nawe japo sijajua jina lako" Derrick akaona amkumbushe ili afahamu walau jina lake

"Ooh samahani niita BM au Bon...oh samahani kuna mahali natakiwa. Kila la kheri Aretha" akaaga kwa haraka akionekana kweli alikuwa anawahi maana aliangalia saa yake

"Retha unamfahamu?" Derrick akamuuliza Aretha ambaye alikuwa kimya muda ule akionesha wazi kupatwa na mawazo

"Aaah hapana, ila nashangaa yeye ananifahamu" akajibu na kuendelea kuangaza macho yake akimtafuta Beruya.

"Oooh basi usihofu. Tutajua tu, huyu Beruya yuko wapi" Derrick akamtia moyo na kwa pamoja waliendelea kuangaza kumtafuta Beruya. Wakauliza mmoja wa msimamizi wa waandaaji,

"Atarudi muda si mrefu kuna dharura mara moja ameitwa ofisini kwake. Mwaweza kumsubiri pale tafadhali" msimamizi akawaelekeza kwenye eneo lililokuwa na meza iliyozungukwa na viti vinne. Wakaelekea kuketi huku Derrick akijaribu kumtania Aretha ili arudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuona kimya kikipita kati yao.

"Derrick" Aretha akaita

"Naam" akaitika Derrick

"Unadhani Ria. .aah samahani Edrian ana maadui wengi?"