Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 143 - UTAFANYA VYEMA

Chapter 143 - UTAFANYA VYEMA

"Retha mbona_"

"Nini kinaendelea mama mbona huniambii" akamuuliza mama yake kwa huzuni

Mama yake akamwangalia Aretha usoni kisha akainama akijaribu kuyazuia machozi yaliyokuwa yakipambana kutoka nje...

"Mwanangu" akaanza kumwelezea huku akiinua uso wake na kumwangalia akaendelea

"Ninakuwa na wasi wasi sababu yaonesha kuna kundi la watu wanatafuta kitu kwa Edrian, na wako tayari kumtumia yeyote au chochote kupata wanachotaka" akamwangalia Aretha kama angeshtuka lakini hakuona hata dalili yoyote ya wasiwasi akaendelea,

"Ninachohofia ni kuwa wasije wakajaribu kutumia ukaribu wako na Edrian na mwisho wakakuweka mtegoni"

Aretha ambaye alikaa kimya akimsikiliza mama yake, akaamua kumuuliza "kwa hiyo mama siku ile nilikukuta kwenye majonzi ni kwa sababu hiyo?"

"Mmmhm...haaa hapana, mbona nilikuwa kawaida" mama yake akasisitiza

"Mama, jambo lolote linalokusumbua huna sababu ya kunyamaza kimya" Aretha akaona vyema amshauri kidogo mama yake

"Kwa kusema kuwa unahofia usalama wangu mama haitoshi kuwa kitu kilichokutoa machozi siku ile.. na mimi sitakulazimisha uniambie." Aretha akasogea alipokaa mama yake akapiga magoti na kumwambia

"Mama, ikiwa nitaondoka, unamaanisha kuwa niachane na Rian. Mama siwezi." Aretha akamwangalia mama yake usoni alipomwambia maneno haya..

"Aaahmmm" mama yake akuguna

"Mama kama niko na Rian, furaha yangu inazidi hiyo hofu." Aretha akaendelea

"Halafu sijui kitu wanachokitafuta kwa Edrian, hawatapata chochote kwangu"

"Retha mwanangu, sio kwamba mimi sioni furaha yako na Edrian, lakini naona kuwa hai na salama ni muhimu zaidi" mama yake akajaribu kumsihi lakini Aretha akainuka na kurudi kuegama kwenye meza

"Mama, kwanza niambie hao watu ni kina nani na wanataka nini. Nitakuelewa ikiwa utanipa maelezo kamili. Mama maelezo yako yanaweza kumsaidia Edrian na ak_" kabla ya kumaliza mama yake akamkatisha

"Retha naomba mazungumzo haya yasitoke hapa. Usimwambie Edrian chochote. Kama umekataa mwanangu siwezi kukulazimisha. Ila kuwa mwangalifu na wanaokuzunguka" Mama akamwambia huku akiinuka tayari kutoka mle ndani

"Lakini mama kwa ni_" Aretha akajaribu kumuuliza mama yake lakini sentensi iliishia hewani

"Hakuna sababu ya kumwambia. Na kwa sababu umekataa ninawajibika zaidi. Endelea na kazi yako mwanangu" hakusubiri tena Aretha aendelee akatoka.

Aretha akashusha pumzi akamwangalia mama yake akiishia mlangoni, "sijui kinaendelea nini, na hao watu ni kina nani na wanataka nini kwa Rian! Nitamuuliza"

Akaendelea kupaweka vyema mezani alipokuwa akipatumia kuchagua picha. Simu yake ikaita, alipoangalia hakusita kupokea huku akitabasamu

"Hellow Rian" akaitikia huku akiegama mezani

"Princess, habari ya mchana" upande wa pili Edrian akamsalimia Aretha

"Safi, umepata 'lunch' Rian?" Akauliza Aretha

"Bado princess, ninamalizia vitu vidogo hapa, nikimaliza nitakula"

"Oooh basi sawa." Aretha akaridhika na maelezo ya Edrian

"Princess, nimepiga nikujulishe baadae sitaweza kuja kukuchukua ila nimeongea na Derrick atak_" Aretha akamkatisha

"Rian..please naweza kwenda mwenyewe hauna_" naye kabla ya kumaliza akakatishwa na Edrian

"Derrick atakuja kukuchukua. Please Retha" Edrian akamsihi kwa sauti ya uchovu

"Basi sawa, nimekuelewa." Aretha akajibu taratibu baada ya kuona sauti ya Edrian ikiwa na hisia za uchovu..

"Umeandaa picha zako?" Edrian akamuuliza

Ndio, ziko tayari" akajibu Aretha.

"Vizuri. Kesho naweza nikashindwa kabisa kukupeleka lakini Derrick atafanya kazi hiyo atakuwa na Charlz" akamuelezea

"Naelewa Rian. Pole kwa uchovu" kwa sauti yenye hisia za kujali Aretha akamwambia

"Asante Retha." Akajibu kukiwa na hisia za furaha!

"Kesho itakuwa siku ndefu lakini naamini utafanya vyema." Akasema Aretha

"Ooooh Asante sana princess. Nitafanya vyema. Usisahau kuwa mwangalifu wakati wote" Edrian akamsisitiza Aretha ambaye msisitizo ule ulimfanya akumbuke kile ambacho dakika chache zilizopita alimaliza kuongea na mama yake.

"Rian" Aretha akamuita Edrian kwa sauti tulivu.

"Niambie princess" Edrian akamuitikia

"Kuna maadui gani wanakutafuta?" Akamuuliza

"Maadui? Wa wapi hao Retha" akauliza Ed.