Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 138 - BEAUTIFUL

Chapter 138 - BEAUTIFUL

"Rian" Aretha akamuita

"Ahmmm" Edrian akaitika.

"Asante kwa kila ulichofanya na unachoendelea kufanya. Siwezi kuzuia furaha ninayoisikia ndani yangu kuona unajali ndoto yangu. Nakuahidi kufanya kila niwezalo kufikia uwezo wa kujisimamia mwenyewe."

Aretha akajieleza kwa ukunjufu wa moyo, huku akijaribu kuyazuia machozi yaliyoanza kujaa kwenye macho yake.

Edrian akatabasamu mkono wake mmoja ukabaki kwenye usukani wa gari huku ule mwingine ukigusa shavu la Aretha ambaye taratibu alilaza uso wake pale.

"Asante Rian"

Hisia za mapenzi zikatawala kati yao, Edrian akijaribu kujizuia kutaka kumkumbatia Aretha.

"Oooh sorry, nimesahau unaendesha" Aretha akashtuka

"Ahmmm" akaitika Edrian kana kwamba aliitwa huku akishukuru Aretha kumwachia, joto la mwili wake lilipanda. Uhitaji wa mwili wake ulikuwa katika vita kutii mamlaka ya utashi wake. Akarudisha mkono kwenye usukani na tayari walikuwa wamekaribia mahali ambapo onesho la Beruya lingefanyika.

Ukumbi wa 'Southern Pole' ulikuwa ndani ya jengo la ghorofa saba. Kwa Edrian kushiriki katika maonesho kama haya hakukuwa sehemu ya ratiba zake lakini alipenda sana sanaa ya uchoraji. Hivyo kumleta kwake Aretha hapa ilikuwa kupata fursa ya kuona maandalizi yanakuwaje na kwa namna gani SGC ingenufaika na ushiriki wake.

"Retha" Edrian alimuita baada ya kuwa ameegesha gari.

Aretha akageuka kumwangalia usoni, "eehmm"

"Can I kiss you please" Edrian akaongea kwa sauti ya kumsihi sana Aretha kwa kuwa alijua unaweza kuwa si wakati mzuri.

Macho ya Aretha yalihama kwa aibu lakini kitu ambacho Edrian alikiomba kilikuwa ni kile alitamani kukifanya muda mfupi uliopita. Akatikisa kichwa kukubali.

Edrian akamshika kidevu Aretha kumfanya amwangalie machoni.

"Retha, I want to see the best of you" akasema kwa sauti ya chini huku akiinama taratibu kuelekea kwenye mdomo wa Aretha. Akampa busu jepesi kwenye shavu lake. Akafanya hivyo kwenye shavu la pili, kisha kwenye paji la uso, akarudi kwenye mdomo. Akaibusu midomo ya Aretha taratibu hadi taratibu ilipogeuka kuwa busu zito. Aretha akampa ushirikiano wa kutosha na kwa pamoja wakajikuta katika mahaba mazito hadi Edrian alivyoachia kupeana nafasi ya kupumua.

Aretha akageuka upande wa pili, akajaribu kujiweka vyema maana nywele zilikuwa zimevurugika kidogo!

"Naomba nikuweke vizuri princess. Am sorry" Edrian akamuomba Aretha baada ya kuona akihangaika..

"Aaah" Aretha akashtuka lakini alikuwa amechelewa maana Edrian alishatoa kitana kwenye sehemu ya kuwekea simu na kutaka kumchana.

"Rian naweza kujiwe_" akajaribu kumuomba ampe kitana lakini Edrian hakumpa akaendelea kuuelekeza mkono kwenye kichwa chake ili apate kumchana.

"Please" Edrian akamwangalia na macho kama mtoto anayeomba kitu

Aretha akatulia kumruhusu amuweke vizuri japo kwa aibu nyingi. Alipomaliza akatabasamu

"You are beautiful Retha" akarudisha kitana.

"Eehm..asante"

Wakashuka na kuelekea sehemu ya kuingilia ambapo kulikuwa na eneo la mapokezi. Edrian alihakikisha hamuachi Aretha hata kwa hatua moja. Watu wachache waliokuwepo pale chini waliwaangalia huku baadhi yao wakimsalimu baada ya kumfahamu.

Baada ya kupewa maelekezo waliingia kwenye lifti iliyowapeleka mpaka ghorofa ya sita. Wakaelekea mlango wa kuingilia ukumbini hapo. Kulikuwa na matengenezo yaliyoendelea ukumbini pale kama sehemu ya maandalizi.

"Oooh Mr Simunge, Aretha karibuni" sauti ya Beruya iliwaondoa kwenye fikira zilizokuwa zikipita kwenye kichwa cha kila mmoja.

"Karibuni sana" akanyoosha mkono kumsalimia Edrian na kisha akaelekeza kwa Aretha.

"Meneja wangu amekuja ofisini kwako" Beruya akamwambia Edrian huku akiwaelekeza mahali kulikuwa na viti na meza

"Atahudumiwa vyema bila shaka" akajibu Edrian

Wakaketi, wakati huo Beruya akawakaribisha vinywaji vilivyokuwa kwenye kijokofu kidogo kilichokuwa karibu na meza.

"Aretha tafadhali jione kuwa uko mahali pako ulipopazoe" akamwambia baada ya kumuona Aretha akiwa na wasi wasi usoni..

"Aaah asante sana Beruya, niko vizuri" Aretha akamjibu

"Naona matengenezo yanaendelea" Edrian akamwambia Beruya ambaye alikubali na kumpa maelezo.