Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 139 - HISIA HIZI

Chapter 139 - HISIA HIZI

Maelekezo ya Beruya kwa Aretha yalienda vyema kabisa, kuanzia kwenye namna ya kuchagua picha kwa ajili ya onesho, lakini pia linapokuja suala la kuelezea msukumo nyuma ya picha. Aretha alijifunza na mara zote Beruya alimpa nafasi ya kuuliza maswali.

Edrian aliwaangalia akiwa ameketi kwenye ile meza ambayo Beruya aliwakaribisha. Aliona vyema kumpa uhuru wa kujifunza Aretha. Macho yake yalikuwa kwenye simu yake akiangalia na kutabasamu,

"She is so beautiful, na hajui kabisa." Aliwaza Edrian, hakujua muda gani Aretha alisimama karibu nae

"Rian" sauti ya Aretha ikamshtua Edrian akaweka simu mezani akamuangalia usoni na kisha kwenye simu yake

Aretha macho yake yalipoangalia simu ya Edrian aliyoiweka mezani akakutana na picha yake mwenyewe akiwa katika moja ya magauni aliyopima dukani kwa Victoria. Akayarudisha macho kwa Edrian ambaye alikuwa katika kutabasamu

"Sorry Retha, nilitamani kuona unapendezaje katika magauni uliyo chagua, nilimuomba V anitumie kila muonekano wako."

Aretha akatabasamu pasipo kusema chochote akaketi kiti kilichokuwa pembeni ya Edrian,

"Nilitamani kuja....lakini nilitaka uwe na uhuru wa kuchagua upendacho pasipo mimi kuingilia uhuru wako. Please R_"

"Rian" Aretha akamkatisha huku akiwa anaangalia vidole vyake...

"Eeehm" akaitika

"Unadhani ninaweza kuwa kama Beruya?" Akauliza

"Aaah" Edrian hakuelewa ni kwa sababu gani Aretha alibadilisha mada waliyokuwa wakijadili. Akashukuru moyoni maana alihisi kumkosea Aretha

"Unahitaji kuwa wewe Aretha na sio Beruya. Ni muhimu ukawa wewe zaidi" akageuka kumuona Aretha ambaye mikono yake ilikuwa ikivifinya vidole vyake

"Retha, usiogope. Utakapoanza hatua ya kwanza utaona wepesi wa kupiga ile ya pili. Wewe ndio kwanza unaanza huwezi kuwa na ubora alionao Beruya. Lakini nataka nikwambie kama mwenyewe Beruya amekuamini, unacho kipaji." Edrian akamwambia

"Mmmhhhmm" Aretha akashusha pumzi na kusema

"Kwa kuwa una imani nami nitajitahidi kufanya navyoweza, ni mambo mageni kwangu ambaye nimezoea kuwa ndani."

"Retha relax" Edrian akamwambia huku mkono wake ukimgusa begani na wakati huo Beruya alirudi kuungana nao

"Oooh samahani Aretha nilikuwa nawapa maelekezo timu yangu ya maandalizi ndio maana imenichelewesha kujiunga nami" Beruya akaongea huku akiuangalia mkono wa Edrian uliokuwa begani kwa Aretha

"Hapana shida Beruya." Akajibu Aretha huku macho yake yakirudi kwa Edrian kumpa ishara ya ule mkono auondoe lakini ndio kwanza akampapasa kumuondolea wasi wasi.

"Nadhani usichukue kila kitu kuwa kigumu kwako Aretha, hebu kichukulie kama ni ujuzi mpya na nzuri zaidi furahia kuanza" Beruya akamwambia huku akiketi.

"Asante sana" Aretha akashukuru

"Bado mnaendelea?" Akauliza Edrian huku akitoa mkono wake begani

"Aah nadhani kwa leo imetosha" Beruya akamjibu

"Na kutokea hapa unadhani mtaonana tena lini?"

"Nadhani tuonane tena ijumaa. Sehemu kubwa ya matengenezo itakuwa tayari. Jumapili tutaleta picha kwa ajili ya kuzibandika mahali pake" akatoa maelekezo

"Asante sana Beruya. Nitafanyia kazi maelekezo yote" Aretha akashukuru na kisha akasimama baada ya kumuona Edrian akifanya hivyo.

"Asante Beruya, mchango wa SGC uko njiani kukufikia" akajibu Edrian

Wakaagana na Beruya ambaye akawasindikiza mpaka kwenye walipoingia kwenye lifti.

"Asante Rian, sijui nitakulipa nini" Aretha akamwambia Edrian mara tu mlango wa lifti ulipofunga.

"Usinilipe bali nifanye nione hatujakosea hatua hii" Edrian akamjibu na kisha akamshika mkono wake, mikono wao ilipogusana wote wawili wakaangaliana machoni..

"Nitafanya kila niwezalo" Aretha akamwambia

Edrian ambaye alisikia kile alichosema Aretha alikuwa katika mawazo yake binafsi. Alitamani kumkumbatia Aretha kwa kuwa walikuwa peke yao ndani ya lifti lakini alihofia iwapo angeweza kujizuia..

"Hizi hisia mbona hazinipi kupumua" akawaza asijue wakati huo aliinama uso wake hata kumkaribia Aretha ambaye alifumba macho akihisi Edrian alitaka kumbusu.

Alipokaribia kiasi cha pua zao kugusana akashtuka, na wakati huo lifti ilifika sakafu ya kwanza ambapo walitakiwa kushuka.

Akageuka na kuangalia mlango uliofunguka.