Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 137 - MPENZI FANYA

Chapter 137 - MPENZI FANYA

Mgahawa wa Lunch Hour kama kawaida yake uliwaridhisha wateja wake kwa kuwapa ladha tofauti ya vyakula.

"Big brother nitakuwa nakula hapa aisee, chakula kitamu mno" Coletha akamwambia kaka yake wakati akinawa mikono yake baada ya kumaliza kula...

"Na nani atupikie nyumbani? Napenda chakula chako" Edrian akamwambia

"Hahaha Zainabu yupo! Kaka Li huwa anamsifia kila akipika" Coletha akajitetea

Li aliyekuwa akikausha mikono yake akamwangalia Coletha, "Sababu anajua kupika kuliko hata wewe"

"Haaaaa wakati mimi nimefundisha karibia vyakula vyote anavyopika!"

"Li muache mdogo wangu, mpishi wa familia" Edrian akamtetea

Li akatabasamu na kunyoosha mikono juu. Aretha aliwafurahia ndugu hawa kwa namna walivyokuwa wakitaniana.

Wakatoka nje pamoja, walipofika nje Li akamshika mkono Coletha wakaenda pembeni kwa sekunde chache kisha wakarudi.

"Bro nyie tangulieni, sisi tutachukua usafiri mwingine kwa ajili ya huyu mdada arudi nyumbani." Li akamwambia Edrian ambaye akitabasamu kumpa ishara ya kukubaliana naye.

Aretha akashtuka na kumwangalia Coletha "Kwani si tunaweza kupita nyumbani"

Edrian akamsogelea Aretha kisha akasema "unatakiwa kwa Beruya Retha"

Aretha akaangalia simu yake, "ooh, ila bado dakika zipo za ku_"

"Aretha wala usihofu, mimi nitafika salama kuna comrade wa usafiri hapa!" Coletha akamhakikishia

Wakaagana huku Aretha na Edrian wakiingia kwenye gari na kuwaacha Li na Coletha wakisubiri usafiri ambao tayari waliuagiza kwa njia ya simu.

"Relax Retha.. watakuwa salama tu wamezoea mbona" Edrian akamwambia baada ya kuona Aretha akiwaangalia sana

"Sawa Rian" akaitikia.

"Pia nilitaka tubaki wawili ili tuongee, najua unataka kuniuliza"

"Ahaaa oooh kweli Rian" Aretha akamjibu.

Edrian akatabasamu, hakuondoa gari akisubiri ndugu zake wafuatwe na usafiri waliouita.

"Sawa Princess" akageuka nusu ili amuangalie vyema usoni Aretha

"Rian" Aretha akaita akijaribu kuyakwepa macho ya Ed yaliyomwangalia

"Nakusikiliza my princess" Edrian akajibu kwa utani akiinama kidogo kama afanyavyo mtu mbele ya mfalme

Aretha akaguna kwa aibu, "Kwa nini umenipa pesa nyingi ambazo sijui nitazifanyia nini Rian?"

Kulionesha dalili za mashaka usoni kwa Aretha, Edrian naye akashangaa inawezekanaje mtu asijue kitu cha kufanya ikiwa ana pesa?

Edrian akawa kimya kwa sekunde chache akimfikiria Aretha na swali lake, kabla hajajibu akawaona kina Coletha wakiingia kwenye gari.

"Rian" Aretha akamuita tena..

"Oooh sorry princess" Edrian akaomba radhi kisha akaendelea na kujibu swali aliloulizwa..

"Retha, una ndoto gani kuhusu picha unazochora?"

"Mhhh, aaah natamani picha zangu ziwe kwenye nyumba ya kila mtu kuwapa faraja" akajibu Aretha na kuinua tena uso wake kumwangalia Edrian

"Vyema. Utafanyaje ili hizo picha zifike kwa kila nyumba?" akauliza Edrian huku akiwasha gari waondoke maana Aretha alitakiwa kwenye maandalizi ya Beruya.

"Aaaahm...nitaziuza" akajibu Aretha

"Utaziuzaje?" Akauliza Ed akionesha kwa kiasi gani alitaka kujua

"Ooohhh bado sijajua Rian ila naamini nitaziuza" akamjibu kwa sauti dhaifu

"Tunahitaji kuwa na mkakati Retha. Na mwisho wa mipango yote ni uhitaji wa fedha" akanyamaza kidogo huku akiangalia magari yaliyosimama kwenye taa barabarani

Aretha aliposikia maneno hayo, moyo wake ukajisikia raha.

"Hizo pesa zitafanya hiyo mipango ifanikiwe. Hebu ione kuwa ni fursa ya kutimiza ndoto yako. Utahitaji kuwa na duka utakalouza hizo picha. Ukifanikiwa kuandaa Onesho lako utahitaji pesa princess. Mimi napenda kupanga mambo kutokea hatua za awali. Umenielewa Retha?" Akauliza Edrian akirudisha macho kwa Aretha kisha barabarani

Aretha akamwangalia pia, "ndio Rian"

Edrian akatabasamu, "nina ruhusa ya kukuondoa kwenye unufaika pia. Nitafanya hivyo nitakapoona unaweza kutengeneza kipato cha kuendesha sanaa yako. Kwa sasa tafadhali mpenzi fanya kile unatakiwa kufanya bila kuwa na shaka. Nitafurahi ukiandaa mpango wako tukauangalia na Derrick ili kuona utawezekanaje"

Aretha alijaa furaha kuu, akamwangalia Edrian kwa macho ambayo mtoto mdogo humwangalia mzazi wake anapompa zawadi nzuri.

"Rian" Aretha akamuita