Joselyn akasonya "Hivi Aretha unadhani utakaa na Ed, atakuacha 'soon', furahia hivyo vinguo unapata" akamtupia maneno Aretha ambaye alinyamaza kimya muda wote huo
"Eeeshhh we Lyn umekuja kutaka shari eeeh" Coletha akapiga hatua kuelekea aliposimama Lyn lakini mkono wa V ukamzuia
"Usifanye hivyo tafadhali" V akamwambia Coletha ambaye alimsikia na kurudi nyuma..
"Na wewe unafurahia ushenzi wa kaka yako, ila kuleni raha kwa muda na_"
"Joselyn tafadhali" V akamkatisha, "sitarajii malumbano kwenye eneo langu la biashara"
"Hahaha V, hujui ni mtu wa namna gani huyo msichana unayemsaidia, utapata hasara kumruhusu aje humu ndani" Joselyn akaongea huku akipunga mkono hewani na kuondoka taratibu
"Samahani sana Aretha kwa hiki ambacho kimetokea. Nakuomba sana unisemee vyema kwa Edrian" V akamwambia Aretha ambaye sasa alikuwa na mshangao wa wazi kumuona dada mrembo mwenye utajiri akimsihi.
Akamshika mkono "dada V usijali, umenisaidia hata hivyo. Nadhani hupendi ugomvi kama nilivyo mimi. Tafadhali usiniwazie vinginevyo"
V akaachia tabasamu kisha akamwangalia Coletha ambaye alikuwa kwenye simu yake, "Mdogo wangu naomba mnisitiri eeeh, namjua Edrian linapokuja suala la mteja"
"Aaah...Da V usijali ila kaka hawezi kukulaumu wewe umefanya kwa sehemu yako" akasema Coletha huku akitabasamu na wakati huo akaandika ujumbe kwenye simu yake.
Walipomaliza mhudumu akabeba nguo na V akawasindikiza mpaka kwenye lifti huku akiwapa kadi yake ya biashara.
"Aretha, nitakuwepo kwenye onesho natamani kuona picha zako."
"Oooh dada V asante nitafurahi kukuona" Aretha alishukuru kwa ukunjufu wa moyo
"Da V, Asante sana" Coletha akamuaga.
Wakashuka mpaka chini huku Coletha akimjulisha kaka yake wako chini tayari. Baada ya muda wakaungana nao huku mhudumu akiweka vyema mizigo yao kwenye gari.
"Sasa nadhani kila mtu ana njaa tunaweza kwenda kula" Edrian akasema huku akimuangalia Aretha kwenye kioo ambaye alikuwa kimya tangu walipoingia kwenye gari.
Linus alikuwa akimtupia jicho mara kwa mara, uvumilivu ukamshinda akauliza, "Aretha are you okay?"
Edrian ambaye muda wote alikuwa akitamani kumuuliza lakini aliona ingekuwa ngumu kwa Aretha kujieleza.
"Aaah haha am okay" Aretha akashtuka na kumjibu Li...
"Coletha kuna jambo lilitokea huko ndani nimuulize V, au aliwa_"
"No Rian niko okay kabisa. Ni vile nimechoka tu, kupima nguo ni kazi kumbe!"
Li aliposikia hivi akatabasamu kwa furaha "kweli ni kazi Aretha ndio maana mimi nikitaka nguo nampa vipimo tu nitaikuta nyumbani"
Coletha aliposikia Li akichangia akashusha pumzi. Akakumbuka alimtumia ujumbe alipomuona Lyn, lakini aliposikia maombi ya V akaharakisha kumwambia kaka yake asimwambie Edrian.
Edrian aliyekuwa akiwasikiliza wote akarudisha macho yake kwenye simu akaanza kumpigia Victoria
Aretha alipoona Ed akipiga "Rian naomba simu yako mara moja nimekumbuka kumwambia mama nitachelewa"
"Aaaah" Ed akashangaa na wote walishangaa
"Please" Edrian akatabasamu akampatia simu yake
"Big bro ya kwangu mimi sijajaza muda wa maongezi" Coletha akamwambia kaka yake
Li alijaribu kujizuia kicheko chepesi ambacho kilimbana kufuatia kitendo kile cha Aretha kujaribu kumficha Edrian ukweli kwamba Joselyn alikuwepo dukani kwa V.
Aretha akapiga simu kwa mama yake, sasa uso wake ukajawa na soni ghafla baada ya kuona jina ambalo Edrian aliandika kwenye simu yake "Mama Yangu". Akaongea na simu ambapo mama yake upande wa pili alishangaa Aretha akimtaaarifu kitu ambacho alishamwambia wakati akitoka nyumbani. Zaidi sana Aretha hakujua kuwa Edrian alishaongea na mama yake kuhusu maandalizi ya Onesho atakaloshiriki Aretha.
Baada ya kumaliza, akamrudishia Edrian simu ambaye alipoipokea akatabasamu zaidi. Alijua kuna kitu kimeendelea na hakujulishwa kwa kuwa alijua kabisa kuwa Aretha alimuaga mama yake kuwa angechelewa. Aliamua kujiunga nao kucheza mchezo waliouanzisha huku akiona raha kwa namna ambayo Aretha alijaribu kuficha.
"Tutakula hapa Lunch Hour" Edrian hatimaye akaongea wakati huo gari iliingia eneo la maegesho ya magari kwenye mgahawa huu maarufu.
Muda huu hakukuwa na watu wengi.