Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 134 - INALETA RAHA

Chapter 134 - INALETA RAHA

Wakashuka kwenye gari na Edrian akawaongoza mpaka mlango wa kuingilia ulipokuwa kisha akamsogeza kwa pembeni Aretha

"Retha naomba uwe huru kuchagua kile unachoweza kuvaa. Usilazimishwe na yoyote. Unahitaji nguo kwa ajili ya onesho la jumapili ndio maana nimekuleta hapa. Watakupa seti nzima ya muonekano wako wa jumapili. Please relax." akamwambia Aretha ambaye macho yake hayakubanduka usoni kwa Edrian.

"Rian unafanya zaidi, hii si sawa nit_"

"Sshhhhh, usiseme hivyo Princess, nitakuelekeza kwa nini ila kwa sasa 'focus' kwenye tukio la jumapili. Unahitaji kuandaa muonekano wako kabla maandalizi hayajakumeza" Edrian akaongea huku akimshika bega Aretha

"Okay. Naomba nilipe kwa kutumia kadi hii" Aretha akamsihi

"No, princess niruhusu leo nilipie na_"

"Lakini Rian umesh_"

"Big brother" Sauti ya Coletha ikawakatisha

"Ameshafika" akawajulisha

Edrian akamgeuza Aretha akiwa amemshika mabegani..

"Nendeni princess. Usisahau chagua kile unataka na usilazimishwe"

Edrian akasalimiana na yule aliyeagizwa kuwachukua kisha akamshika mkono Coletha na kumnong'oneza sikioni na kumfanya mdogo wake amwangalie usoni na kuitikia kwa upole. Akawaacha wakaondoka na yeye akarudi kwenye gari,

"Bro, am sorry lakini nashawishika kusema unafanya vitu vya kunishangaza leo."

"Mmh kweli Li?" Akashtuka Ed na kumwangalia Li

"Hahaha haya mambo ya Brian naona yanaanza na kwako!" Akacheka taratibu Li

"Hahahhaha no way Li. Natumia tu uungwana" akajitetea Edrian kabla ya kuangalia simu yake na kupiga namba..

"V, she is there. Tafadhali kumbuka uchaguzi niliokupa." Edrian akaongea huku upande wa pili ukijibu, kisha akaendelea

"Basi sawa, niko kwenye mtandao watakachochagua nitalipia hapa."

"Asante V" akamaliza Edrian

Li alikuwa akitabasamu macho yake yakimwangalia kaka yake. Edrian alipomaliza kuongea na simu macho yake yakakutana na yale ya Li ambaye alikuwa akitabasamu

"Vipi Li mbona umeniangalia hivyo?" Akauliza Edrian

"Hehehehe sasa nimepata sababu ya kuendelea na useja wangu haaaa"

"Why" Edrian akamuuliza Li kwa dhati

"Umekuwa kama Brian bro, unatafuta hadi nguo ya kuvaa Aretha hahaha, Brian sasa hivi yuko sokoni anatafuta vitunguu"

"Hahahhahahha Li acha, Bri mbona anajua hadi kuosha vyombo teh teh" Edrian akacheka kweli

"Seriously!, you guys are no longer the ones I used to know hehhehe" Li akacheka

"Relax Li, kumsaidia mtu kutimiza ndoto yake inaleta raha. Najisikia hivyo mara zote ninapofanya kitu kwa mtu ambaye najua asingeweza pekee. Kama vile tunafanya kwa watoto wetu pale Peace House" akajielezea Edrian

"Hahaha haya bro. Umesema kuna mahali tunaenda?" Akauliza Li

"Hakuna mahali Li, nataka tuongelee mambo ya biashara huko Exchange Tower na kama umekamilisha ripoti za Jumamosi"

"Ooooh, sawa." Li akaitikia.

"Twende tuwasubiri hapo mgahawani nimemwambia Coletha wakimaliza anijulishe ni zoezi fupi tu"

Victoria Style and Designs ni kampuni ya ubunifu na mitindo ambayo kwa A-Town ilichukuliwa kuwa namba moja kwa kubuni na kuuza nguo ghali sana. Ubunifu wao ulikulibalika sana na bidhaa zao zilitumiwa na watu maarufu wenye majina. Mfano ungevaa nguo yenye kubuniwa na kushonwa na Victoria Style and Designs, ilikuwa rahisi kabisa mtu kutambua ilitoka kwao.

Aretha na Coletha walimfuata kijana yule aliyeagizwa kuwachukua. Kwa Coletha naye ilikuwa mara ya kwanza kuingia kwenye jengo hili, japokuwa aliwahi kuvaa gauni lililobuniwa na kuandaliwa na VSD ambalo alioewa zawadi na Edrian.

Wote walikuwa wakiangalia kwa mshangao mpangilio uliokuwepo. Waliposhuka kwenye lifti ghorofa ya tano, walikuwa kwenye duka kubwa la nguo la Victoria.

Coletha akamshika mkono Aretha huku akiubana kwa nguvu

"Eeeehwwww tamaa isinipate kabisa, eee Mungu nisaidie"

Aretha akatabasamu aliposikia maneno ya Coletha mara walipoona nguo zilizokuwa dukani mle.

"Karibuni sana" Walipokelewa na msichana mrefu wastani ambaye alikuwa kwa mfano wa mwanamitindo kwa namna alivyovaa na kutembea.

"Asante" wakasema wote kwa pamoja.

"Aretha" Akauliza huku akihamisha macho kati yao kujua Aretha ni yupi

"Mimi hapa" akaitika Aretha.

"Ooooh...karibu."