Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 131 - NGUVU YA UPENDO

Chapter 131 - NGUVU YA UPENDO

"Unampenda eeeh" Coletha akamwambia kwa sauti ya chini huku akisogea mbali na sikio la Aretha baada ya kumuona namna alivyoshtuka.

Aretha akainama kukwepa uso wa Coletha ambao ulijaa tabasamu la furaha, akashukuru kwa mlango kufunguliwa na Edrian akawa wa kwanza kuingia.

"Big brother!" Coletha akaita kutokea kiti cha nyuma walipokaa na Aretha

"Nambie baby sisy" Edrian alijibu na kugeuka

"Tuanzie kwenye chakula nina njaa si hata wewe Aretha" akasema Coletha huku akimuingiza na Aretha kwenye maongezi

Edrian akajaribu kumwangalia Aretha ambaye alikaa nyuma ya kiti alichokalia yeye. Akapata taabu kumuona vyema lakini akaendelea

"Kweli Retha, nawe una njaa?" Akauliza huku akiangalia kwenye kioo kumuona anavyojibu

"Aaaahm" hakuelewa aseme ana njaa au la maana moyoni alikuwa na shauku ya kutaka kujua nini Edrian alitaka kufanya. Hakumwambia kusudi la safari hii, ila aliamini kuna kitu cha msingi maana isingekuwa rahisi kumwambia aombe ruhusa ya kukosa vipindi chuoni.

"Coletha wewe umetoka nyumbani muda si mrefu hiyo njaa imetoka wapi?" Akauliza Ed akihamisha swali kutoka kwa Aretha maana alijua kilikuwa gumu kwake kujibu

Li akacheka taratibu na kuondoa gari, "Bro muache aendelee na hii tabia ya kupenda kula kula atamfanana shangazi Latty hahah"

"Hapana sitaki kabisa kunifananisha mwili wangu na wa shangazi aiiii" Coletha akalalamika. Shangazi yao huyu alikuwa anapenda kula mara kwa mara hata ikampelekea mwili wake kuongezeka na kulazimika kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa kidaktari kutokana na hatari za kiafya zilizomuandama.

Aretha alitabasamu akiwaangalia ndugu hawa walivyofurahi kwa pamoja japokuwa waongeaji walikuwa ni Li na Coletha huku Edrian macho yake yalikuwa kwenye simu yake akiandika

"Retha are you comfortable?" meseji ikaingia kwenye simu ya Aretha ikiachia mlio ambao uliwashtua Coletha na Linus lakini hawakutilia shaka. Aretha hakujua kama ujumbe ule ulioingia ulitoka kwa Edrian akaangalia simu. Oh hapo hakuweza tena kuficha maana Coletha alimuona akitabasamu na kuangalia kiti alichokaa Ed

Akamjibu, "Am okay Rian. Tunaenda wapi?"

Edrian yeye alizima sehemu ya mlio wa simu yake hivyo ujumbe ulipoingia hakuna aliyejua ila tabasamu lake lisingefichika kwa Linus ambaye aliendelea kuendesha gari..

Coletha alipogundua akanyamaza na kuangalia simu yake kisha akamtumia meseji Li,

"Kaka Li nilikwambia, Bro anampenda Aretha hahahah wanatumiana meseji"

Li akashtuka baada ya kusikia mlio wa simu yake kuonesha kuna ujumbe uliingia, akaichukua huku akiendelea kutupia macho yake barabarani.

"Nina "Speed Tickets" mbili angalia usijepata nawe" Edrian akamwambia Li alipomuona akichungulia simu yake

Li hakuendelea kusoma akatikisa kichwa na kucheka taratibu mdogo wake na drama zake.

"Safari yao ikaishia Golden Bank, Edrian akageuka na kumwambia Linus "unaweza mpeleka baby sisy akachukue kitu cha kula jirani na_"

"Hapana Big brother tutawasubiri" Coletha akamkatisha

"Retha twende" Edrian akamwambia Aretha ambaye bado hakuelewa kwa nini wapo benki.

Coletha akamgusa begani Aretha na kutabasamu akachukua begi lililokuwa miguuni pake akimuacha ashuke.

Edrian akasimama nje akimsubiri Aretha ambaye baada ya kushuka macho yao yakagongana.

"Umependeza Retha" Edrian akamwambia

"Aah. .Asante Rian" akaitikia na kujiweka sawa

"Let's go" Edrian akanyoosha mkono kumuelekea Aretha ambaye akaangaza pembeni kuona watu wachache waliokuwepo kama waliwaangalia

"Rian tunaweza kwenda bila kushikana mikono eeh!" Aretha akamsihi Ed taratibu kwa sauti ya chini

"No Retha, twende" Ed akaendelea kuunyoosha mkono akimuangalia machoni. Aretha akaweka mkono wake kwa Ed na wakaondoka

Ndani ya gari Coletha alitamani kuruka kwa furaha, "nilikwambia kaka Li, yule kinyonga amepata dawa yake hahhahhhaha"

"Coletha, unapenda umbea wewe haaaa, ungekuwa unajua vita vinavyomsubiri ungemuombea kwenye sala zako. Humjui Lyn" Linus akaongea huku akiegama kwenye usukani wa gari!

"Kaka Li, hakuna awezaye ishinda nguvu ya upendo. Wanapendana hebu waangalie walivyoshikana mikono he he he he" Coletha akamwambia Li huku akiangalia nje.