Siku iliyofuata Edrian aliingia ofisini mapema sana, masaa mawili kabla ya muda wake wa kawaida. Alijikunja vyema akipitia ripoti mbalimbali huku ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya mkutano wa bodi ya SGC. Aliangalia ratiba yake kwa siku nzima ambayo ilikuwa imejaa, akajaribu kuona yapi anaweza kuyapunguza mapema kabla ya muda alioafikiana na Aretha.
Alikuwa na mpango ambao alikusudia umsaidie Aretha anapofanya maandalizi ya kushiriki onesho la Beruya. Na katika mpango wake alimshirikisha Coletha ambaye alikubali kujiunga nao ili kumpa uhuru Aretha.
Muda wa kuingia wafanyakazi wote ulipofika, Allan alikuwa wa kwanza kuingia pale ofisini, akaelekea ofisini kwa Ed,
"Habari ya asubuhi Bro" akamsalimia Edrian baada ya kuingia, akaitikiwa kwa tabasamu lililoonesha furaha usoni kwa Edrian
"Salama, vipi mnaendeleaje huko nyumbani?" Akarejesha salamu kwa Allan
"Tuko salama. Mama amekusalimia sana na anashukuru kwa kumpa kijana wake nafasi ya kutimiza ndoto zake hahahahha!" Allan akaongezea wakati akiketi. ..
"Hahahaha hamna shida, wewe ni familia" Ed akajibu huku akicheka. Allan kwa familia yake alihesabika kuwa ni sehemu ya familia kwa jinsi walivyokuwa wameshibana haswa na Linus.
"Bro, leo mapema sana naona, any special meeting?" Akauliza Allan
"Hahaha nope! Nina jambo binafsi mida ya saa sita nadhani kutokea hapo utasimamia yaliyobaki ikiwemo mkutano na Sangile Motors."
"Wale wa magari ya mikopo?" Akauliza Allan
Yes. Hukupata nakala ofisini kwako?" Ed akauliza kwa mshangao
"Niliipata, sikuwa na muda nayo sana, ripoti za bodi zilinimeza. Samahani Bro" Allan akaomba radhi.
"Usijali, sote tuna ratiba ngumu hii wiki, naelewa" akajibu Ed.
"Kweli, kuna kitu kingine bro kabla sijatoka kuikabili siku?"
"Yes Allan, umefikia wapi na watu wa Jamii kwenye andiko bora la mradi?" Akauliza Ed
"Tuna kikao kesho kupitia mawazo yatakayotolewa na maeneo yetu yote. Mrejesho nitakupatia mara moja tutakapomaliza" akajibu Allan
"One more thing... nataka SGC idhamini kwa asilimia 15 ya Onesho la "Color my Heart" litakalofanyika Jumapili hii. Meneja wa Beruya George atakuja na andiko lote leo mchana. Najua ni haraka kuweza kuwa na muda wa kujadili lakini ni maamuzi sahihi" Edrian akamaliza na kuegama kichwa chake kwenye kiti.
Moyoni alitamani ajifinye ili acheke kwa kuwa hakuamini kama mapenzi yalimfanya atumie nafasi yake kwa SGC kushawishi maamuzi. Akatabasamu akimuacha Allan akimshangaa
"Kuna cha ziada ninatakiwa kujua Bro" Allan akauliza huku akiinua jicho lake kumwangalia Ed ambaye ni kama ghafla mawazo yake yalimmeza
"Bro"
"Eeehm, unasema?" Akauliza Ed
"Hahaha nauliza kama kuna cha ziada natakiwa kukifahamu"
"Aaaaah Allan okay, nisipokwambia hata hivyo yule comrade mwenzio atakwambia. Najua una habari ambazo mimi sijazithibitisha. Mimi na Aretha Thomas ni wapenzi, na nakuomba usiniigizie hapa kwamba unashangaa ha ha ha " Edrian akamwambia
"Ooooh. ...hongera sana bro" Allan aliyekuwa akijaribu kuufanya uso kuonesha kuwa ile ni taarifa mpya kwake, akamjibu Ed.
"Okay, hivyo atashiriki kwenye Onesho la Beruya kutambulisha uchoraji wake kwa jamii ndi_" Ed akakatishwa kwa ghafla na Allan
"Nimekuelewa tafadhali wala usiendelee kujieleza.." Allan alimfahamu Edrian ugumu alioupata kuelezea mambo yake binafsi kwake
"Oooh asante Allan, umeelewa haraka hahaha"
"Hahaha najua"
Mlango ukagongwa na kuwafanya washtuke huku Allan akiinuka na kuaga
"Uwe na amani yatatekelezwa yote kwa haraka"
Loy akaingia akiwa na kikombe cha kahawa. Alipomuona Allan ambaye alikuwa akielekea pale aliposimama akashangaa
Allan akainama na na kumnong'oneza
:Na mimi kikombe cha kahawa kabla sijakuchomea ulivyochelewa"
Loy akakamaa, akimwangalia Allan ambaye alifungua mlango na kutoka.
"Za asubuhi bosi" Loy akasalimia na kuweka kikombe cha kahawa mezani pembeni ya kingine ambacho kilikaribia kuisha..
"Salama Loy, nao__" kabla Edrian hajaongea Lot akimkatisha
"Nisamehe bosi nimechelewa, nilianzia hospitali"
Edrian ambaye macho yake yalikuwa kwenye kompyuta akainua uso na kumtazama Loy "Unaumwa?"
"Hapana bosi, ni mgeni wangu"