Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 129 - MTEKAJI ASIYE NA MADHARA

Chapter 129 - MTEKAJI ASIYE NA MADHARA

Ilipofika muda wa mchana, Edrian akainuka alipokuwa amekaa kwenye kiti chake ofisini akajinyoosha. Tangu alipoingia asubuhi hakuwa ametoka nje ya ofisi yake, zaidi ya kuinuka mara mbili tu kunywa chai ambayo nayo ni Loy ndie aliileta kwa lazima. Akashukuru mpaka muda huo alikuwa tayari amemaliza asilimia 95 ya ripoti na kutoa mrejesho uliotakiwa. Akachukua simu yake na kugusa namba ya Aretha akapiga, simu ikaita kwa sekunde chache kisha ikapokelewa.

"Hello Princess" akaongea huku akiegemea kwenye ukuta pembeni ya dirisha, macho yake yaliangalia nje ambapo mwanga wa jua ulikuwa ukiakisi vioo katika majengo marefu ya A-Town

"Rian" sauti ya Aretha ilikuwa ya utulivu

"Hujaenda chuo Retha?" Akauliza kwa mshangao kwa kuwa kulikuwa na utulivu mkubwa kwa upande ule wa Aretha

"Hapana, nipo chuo. Nimeingia "Drawing Room" naona nimepata bahati hakuna mtu mwingine humu" akajibu Aretha

"Oooh sawa princess. Uko tayari?" Akauliza Edrian

"Niko tayari, nimeomba ruhusa kwa wakufunzi wenye vipindi viwili baadae. Unakuja?" Aretha nae akamuuliza

"Princess" akaita kwa upole Ed

"Aahm Rian" Aretha akaitika kwa sauti yenye mashaka

"Nina kazi moja ndogo namalizia hivyo na_"

"Usijali Rian twaweza fanya wakati mwingine" Aretha akamkatisha

"Hahaha Retha sijamaanisha hivyo. Ila kuna mtu atakuja kukuchukua hapo na tutaungana hapa ofisini kwangu" akamjibu Edrian

"Ooh basi sawa, ni nani huyo?" Kulikuwa na uchangamfu kwenye sauti ya Aretha uliomfanya Edrian kutabasamu kwa kuhisi huenda hamu yake ya kumuona Aretha iko katika uwiano sawa na binti huyu.

"Utamuona Retha. Atatumia gari nayotumia mara nyingi nawe. Atakutafuta akifika dakika chache kuanzia sasa"

"Sawa, Rian. Nitamsubiri pale pale Utawala" Aretha akamjulisha Ed hakutaka kumsumbua dereva aliyetumwa kumchukua

"Asante Retha. See you soon. Love you" akamaliza na kukata simu huku wakati huo akipiga tena simu nyingine

"Hello Li, tayari umeondoka?" Akamuuliza Linus ambaye alimuagiza akampitie kwanza Coletha ambaye alikuwa nyumbani, na pia aweze kuchukua gari ambayo alijua itakuwa rahisi kwa Aretha kuitambua, Volvo C60 SUV ambayo mara zote aliitumia alipokutana nae. Alifanya hivyo baada ya kupata chai ambapo alijua anaweza kuchelewa, akampigia Linus na kumuomba waongozane nae. Linus alimpompa mrejesho wa kuwa yuko tayari na Coletha na wanaelekea Capital University akashusha pumzi na kurudi kumalizia sehemu ndogo iliyobaki katika ripoti zote.

Akaelekeza macho yake kwenye kompyuta, sauti ya bofya bofya iliyotoka kwenye kompyuta yake ilisikika.

***********

"Kaka Li, Big Bro atamuoa Aretha eeeh, anavyomjali!!" Coletha aliongea na Linus njiani wakielekea Capital University kumchukua Aretha kama maelekezo ya Edrian yalivyokuwa.

"Coletha hatuna stori nyingine eeeh! Tangu umeingia kwenye gari unamuongelea kaka yako tu hapa na Aretha" Linus akalalamika

"Haahhaha kaka Li, sasa hata hii safari si tunaenda kwa Aretha aaah" Coletha aliongea kwa shauku kubwa sana ya kuonana na Aretha.

"Uuuhmmm" Linus akashusha pumzi macho yake akiyakaza barabarani ili kumuepuka mdogo wake na mazungumzo yake

Kimya cha dakika moja kikapita Coletha akiwa ameweka macho yake kwenye kioo cha simu. Lakini haikuchukua muda mrefu

"Kaka Li, Aretha sio kama yule kinyonga mimi namuona natamani hata aje tuishi wote pale na_"

"Aaaaargh" Linus akalalamika

"Nini kaka Li, kwani wewe humpendi Aretha?" Coletha akamuuliza akiwa ameketi kiti cha nyuma

"Aiseee Coletha, hukubali kushindwa. Daah haya. Namkubali sana Aretha si kwa sababu nyingine ila ni kwa sababu moja tu. Ni mtekaji asiyekuwa na madhara" Linus akaongea huku akimchungulia mdogo wake kwenye kioo akiona kuchanganyikiwa kwake.

"Mtekaji, unamaanisha nini kaka Li? Aahm!"

"Tumia akili yako kuelewa na sio kuongea Coletha" Linus akamjibu na kuendelea kuendesha huku wakikaribia maeneo ya chuo

"Sitaki kufikiri zaidi kaka Li, kama unamkubali inatosha, mambo ya mtekaji sijui asiye na madhara unayaelewa zaidi mwenyewe na comrade mwenzio" Coletha akamjibu na kuangalia simu yake kisha akapiga simu, kabla simu haijapokelewa Linus akamuuliza

Unampigia Aretha eh?