Chapter 123 - MJINGA

Ed alipiga hatua akimkokota Joselyn wakaelekea kwenye mlango mkubwa wa nyumba iliyokuwa mbele yake. Mandhari ya asubuhi ile ilifanya eneo lile kuwa kijani safi iliyozungukwa na bustani nzuri ya maua iliyoonesha kutunzwa vyema. Lakini kwa namna Ed alivyochafukwa asubuhi hii hakujali nini macho yake yaliona.

"Edrian niachie unaniumiza" Lyn akalalamika huku akijaribu kuunasua mkono wake

Edrian akasimama, akamwangalia kwa macho makali kisha akauachia mkono wake kwa nguvu na kumfanya Lyn ayumbe kurudi nyuma lakini akawaza kusimama vyema. Walikuwa wamefika karibu na mlango, na mara mlango ukafunguliwa, mama yake na Lyn akatoka.

Kwa hali aliyoiona akajua kuna jambo, "shikamoo mama" Edrian akamsalimia

Marhaba mwanangu, karibu ndani" akasogea kumpisha, lakini Ed hakuonesha dalili zozote za kupiga hatua akamshukuru kwa kuweka mikono pamoja..

"Mama, kabla sijafanya kitu chochote kibaya nikajuta naomba niseme mbele yako."

"Mwanangu unaonaje kama ukija tuongee wakati tumeketi ndani"mama huyu akamsihi Edrian kwa kuwa aliamini jambo lolote ambalo Lyn amelifanya litatakiwa kutatuliwa kwa kusikilizana

"Mama," si kila mtu ana muda wa kukaa na kuongea, halafu yeye ndie mwenye makosa na hap__!

"Joselyn" mama yake akamkatisha kisha akarudisha macho kwa Edrian ambaye alimwangalia Lyn asiamini maneno aliyoyasikia kutoka kwa binti huyu akimwambia mama yake.

"Mwanangu naomba tu unisamehe, nakuomba uingie ndani tuongee"

Edrian akaona si vyema na yeye kukosa adabu kwa kutomsikiliza mama huyu!

Sawa, mama"

Wakaingia ndani, Edrian alikuwa akiangalia mazingira ya mle ndani. Japokuwa alijua kuwa uchumi wa Martinez haukuwa na shida yoyote, muonekano wa sebule yake machoni pa Ed ulizidi kiwango cha utajiri ambacho kilionekana. Makochi yalikuwa ya ghali sana huku nakshi zake za maua zikivutia utadhani vilimilikiwa na mwana mfalme wa Saudi Arabia.

Baada ya kuketi, mama akamuuliza angetumia kinywaji gani, lakini Edrian akamkatalia,

"Nashukuru mama, nina kazi zinanisubiri ofisini. Nimekuja ili kujiweka wazi kwenu mfahamu uamuzi wangu" akameza mate kumpa nafasi mama yake Lyn kumsikiliza...

"Karibu useme tu mwanangu"

"Naomba Joselyn ufahamu kuwa mimi sio mpenzi, wala mchumba wako kuanzia sasa. Mama sihitaji Joselyn aingilie maisha yangu kabisa tena hasa kuonekana kwenye shughuli zangu." Ed alimwangalia Joselyn ambaye alitaka kusema kitu lakini mkono wa mama yake ukamkatisha ananyamaze..

"Mama, leo asubuhi naingia ofisini, binti yako amemtukana mfanyakazi wa__"

"Sio mfanyakazi wako ni mwanamke wako, unataka kuniong__"

"Joselyn naomba ukae na unyamaze" mama kamzuia Joselyn ambaye alisimama alikurupuka ghafla na kusimama

Akagoma kukaa, Edrian alipoona hivyo akaamua kuinuka na kumwambia mama yake Joselyn,

"Mama naomba niseme hivi kwa sasa mimi simtaki kabisa huyu binti yako karibu na nyumba yangu wala ofisini kwangu. Na kwa sababu hiyo akijaribu kulazimisha mama, matokeo yake sitahusika nayo." Akameza mate na kuendelea

"Mama, leo nimekuwa na kiasi lakini siku nikikosa naomba ujue nilikwisha kutoa taarifa. Nashukuru kunipokea naomba niondoke"

Mama ambaye alikuwa kwenye huzuni kubwa japokuwa alijikaza akasema

"Baba umeeleweka kabisa, nashukuru sana kwa ustaarabu wako" akasema huku akiinua kumtoa Ed

Joselyn alipoona Ed anaondoka, akapiga hatua kwa haraka na kumshika mkono Ed

"Babe, huwezi kuniacha acha tu, kumbuka tulikuwa sawa kabla ya A_"

"Niache Joselyn" Edrian akamwambia akionesha kujizuia kutumia nguvu

Mama yake Joselyn akamsogelea mwanae na kumshika kwa nyuma

"Mwanangu hebu msikie mwenzio na umwa_"

"Hapana siwezi niache" Joselyn akajibu kwa jazba na kugeuka kwa nguvu kitendo kilichopelekea mama yake kukosa uwiano na kuanguka

Edrian aliyesimama hatua chache kutoka alipoangukia mama huyu alimwangalia Lyn ambaye alimgeukia pasipo kujali mama yake aliyeanguka chini...

PAAAAH!

Sauti ya kibao kilichoshuka usoni kwa Lyn ilisikika na kusababisha mama aliyekuwa akiinuka kushtuka kwa mshangao

"Mjinga sana Lyn, unamfanyia hivi mama yako!" Sauti ya Ed ilijaa hasira, akaelekea alipokuwa mama yake Lyn na kumuinua taratibu