Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 124 - UUNGWANA WA ED

Chapter 124 - UUNGWANA WA ED

Edrian alipomkalisha mama yake Lyn kwenye kochi akageuka na kumwangalia Lyn aliyekuwa akitiririkwa na machozi asiamini kama Ed ndie aliyempa kibao kile

"Am not sorry for that Joselyn and I don't want to see you anymore" akapiga hatua kuelekea mlangoni akimuacha mama akimsogelea binti yake. Alishangaa ni kwa namna gani mama huyu alivumiliana na mwanae hata asijali namna alivyomdharirisha.

Akatoka kuelekea alipoegesha gari yake nje. Akaingia na kuangalia simu yake ambapo alikutana na simu zilizopigwa kutoka kwa Allan, Linus mdogo wake, Captain na nyingine chache za kikazi

Akampigia Allan huku akiwasha gari na akaondoka mahali pale.

"Brother, are okay" Allan akauliza kwa wasi wasi

"Am okay. Niko njiani narudi, wait for me in my office"

Baada ya kukata simu simu ya Captain iliingia

"Yes" kaitikia Ed

Upande wa pili Captain akamwambia "Good news Bro kuna vitu tumepata kuhusu binti wa Martinez huko S.A, lakini cha msingi sana kuna taarifa ya uhujumu unaofanywa na baba yake ambao ukiwekwa wazi atapotea kabisa kwenye game"

"Great Captain, nitakuona baadae"

Akakata simu na kuendelea na umakini wake barabarani mpaka alipofika ofisini. Mara alipofika akamuuliza Loy iwapo Renatha alimkabidhi faili

"Hapana bosi"

"Mmmmmm" akaguna na kabla Loy hajatoa wazo

"Mwambie nalihitaji sasa. Na Allan?" Akauliza

"Yuko ofisini kwako bosi"

Akapita hatua na kuingia ofisini kwake. Wakasalimiana na Allan ambaye alijua leo bosi hakuwa na hali njema.

"Allan naomba uwajulishe watu wa ulinzi kuwa Josely Martinez Kussah haruhusiwi kuingia kwenye mazingira ya jengo hili. Awe anakuja kwangu au ofisi nyingine humu ndani. Na pili hakuna ruhusa kwa mtu asiye VIP kutumia lifti au kuingia kupitia mlango huo."

"Sawa bosi"

"Kuhusu miradi ya maendeleo ya jamii naomba lile shindano la andiko bora la mradi lifanyike. Itisha mkutano na watu wa jamii maeneo yetu yote tuone tutafanya nini kurudisha kwa jamii kupitia shindano hili"

Allan akafurahi kusikia hivi, " nitafanya hivyo ASAP. Tuna kikao cha bodi wiki ijayo kama ratiba inavyoonesha. Nafikiri tuwe na kikao maalumu kukamilisha ripoti zote"

"Ni sawa nakubaliana nawe kabisa" simu ikaita akabonyeza

"Bosi Renatha yuko hapa." Sauti ya Loy ikasikika

"Mruhusu aingie"

Allan akataka kutoka lakini Ed akampa ishara abaki. Mlango ukafunguliwa na Renatha akaingia, alipokutana macho na Allan akaonesha mshangao kwa kuwa alitegemea kumkuta Ed pekee. Akawasogelea na kunyoosha faili kumkabidhi Ed

"Nilidhani ungemkabidhi Loy, kwa nini ulibaki nalo?" sauti ya Ed ilibeba mamlaka ya kiti alichokalia hata kumfanya Renatha kupatwa na hofu lakini akajiweka sawa na kuachia tabasamu

"Kwa sababu hukunipa maelekezo hayo Mr Simunge" akamwangalia usoni na kisha akayarudisha kwa Allan ambaye alimwangalia kwa kushangazwa na ujasiri wake

Edrian akalipokea na kumkabidhi Allan. "Check mrejesho wa Renatha kuhusu tukio la G-Town." Akiinua macho na kumwangalia Renatha

"Naomba radhi kwa kile kilichotokea asubuhi ya leo, hukutakiwa kurushiwa maneno yale. Nitaelewa ikiwa utalalamika kwa mamlaka husika. Lakini barua ya kuomba radhi nikaitika kwenye barua pepe yako. Haitajirudia tena na pole kwa usumbufu uliojitokeza" Edrian aliongea kwa kumaanisha akimuacha Allan akishangaa nini kilitokea

"Hapana shida Mr Simunge. Apology accepted. Hatuhitaji kufikishana kwenye mamlaka." Renatha akajibu na kuachia tabasamu

"Basi mrejesho wako nitauhitaji kimaandishi kama ambavyo yangu itakuja kimaandishi"

"Nitafanya hivyo" Renatha akakubali

"Nashukuru waweza kuendelea na kazi zako" Edrian akamruhusu

Baada ya Renatha kutoka, alijua Allan alistahili kupewa maelezo ya kile kilichotokea asubuhi lakini hakujua aanzie wapi. Akajikaza na kumuelezea nini kilitokea lakini hakumsimulia kilichoendelea kwa kina Joselyn. Allan alielewa kabisa kuwa bosi wake ni msiri linapokuja suala la maisha yake binafsi.

Walipomaliza kuongea, akampa maelekezo Loy kuandika barua ya kuomba radhi akiamini ni kitendo cha kiungwana na ni utaratibu wa kimaadili kwa SGC. Kama Lyn angekuwa ni mfanyakazi wa SGC basi hatua za kinidhamu zingechukuliwa dhidi yake.