Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 117 - JICHO LA TATU

Chapter 117 - JICHO LA TATU

"Unakumbuka siku ile nakurudisha nyumbani tukapata ajali ndogo?"

Aretha akashtuka na kuinua uso kumwangalia Edrian ili aendelee

"Ile gari ilifanya makusudi kuingia kwa mbele kwa ghafla. Na hiyo gari imewahi kufika karibu na ofisini kwangu lakini pia hapa nyumbani."

"Eeeeh" akashtuka Aretha.

"Retha nakuomba uniamini na kile najaribu kufanya"

Aretha akabaki kimya kwa sekunde chache akamwambia Ed

"Rian, huwezi kuwa unakatisha ratiba zako kila mara kwa ajili yangu. Kwanza unanifanya nijisikie vibaya na nisiwe na maamuzi yangu binafsi" akaongea taratibu huku akishika mkono wa Ed

Edrian akamwangalia kisha akatabasamu, "nimekuelewa Retha, najua nakulazimisha uishi ulimwengu wangu ambao nimeuzoea una unafiki na kuzungukana kwa wingi. Nitajitahidi kukupa uhuru wako"

Macho ya Aretha yakawaka kwa furaha, akamkumbatia Ed. "Asante Rian nimekuelewa"

Edrian akatabasamu akishangaa kumbatio alilopewa kwa ghafla lilihusiana na Aretha kupenda uhuru wake au ndio walikubaliana kuhusu kuweka mtu wa kumfuatilia.

"It's okay Retha"

Kwa wakati huo Edrian hakutaka tena kuendelea na mazungumzo yale baada ya kumfahamu Aretha kuwa ni mtu anayeheshimu maisha yake binafsi.

"Retha" akaita taratibu na kumfanya Aretha kutoka kifuani kwake kwa aibu huku akitazama chini

"Abee"

"Nakuomba usimkasirikie Charlz, endelea kuwa karibu naye. Yeye ni jicho langu la tatu linapokuja suala la usalama wako" Ed akamsihi kwa kutambua kinachoweza kutokea kwa Aretha kufahamu Charlz ni rafiki wa Derrick.

"Sawa Rian."

Wakashuka kuelekea kwenye geti.

"Rian sio lazima uingie kama una haraka" Aretha akamwambia Ed wakati wakisubiri geti kufunguliwa.

"Sio heshima pia kuja hadi hapa na kuishia nje tu Retha" akampa na tabasamu la kumuonesha hatobadili maamuzi yake ya kuingia ndani.

Frans akafungua geti dogo, alipomuona Ed akiwa na dada yake akaachia tabasamu na kumsalimia. Baada ya kusalimiana akataka kufungua geti kubwa ili Edrian aingize gari lakini Aretha akamuwahi

"Usifungue Frans hatakaa sana"

Ed akatabasamu zaidi akimuangalia Aretha usoni naye alikwepesha macho na kisha akapiga hatua kuelekea mlangoni akimuacha Ed amfuate kwa nyuma.

Frans aliyebaki mlangoni akawa akimshangaa dada yake kwa hatua aliyopiga akimuacha Ed.

"Anamtimua mgeni aaaaaisee" akawaza.

Aretha akageuka mara alipofika kwenye ngazi za kuingia kwenye kibaraza cha nyumba ile..

"Nisubiri hapa ngoja nimuite mama umsalimie" akamwambia Ed ambaye naye alisimama huku akitabasamu

"Hutaki niingie ndani Retha?" Akamuuliza kwa kumtania huku akiinua jicho

"Aaaah sio hivyo Rian n..ni. .aa namjua mama ukiingia hautaondoka sasa hivi. Sio salama kutembea usiku" Aretha akajitetea lakini alimaanisha ukweli uliokuwa moyoni mwake. Hakutaka Edrian achelewe kwa namna mazungumzo yao yalivyokuwa. Naye pia alihofia usalama wa Edrian.

Akaingia ndani akimuacha Ed ameegama kwenye ukuta wa kibaraza kile. .

Mama akatoka nyuma akifuatiwa na Aretha,

"Mwanangu karibu, huyu binti yangu kakuacha usimame tu hapo nje"

Akamwangalia Aretha kisha akarudi kwa mama "Na mimi mama nimeshangaa leo nimewekewa zuio la kukaribia ndani"

Aretha akashtuka na kumwangalia Ed ambaye alimpa tabasamu na kuanza kuvua viatu huku mama akisimama pembeni kumkaribisha ndani. Alipoona mama yake anaelekea kumpisha Ed kuingia ndani akaamua kutafuta namna lakini akachelewa maana Ed aliingia ndani akifuatana na mama na Frans.

"Ooooh tafadhali hakuna anayenisikiliza...Aaargh" Aretha akapiga hatua na kuingia ndani akiweka tabasamu bandia usoni...

"Mwanangu heri umekuja upate chakula kabisa" mama akamkaribisha kwenye meza ya chakula

"Asante sana mama, nashukuru kuniwazia leo mchana sikula chochote" Ed akamjibu huku akielekea kuketi mezani. Ukweli ni kuwa hakuwa amekula mchana kwa sababu ya Lyn na vituko vyake.

"Unaona Retha, mwenzio hajala na wewe unamkimbiza tu" mama akamsema Aretha ambaye alimwangalia Edrian akishangaa kama kweli alikuwa hajala au ni sehemu ya kumkomesha kwa mama yake!

Edrian akampa ishara amsogelee baada ya kuona mama akielekea jikoni. Aretha akamsogelea na kuinama alipokuwa ameketi

"Ni kweli sijala princess."