Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 115 - FUKUTO LA WIVU

Chapter 115 - FUKUTO LA WIVU

"Retha nisubiri nakuja kukuchukua" Ed akamkatisha Aretha kabla ya kumaliza.

"Rian no...una ratiba za muhimu ji__" Aretha akajaribu kumkataza lakini jibu lililofuata likamfanya ashushe pumzi na kuamua kutulia

"Wewe ni wa muhimu na uko kwenye ratiba yangu. Tafadhali nisubiri pale Utawala nitafika ndani ya dakika 20" Ed wakati anamaliza maneno haya alikuwa amesimama akimpa ishara Captain kufanyia kazi yale waliyoongea...

"Okay Rian." Aretha akajibu kwa unyonge kisha akakata simu.

Kwa upande wa Ed alijua anachofanya ni sahihi kwa sababu hakutaka usalama wa Aretha ulete shida kwa wakati ambao alimhitaji sana.

"Tuonane kesho, na taarifa sahihi. Nitaanza na hii niliyonayo." Ed akamaliza na kuondoka kuelekea kwenye gari lake.

"Siwezi kukuhatarisha, lakini nataka kukuona pia. Wait a little more princess, an coming" aliwaza moyoni huku akiendelea kukata mitaa kuelekea Chuo Kikuu cha Capital.

Aretha alikaa kwenye vibwete vilivyokuwa karibu na jengo la Utawala, hisia zake zilinyong'onyea mara aliposikia Ed anamfuata mpaka shule. Alipenda kumuona Edrian lakini hakutaka kuwa sehemu ya mabadiliko ya ghafla ya ratiba zake. Hakutaka kuwa mzigo kwa mtu ambaye alitamani awe msaidizi tu wa furaha yake.

"Aretha, muda huu Utawala unasubiri nini rafiki yangu?" akashtuliwa na sauti ya kiume iliyotokea nyuma yake na kumfanya ashtuke na kugeuka kwa haraka..

"Aaahm...oooh Charlz ni wewe aa. .umenishtua" akaweka mkono kwenye kifua akainama akishusha pumzi

"Nimekushtua mrembo?, maana si kawaida yako hata mara moja kuwa maeneo haya" akaongea Charlz huku akiangaza huku na kule kuona kama kulikuwa na mtu aliyekuwa alimsubiri

"Aaahm n..nna. .namsubiri mtu sasa hivi nitaondoka" Aretha akasita lakini akamwambia

"Ooohw Aretha jioni hii unamsubiri nani?" Charlz akaamua kumchokoza Aretha, japokuwa alishahisi atakuwa Edrian kwa namna walivyoongea kwenye simu, bado alitaka kuona atamwambia au la!

"N.nani...kwa maana gani?" Aretha akamshangaa Charlz na hili swali

"Yaani ni nani anayekufanya umsubiri hapa Aretha au nirudie kuitengeneza sentensi" Charlz akakaa kwenye kibwete huku akamtazama

"Mhhhm ..aah Charlz!! mtu anakuja yuko njiani, tafadhali usiulize zaidi" Aretha akageuka na kuangalia kwingine

"Oooh basi vyema, nitakusaidia kumsubiri tukiwa wote" Charlz akakunja na miguu kuonesha hakuwa na mpango wa kuondoka.

"Aahm ulikuwa una mambo yako Charlz endelea tu" Aretha akaanza kumsihi tena hakuhitaji huyu rafiki ajue ukaribu wake na Edrian Simunge.

"Wewe ndio mambo yangu kwa sasa, acha tusubiri pamoja" Charlz akakunja mikono kifuani kuonesha hakuwa na mpango wa kuondoka. Aretha akamwangalia kisha akatoa simu yake na kutaka kuandika meseji kwa Edrian. Ghafla Charlz akampokonya simu na kuinuka huku akimuonesha kuwa atakimbia nayo..

Aretha akainuka kujaribu kumkimbiza ampe simu yake. Wakati hayo yakiendelea Edrian aliegesha gari katika maegesho ya chuo huku akiangalia Aretha na Charlz walivyokuwa wakikwepana. Akachukua simu yake na kuipiga namba ya Aretha.

Charlz alipoona simu inaita akaangalia kwenye skrini na kuona jina lililoandikwa pale akatabasamu. Muda huo Aretha aliutumia vyema kumpokonya simu na macho yake yakawaka kwa kuona namba ya Ed ndio ilikuwa kwenye kioo cha simu. Kabla ya kupokea akaongeza huku na kule mpaka macho yake yalivyoona gari ya Ed na mwanga wa simu uliokuwa ukiwaka kuonesha ni yeye akipiga.

Aretha hakupokea bali aligeuka na kumuaga Charlz aliyesimama akiingalia gari ambayo alijua ni ya Edrian.

"Haya nakuacha cha ukorofi, kwa heri" akapiga hatua kuelekea gari ya Ed iliposimama. Ed akaweka simu pembeni alipoona Aretha anaelekea alipo.

Aretha akafungua mlango na kuingia kwenye gari, "Sorry Rian, nimeacha kupokea sababu nilikuona tayari." Akamwambia huku akifunga mkanda

"Mmmmmm" Ed akaguna na kumfanya Aretha kushtuka na kujaribu kumwangalia usoni japo hakuweza kumuona vyema sababu ya mwanga mdogo ambao ulimulika upande walipokuwa.

Edrian akawasha gari na wakaanza kuondoka eneo la chuo, mwendo ulikuwa kama wa mtu asiye na haraka kabisa.

"Rian, usinge__"

"Nisingekuja Retha eeeh?" Edrian akageuka