Edrian, huyo mwanamke alikuja kutaka nini?" Lyn akauliza huku akimpita Ed na kwenda kuketi.
Edrian akakunja ngumi mikono yake akatamani apate kitu cha kupiga ili kupunguza hasira aliyoisikia ikimpanda taratibu.
Akaelekea kufunga mlango na kisha akasimama pale pale mlangoni akimwangalia Lyn ambaye alimtega mgongo.
"Joselyn last time nilikwambia uwe na adabu na ofisi yangu. Wewe sio mfanyakazi hapa, na hata kama ungekuwa mfanyakazi bado hiyo sio heshima kuvamia ofisi yangu kama unaingia kwako"
Lyn akageuka na kumwangalia Ed kwa sekunde halafu akainuka na kuelekea aliposimama, "okay babe am sorry, yule mwanamke aliyetoka humu ni nani?" Akasimama akimuangalia usoni Ed
"Kwa hiyo nikupe taarifa kama nani Lyn, bodi ya wakurugenzi, au menejimenti aaah?" Mtetemo wa hasira kifuani kwa Ed aliposema maneno haya ukamfanya Lyn ashtuke
"Ed am sorry, unanikasirikia kwa nini, sababu ya huyo mwanamke au nimefanya nini zaidi?" Akauliza hali mikono yake akiiweka kiunoni
"Hujui unachofanya au unajifanya hujui!" Akauliza Ed kwa ukali
"Nimefanya nini babe?" Lyn akauliza kwa mshangao...
"Kwa nini uko hapa Lyn?" Ed akauliza huku akipiga hatua kuelekea kwenye kiti, lakini kabla ya kufika Lyn akamshika mkono na kumkumbatia kwa nyuma. Kitendo hiki kilifanya mwili wa Ed kukakamaa kama aliyepigwa na radi
"Babe, usinifanyie hivi basi. Nimekuja tuzungumze kidogo" Lyn akamjibu kwa sauti ya kudeka
"Niachie Lyn" Ed akamtahadharisha
"Sikuachi babe" Lyn akajibu na tena akakaza mikono yake iliyopita tumboni kwa Ed na kichwa akakiegemeza mgongoni.
Edrian alihisi kama sumu ya nyoka ikimpanda hadi kwenye moyo akamshika mikono na kuitoa tumboni kisha akageuka. Macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira akionesha wazi alikuwa akijizuia kuendeshwa na hisia hizo
"Lyn sema kilichokuleta nikiwa kazini"
Joselyn akatabasamu na kuelekea kilipo kiti, akaketi na kisha akatoa kwenye mkoba wake boksi ndogo sana. Akaifungua na kuiweka mezani.
Macho ya Ed yaliangalia pete ikiwa imewekwa vyema kwenye kiboksi kile huku nakshi yake iking'arishwa na almasi.
"Nataka univishe pete wikiendi hii" Lyn aliongea huku akitabasamu kwa furaha
"Huyu mwanamke anataka kunitawala eeh" Edrian aliwaza huku akimuangalia kwa mashaka
"Kwa nini nikuvishe pete kwa amri yako na sio kwa matakwa yangu eeeh" Ed akauliza akimkazia macho
"Hebu keti kwanza babe, let's talk" Lyn akamwambia akimuelekeza kuketi kwenye kiti chake. Edrian akaelekea kuketi. Akainua macho yake kumpa ishara Joselyn aendelee
"Ed babe.. Mimi ninajua kuwa usipofanya hivi utaendelea kumfuatilia yule mwanamke au huyu aliyetoka hapa" akaongea huku sura yake ikionesha kukerwa
"Lyn unajua sipendi kabisa kuyachukulia mambo ya ofisini kwako kama yanahusika nawe. Na kuhusu pete, sitafanya kama kama utakavyo. Siendeshwi nawe." Akamwangalia Lyn kwa jicho la ukali
"Edrian Simunge, mimi na wewe ni milele pamoja." Akainuka Lyn
"Na hii pete itabaki hapa, tafakari niliyosema" akaanza kuondoka, alipofika mlangoni akageuka na kumpeperushia busu Ed huku akitabasamu
"Wewe ni wangu milele Ed" akasema kisha akafungua mlango na kutoka. Edrian akachukua ila pete akaiangalia kwa hasira lakini wazo moja likamjia akaiweka kwenye droo huku akitabasamu.
"Joselyn ni suala la muda mfupi tu kelele zako zitaisha."
Akainua simu yake nakuandika ujumbe mfupi kumuuliza Aretha muda ule alikuwa wapi. Dakika kadhaa zikapita, ndipo mlio wa meseji ukasikika kwenye simu yake,
"Sorry Rian..nilikuwa darasani na ukishika brashi mwalim hakuruhusu kuacha mpaka umalize. Nimeaga kuja short call, how are you?"
Tabasamu safi lilionekana usoni kwa Ed, akaanza kuijibu
"I miss you Retha. Unatoka saa ngapi?"
Akajibu Aretha, "Leo ninamaliza saa mbili usiku. Rian itakuwa usiku labda kesho"
Edrian akacheka taratibu kisha akaandika "Nitakurudisha nyumbani. Rudi darasani mwalim atashtuka. I love you Retha"
Akaweka simu na kuendelea na kazi.
******************
Joselyn alipotoka ofisini kwa Ed akaelekea kwenye ofisi ya Loy.
"Hey Loy, yule mwanamke niliyekutana naye hapa ofisini kwake wapi?"
Loy akainua uso na kumwangalia Lyn kwa mshangao wa wazi