******************
Joselyn alipotoka ofisini kwa Ed akaelekea kwenye ofisi ya Loy.
"Hey Loy, yule mwanamke niliyekutana naye hapa ofisini kwake wapi?"
Loy akainua uso na kumwangalia Lyn kwa mshangao wa wazi kisha akauliza
"Unamaanisha Renatha au?"
"Aaah kumbe anaitwa Renatha, niambie ofisi yake" Lyn akainama akimuangalia Loy kwa kutaraji kusikia ofisini kwa Renatha..
"Anatumia ofisi ya Meneja Beno kwa sasa"
Akamkonyeza na kisha akatoka mle ofisini akimuacha na maswali, Loy ambaye awali alishuhudia namna ambavyo Renatha alimjibu Lyn baada ya kumuuliza kwa dharau kwa nini alivaa sketi aina ile pale ofisini.
"Sijui nini kitaendelea huko ndani" akawaza Loy.
Haikumchukua muda Lyn kuingia ofisini kwa Meneja Beno pasipo kugonga mlango.
Meneja Beno ambaye alikuwa kwenye meza yake akielekezana na Renatha aliinua uso na kumwangalia Lyn
"Karibu" meneja Beno alimkaribisha huku akimuonesha kiti aketi. Na wakati huo Renatha alipogeuka na kumuona Joselyn akarudi kwenye meza yake iliyokuwa hatua chache kutoka alipokuwa.
"Asante, nadhani nahitaji kuonana na huyu dada asiyejua maadili ya kazi" Lyn akaongea huku akielekea kuketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza ya Renatha..
"Samahani Miss Kussah nadhani unatumia lugha isiyo sahihi, halafu wageni wanaokuja hapa wako chini yangu. Tafadhali nijue nakusaidia nini" Meneja Beno akamuelekeza Lyn ambaye aliketi kwenye kiti mbele ya Renatha akimuangalia kwa dharau. Meneja Beno alimfahamu Joselyn kuwa na binti wa Martinez lakini hakuwa anajua haswa mahusiano ya Lyn na Edrian bosi wake.
Renatha akaachia tabasamu, "Usijali Beno acha nimsikilize mteja wetu hata kama hana adabu"
Meneja Beno akabaki njia panda akimwangalia Lyn na kisha Renatha, akahisi huenda wanafahamiana. Akainuka na kutoka mle ofisini awaache wazungumze
"Unataka niwe na adabu kwa mtu kama wewe tsk. ..tsk. ..siwezi" Lyn akaongea
"Okay, kwanza sijui tatizo lako ni nini, na wewe ni nani hapa. Maadili yangu hayapangwi na wewe, kama bosi wangu hajapata shida wewe hata useme nini hainishtui" akaongea Renatha
"Eeeeh wewe hunijui, utanijua sasa, kama unajisogeza kwa bosi wako ili akuone unapoteza muda wako" kwa kujiamini Lyn akaongea
"Hahahahah unasumbuliwa na nini dada, unadhani kila anayeingia kwa bosi ana mawazo kama yako. Umepotea" Renatha akaongea huku akicheka
"Sikia Renatha, usijifanye mjuaji, hujui unayemzungumza nae" akasimama Lyn
"Vaa vizuri kama unataka kubaki kwenye kampuni...na Edrian Simunge abaki kuwa bosi wako na si zaidi ya hivyo ufikiriavyo"
Akageuka na kuanza kuondoka
"Wewe sio bosi wangu hata kunipa maelekezo, na ikiwa nimeazimia kitu huwa sikikosi. Usinijaribu pia" Renatha akamjibu na kuinuka kuelekea mlangoni
Lyn aliyekuwa mlangoni akageuka kutaka kumjibu Renatha, lakini kabla ya jibu kumtoka simu iliyokuwa mezani kwa Renatha ikaita.
Renatha akarudi na kupokea...
"Sawa bosi" akaitikia mara baada ya kupokea simu na kusikia maelekezo ya upande wa pili. Akageuka kumwangalia Lyn huku akiweka tabasamu
"Tuko kazini, mwenzetu unazurura tu"
Lyn aliyekuwa amesimama akamwangalia huku dalili za hasira zikiwa wazi usoni kwake! Akaondoka na kufunga mlango kwa nguvu akimuacha Renatha akicheka taratibu.
"Siamini kama Ed anaweza kuwa na mtu wa aina hii"
Akatoka na kuelekea ofisini kwa Allan.
**********************
Edrian ambaye hakujua nini kilikuwa kinaendelea kwenye jengo lake alishtuliwa na simu ya Joselyn ambayo hakutaka kabisa kuipokea lakini ujumbe uliotumwa ulimfanya apokee mara ilipoita tena...
"Lyn unataka nifanye nini u__" kabla ya kuishusha vyema hasira yake Lyn akamkatisha Edrian
"Ed simtaki huyo Renatha"
"Mmmmmm" Ed akaguna
"Huyo dada anakutaka halafu na__" Edrian hakuweza tena kuvumilia akamuuliza kwa hasira
Wewe kama nani unipangie wafanyakazi "wangu, nadhani umeshindwa kujua mipaka yako" kisha akakata simu. Mara hiyo akampigia Captain,
"Niandalie utafiti wa kutosha kuhusu Lyn huko S.A na ikibidi dukua mawasiliano yake yote. Nakupa masaa 42 Captain nataka kumaliza hii kesi"
Edrian alipomaliza kuongea, akampigia tena Derrick ambaye alipokea
"Uko free?"