Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 111 - NJIA PANDA

Chapter 111 - NJIA PANDA

"Karibu uketi"

Ed akamkaribisha kisha akarudisha tena macho yake kwenye kompyuta

Renatha akaketi huku macho yake yakimwangalia Ed aliyekuwa makini kusoma yaliyokuwa mbele kwenye kompyuta yake.

Ukimya ule uliendelea kwa sekunde kadhaa mpaka Ed aliposhtuka

"Utaendelea kuniangalia hadi saa ngapi ili nikusikilize Renatha"

Renatha alishtuka baada ya kugundua Ed amejua alivyokuwa akimwangalia..

"Aah hm hapana Mr Simunge..n..nilikuwa nasubiri unisikilize" akajitetea

"Nakusikiliza" Ed akainua kichwa na kumwangalia

Renatha akaachia tabasamu baada ya kuona Ed kampa nafasi akiacha alichokuwa akifanya..

"Nataka kuongelea ripoti ya jumla ya G-Town"

"Mmhhm..ungeweza kuongea na MO kuliko kuja kwangu" Ed akamjibu kichwa chake akiegemea kwenye kiti

"Allan yuko nje kiofisi na ni kitu nimekigundua ambacho nafikiri wewe una mamlaka ya haraka kukifanyia kazi" Renatha akajitetea ili kuonekana alikuwa kikazi zaidi..

"Mmmmm" Ed akaguna huku akikuna kidevu chake taratibu

"Kwanza nimeona kuwa kuna uwezekano wa kuwa na 'mamluki' kule 'site' ambao walitaka kuharibu taswira ya mgodi" Renatha akaeleza kwa shauku kuu ili Ed aone mchango wake..

"Jingine uliloona maana hili timu yangu ilishaliona" kwa utulivu kabisa Ed akajibu na kumfanya Renatha kukunja mikono yake lakini akajikaza na kuendelea!

"Lakini nina mashaka na yule OP, kwa nini alipohojiwa alionesha kukubali kwa haraka makosa kama hakuwa anajua chochote? Hakuonesha mshangao wowote ni kama hali hiyo ilikuwepo na yeye alikuwa anajua!"

Ed akamwangalia Renatha akagundua alichosema kilikuwa na mantiki.. "oooh okay, nadhani hilo linafaa kuangaliwa upya. Nina swali?" Ed akamkazia macho Renatha

"Niuliza bosi" Renatha akasema huku akitabasamu

"Uko hapa kuisaidia serikali kuona kama tunaendesha shughuli zetu kwa kuzingatia sheria na vigezo ee? Ed akauliza huku akikuna kidevu chake taratibu

Renatha akaitika kwa kichwa...

"Sasa hii taarifa ni kama unatanguliza maslahi ya SGC kuliko ya serikali inayokulipa?" Ed akamuuliza akimkazia macho usonj

Renatha akaachia tabasamu na kisha akamjibu

"Ni ubinadamu pia kujali mamia ya watu walioajiriwa na SGC kuliko kufikiri kutoa ripoti ya haraka kuiangamiza. Kuna watu ukiitoa SGC maisha yao yanaweza kabisa kuteketea"

Edrian akamtazama Renatha usoni kisha akaachia tabasamu jepesi kisha akamshukuru, "Asante Renatha tutalifanyia kazi mapema. Nashukuru kuliona."

Moyo wa Renatha ulipatwa na furaha, "Mr Simunge kwa hilo uamini ninawaza maslahi ya SGC na si tu kile kilichonifanya kuwa hapa"

Edrian akarudisha tabasamu lile na kumuashiria amekubaliana nae.

"Tunaweza kupata chakula cha mchana pamoja leo kama pongezi kwa nilichofanya?" Renatha akamuuliza Ed

Edrian ambaye moyoni alimsoma vyema binti huyu na kuona alitamani kuwa karibu naye kwa namna alivyotaka kumuonesha alichofanya. Alijua kabisa Renatha kamletea taarifa hii yeye kwa makusudi kama karata ya kumpiku akubaliane na matakwa yake

"Sawa Renatha..lakini haitakuwa leo kwani nin__" mlio wa simu ulimkatisha Ed. Ilikuwa ni simu ya mawasiliano ya ndani,

"Sorry" akamwambia Renatha na kisha akachukua simu na kuweka sikioni

"Nani Loy" akauliza baada ya kusikia sauti ya Loy ikimpa taarifa ya uwepo wa mgeni

Sura ya Ed ghafla ikabadilika aliposikia jina la mgeni "mwambie asubiri, namalizana na Renatha" akakata na simu.

Renatha alipoona sura ile ya Ed ikiwa imejikunja kuonesha mgeni aliyekuwa nyuma ya mlango ule alikuwa hakuwa kwenye matarajio yake leo..

"Sorry...Nina mgeni, kama kuna la ziada niambie kabla haujaondoka"

"Hapana sina, ila umesema leo hatutakuwa na 'lunch' au tufanye chakula cha jioni"

"Hapana Renatha, nitakujulisha kati ya kesho au keshokutwa. Nashukuru" kwa jibu hili Renatha akainuka na kushukuru kisha akatoka

Edrian akashusha pumzi, "what have I gettin myself into"

Mlango haujafunguliwa kama alivyotaraji.. akasubiri dakika mbili zikapita akainuka kuelekea mlangoni, lakini kabla ya kufika, mlango ukafunguliwa kwa nguvu. Joselyn akaingia huku akionesha kabisa kuwa na hasira.

"Edrian, huyo mwanamke alikuja kutafuta nini?" Lyn akauliza huku akimpita Ed na kwenda kuketi.