Chapter 110 - RENATHA

"Renatha, siku ya kwanza umerudi bila taarifa njema kwangu zaidi ya kuwapa serikali faida" aliongea TM akiwa ametulia kwenye kiti chake huku akizungusha kitufe mkononi mwake

"Baba, Ed___"

"Sssssshh mara ngapi nakuambia usiniite 'baba' tunapozungumzia kazi Renee?" Sauti yenye mitetemo ya hasira ilimfanya Renatha kukakamaa ghafla..

"Samahani ba..aaah boss" Renatha akaomba msamaha

"Na kama mimi ni boss wako, nani amekupa ruhusa ya kuongea ukiwa umeketi kwenye kochi?" TM aliendelea kuongea pasipo kutazama usoni kwa Renatha.

Renatha akasimama mikono yake ikakutana mbele kama mmoja ya wafanyakazi wa baba yake.

"Samahani ba...boss, haitajirudia" akainama na kisha akaendelea, Simunge hakuwepo ofisini karibia siku nzima. Kesho nitajitahidi kuwa karibu naye..am sorry boss" Renatha akayasema maneno haya pasipo kumtazama baba yake lakini ungeweza kuona mikono yake ilivyokunjwa kwa uchungu na hasira kwa namna ambavyo TM alimchukulia.

TM akageuka na kumwangalia usoni kisha akamwambia, "njoo ukae hapa Renee"..

Renatha hakutikisika wala kuonesha kuchukua hatua yoyote "Asante boss hapa panatosha" akajibu na kuendelea kuinama akisubiri apewe ruhusa ya kuondoka..

"Renatha" sauti ya ukali ilimtoka TM na kumfanya Renatha kukakamaa zaidi lakini bado hakupiga hatua kumsogelea bali akaendelea kusimama alipokuwa

Baada ya kuona msimamo wa Renatha, TM akatabasamu kisha akamwambia, "unaweza kwenda binti yangu" sauti yake haikubeba hisia zozote za ubaba kwa mtoto wake na ikawa kama anamwambia mfanyakazi wake tu.

"Asante boss" Renatha akageuka na kuondoka huku macho ya TM yakimwangalia mpaka alipoona mlango umefungwa.

"Ubishi kama wangu" akawaza moyoni.

*********************

"Unataka kuniambia unamruhusu Lyn kuwa karibu nawe sababu unaogopa taswira yako kwa walimwengu?" Brian alimuuliza Edrian asubuhi ya leo kwenye simu

"Bro, ninahitaji ushahidi mdogo tu ili kumfunga kabisa kinywa Lyn." Ed akiwa ofisini aliongea na simu

"Ooooh na je Aretha kasemaje! Anakubaliana na huo mpango?" Akauliza kwa kujali Bri

"Amekubali japokuwa najua ana mashaka nao, Bri unanifahamu, tena wewe ulishasema Lyn sio msafi kama nilivyomuona.. nataka kutafuta uchafu wake kidogo ili niwe na kitu cha kumshika atulie"

Ed akashusha pumzi na kukuna kidevu chake...

"Okay, nafikiri utahitaji kuanzia kule ambako Derrick alimuona. Mtumie D, anaweza kuchimba taarifa za yule mtu ambaye alikutana nae..huko S.A. Joselyn sio 'innocent' kama alivyo hapa"

"Sawa bro, nakubaliana nawe."

"Kitu kingine Ed....Rose anaomba mje na Aretha wikiendi hii" Bri akamjulisha

"Hahahahha sasa Rose bado yuko mapumziko, tutamsumbua" Ed akawa na wasi wasi

"Aiisee mlete Aretha mtu asije akagoma kula unanielewa eeeeh!" Bri akasisitiza kwa utani

"Ha ha aha haya baba mtarajiwa...nitaongea na Retha... mwanachuo yule" Ed akamjibu huku akicheka

Walipomaliza mazungumzo akakata simu na kisha akampigia Derrick ambaye kwa wakati huo hakupokea bali akamtumia ujumbe kuwa alikuwa darasani. Akataka kumpigia Captain lakini akamtumia ujumbe akamjulisha kuwa ataenda kuonana nae jioni ile.

Akarudisha macho kwenye kompyuta iliyokuwa mbele yake na vidole vyake vikawa vikipanda na kushusha ripoti mbalimbali za SGC. Muda mfupi baadae Loy akamjulisha uwepo wa Renatha aliyehitaji kuongea nae. Akamruhusu kuingia huku macho yake yakiwa yamekamatwa na barua pepe moja iliyotoa ripoti ya makosa yaliyofanyika kwenye mgodi wao wa G-Town, akakaza macho kusoma, hata sauti ya mlango iliposikika kufunguliwa bado hakubanduka kwenye kioo cha kompyuta.

"Habari Ed ahm. .Mr Simunge" sauti ya Renatha ilisikika akiwa amesimama hatua chache kutoka ilipokuwa meza ya Ed

"Salama, Renatha, nikusaidie nini?" Ed akajibu pasipo kumwangalia

Renatha akajikaza na kuendelea japo alijisikia vibaya kuona Ed hakumpa umakini wowote

"Naweza kuketi?" Akauliza

Ndipo Ed akainua uso wake kumwangalia Renatha. Muonekano wake asubuhi hii ulimfanya kuwa na mvuto wa tofauti. Renatha alivaa sketi nyeusi na alichomekea kwenye blauzi ya rangi ya bluu. Nywele zake alizibana pamoja huku akiachia chache zilizoanguka upande mmoja.

"Karibu uketi"