Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 109 - SALAMA NAWE

Chapter 109 - SALAMA NAWE

"Edrian, binti yangu bado mchanga sana kukutana na misukosuko kama hii. Najua kwa sasa siwezi kumwambia chochote kwa kuwa amekwisha kukupa maamuzi yake lakini nahofia usalama wake. Hajui mambo mengi na anachojua sasa ni hizo hisia alizonazo juu yako. Anaamini ataweza kupambana lakini bado hajakutana na visiki." Mama yake Aretha aliongea kwa huzuni baada ya Edrian kumsimulia machache yaliyohusiana na Joselyn na namna ambavyo wanajaribu kulishughulikia jambo hilo

"Mama ninajua hakuna mtu anayeweza kukubali binti yake awe katika hali hii. Nakuomba unipe nafasi na nakuhakikishia mama atakuwa salama. Nitaghairi ikiwa kutakuwa na dalili zote za hatari kwake." Edrian akamhakikishia mama yake Aretha.

"Kama nilivyokuomba tangu awali, binti yangu anahitaji kuingia katika ulimwengu wa sasa kupitia mikono yake. Msaidie hapo huku hayo mengine ukiyarekebisha taratibu" mama yake Aretha akamuomba Ed

"Bila shaka kabisa mama, nitafanya kila kitu na wewe utakuwa shahidi mama"

Baada ya mazungumzo hayo mafupi Ed akainuka huku mama yake Aretha akielekea chumbani kwa binti yake kumpa taarifa Coletha, ambaye alikuwa akiendelea kupiga stori na Aretha.

Baadae waliaga na kuondoka kurudi nyumbani. Kwenye gari mara kadhaa Coletha alijaribu kumuuliza kaka maswali ya kichokozi kujua nini kinaendelea kati yake na Aretha lakini hakupata majibu ya moja kwa moja.

"Coletha please quit... najua unataka kujua, wakati ukifika nitakwambia"

"Brother, aargh! Najua Joselyn na wewe hamuwezi kuwa pamoja hata mara moja, nyie ni pande mbili za dunia ambazo hazitaweza kukutana!"

Ed akamwangalia kwa jicho la mshangao Coletha, "nani kakuambia" akamuuliza huku akitabasamu

"Aaai Bro, nilishuhudia ulipokuja Jumamosi siku ile na namna uliniuliza kwenye simu kama Aretha yupo ...nilijua kabisa maombi yangu yamejibiwa" Coletha kwa ujasiri wote akamjibu Ed

"Maombi gani hayo Coletha ha ha ha" Ed akacheka taratibu na kuuliza

Bro nayajua mwenyewe ila niliyaomba kwa bidii ile mbaya, lakini kaka Aretha yuko poa sana hana ujeuri kam__"

"Coletha" Ed akamuita akimkatisha

Coletha akamuangalia kaka yake na alipoona ile sura akajua amevuka mpaka

"Samahani bro" Coletha akaomba msamaha lakini alipomuangalia vyema kaka yake aliona tabasamu lake

"Coletha, naomba umchukulie kuwa rafiki uliyempata, hayo mengine unayowaza yaache kwanza" Edrian akaona amuweke sawa mdogo wake kwa kuwa alijua asipofanya vile Coletha atafanya mkakati wao uwe mgumu.

"Aaaah bila shaka bro, mimi nampenda bure yule dada" Coletha akamjibu kaka yake kwa furaha baada ya kusikia ombi la kaka yake..

Wakaendelea na safari ya kurudi nyumbani kwa furaha japokuwa Ed aliendelea kutafakari kwa kina ni kona gani aitumie kumbana Joselyn.

******************

"Retha mwanangu una uhakika na haya maamuzi unayofanya maana ni wazi kuwa huna uzoefu na mapenzi mwanangu"

Aretha ambaye mwanzo alijitahidi kuepukana na mazungumzo haya lakini hakuweza kufua dafu mbele ya mama yake!

"Mama sijui ila nafikiri kumsaidia Ria.aah..Edrian kuwa na furaha. Nisamehe kwa kuwa sijui ni kwa namna gani nitafanya ila kumsaidia kwenye mipango yake itanipa farijiko" Aretha akaongea taratibu akiminya vidole vyake huku akikwepa kuyaangalia macho ya mama yake..

"Lakini mwanangu unamjua huyo binti? Ni vyema ukajiribu kumuepuka, kwanza kwa alivyonieleza Simunge anaonesha kuwa ni mtu wa shari. Nakuhofia mwanangu sababu nakujua hapendi shari"

Aretha akashusha pumzi na kuinua uso kumwangalia mama yake kisha akasema, "sipendi shari mama, nitajaribu kumuepuka ila asijaribu kumchukua Edrian kwa nguvu.. nitajifunza kuwa kama yeye"

Mama yake Aretha akashtuka baada ya kusikia maneno hayo akatabasamu na kumsogelea binti yake, "usiwe mgomvi sababu ya kupenda mwanangu, Simunge anakupenda hilo liko wazi usoni kwake. Lakini usikubali mtu akuburuze hovyo. Nafurahia kuona umebadilika haraka kupambania yaliyo yako"

Akamkumbatia na kisha akainuka kuondoka akimuacha Aretha akijishangaa mwenyewe kwa msukumo uliompata ghafla wa kumkabili Joselyn.

"I love you Rian... natumaini hatua hii ninaichukua salama nawe" akawaza moyoni taratibu.