Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 106 - NILIKUWAZIA

Chapter 106 - NILIKUWAZIA

Aretha akamwangalia kwa mshangao Ed usoni asiamini kama maneno yake aliyaelewa vyema

"Lakini Ria__" kabla ya kumaliza alichotamani kusema macho ya Edrian yakimwelekea Aretha mara moja kabla ya kurudi barabarani

"Retha, unaogopa kuja kwangu?" Aliuliza Ed kwa sauti yenye kujali

"No..no Rian, namaanisha hivi...aaaah" Aretha akameza mate ili kumwelezea lakini Ed akamuwahi

"Princess hakuna sababu ya kuwa na shaka, utakuwa salama na acha mawazo mabaya eeh"

"Aaah mimi na mawazo mabaya hapana" Aretha akatikisika kichwa kukataa

"Okay Retha, kuna vitu tunahitaji kuviongelea na sehemu nzuri ni pale nyumbani ofisini kwangu!" Edrian akamueleza

"Aaaahm, una ofisi nyumbani!" Akauliza kwa sauti ya chini ambayo Ed aliisikia

"Yes Retha"

Kimya kikapita kati yao, Edrian akili yake iliwaza ni kwa namna gani atamueleza Aretha. Hakuwa anajua litapokelewaje na binti huyu, alihofia kumpoteza Aretha. Alikusudia kutumia maelezo yote na ikibidi hata usaidizi wa ndugu zake kumhakikishia Aretha kuwa anampenda.

Kwa upande wa Aretha mawazo yake yalikuwa kwenye nini kimemfanya Ed ampeleke nyumbani kwake. Wangeweza kuongea hata kwenye gari, lakini kila alipofikiria kuwa nyumbani kwa Edrian mapigo ya moyo yaliongezeka na akajikuta anakunja mikono na kuvunja vidole vyake.

Baada ya dakika kadhaa walisimama kwenye geti la nyumbani kwake Edrian. Geti likafunguliwa na mlinzi, akamsalimia kabla ya kuendesha hadi eneo la maegesho.

"Karibu Retha" Edrian akamkaribisha mara alipoegesha gari. Wakashuka na kumpa hakikisho na faraja Ed akamshika mkono Aretha wakaelekea ndani, na kabla ya kuingia mlango ulifunguliwa.

Macho ya Coletha yakakutana na picha ambayo ilimfanya aachie tabasamu murua huku akimwangalia kaka yake

"Kaka leo mapema sana eeeh...karibu Aretha"

Ed akajua kinachoendelea kwenye kichwa cha mdogo wake akatabasamu wakati huo Aretha alikuwa akijaribu kutoa mkono wake uliokamatwa vyema na mkono wa Ed lakini alichoambulia ni mkono kukamatwa zaidi. Akaiitikia salamu ya Coletha,

"Asante Coletha za tangu jumamosi"

"Ni njema tu, nimefurahi sana kukuona" tabasamu halikuondoka usoni kwa Coletha.

"Baby sisy, umesimama mlangoni" Edrian akamshtua Coletha ambaye muda wote aliongea huku kasimama mlangoni. Akasogea na kuwapisha waingie ndani, akutegemea wangekaa sebuleni lakini hawakukaa. Wakaelekea kwenye ngazi zilizopandisha juu kwenda ofisini kwa Ed.

Macho ya Aretha yaliangaza huku na kule akiangalia mandhari nzuri ya ndani ya nyumba ile. Kuta zilinakishiwa kwa rangi nyeupe na kijivu, huku sehemu za picha zikibeba picha za madini tofauti.

"Anapenda madini kweli Rian" aliwaza Aretha mpaka aliposhtuliwa na funguo zilizofungua mlango na wakaingia ndani ya ofisi hii.

"Karibu Retha" Ed akamuelekeza kwenye kochi lililokuwa mbele yao.

"Asante Rian, hii ni ofisi yako haaa...nzuri mno" Aretha akaendelea kuishangaa kwa namna ilivyokuwa. Haikulingana na ile ya Ashante kwa ukubwa lakini ilipangiliwa na mvuto wa kipekee ulivuta macho ya Aretha.

Edrian akakaa pembeni ya Aretha na akaendelea..

"Retha"

Aretha akageuka na kumwangalia usoni Ed, "Abee"

"Utatumia nini?"

"Haaa hapana, nimetosheka, ile juisi ilinishibisha sana"

"Oooh basi sawa. Kuna biskuti zaweza kufaa wakati tunaongea" Ed akaendelea kumuonesha kujali kwake Aretha

"Biskuti sawa"

Ed akainuka na kusogea ilipo droo ya meza yake akavuta na kutoa boksi moja la biskuti.

"Nilinunua tena kama niliwaza siku moja utazihitaji hapa" akasema Ed baada ya kumkabidhi Aretha zile biskuti. Tabasamu la Aretha likauyeyusha moyo wa Ed.

"Ooooh Rian... Asante sana tena sana" Aretha akashukuru na kuanza kutafuna moja aliyoitoa tayari.

"For you princess" akasema maneno haya Ed huku akitabasamu kabla ya kuendelea na kila kiliwaleta.

"Retha, nakuomba unisikilize kwa makini" Ed akaanza kitendo kilichomfanya Aretha aweke boksi pembeni na kusikiliza kwa makini.

"Tangu siku niliyokutana na wewe kwenye Rising Star Show, hisia zangu zilivutiwa sana nawe. Moyo wangu haukuwahi kutulia, nilitamani kukufahamu zaidi. Nilijitahidi sana kuamini kuwa si kitu zile hisia zilikuwa za kipindi kifupi" Ed akajieleza