Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 107 - ATAISHI HAPA

Chapter 107 - ATAISHI HAPA

"Hellow kaka Li!" Coletha aliongea kwenye simu na kujibiwa upande wa pili

"Vipi Coletha" sauti ya Li upande wa pili ilisikika

"Mambo huku nyumbani ni moto kaka" Coletha akaanzisha

"Kuna nini tena" Li akauliza kwa mshtuko

"Shtuka pole pole kaka, Aretha yuko hapa na BB" Coletha akaongea kwa sauti ya chini

"What" Li akashangaa zaidi na kabla ya kusema zaidi Coletha akamuwahi

"Kaka naenda ofisini nisikilize wanaongea nini?"

"Aah hapana, eeeh baby sis usijaribu kufanya hivyo un___?"

"Najua unataka kusema ni umbea katika viwango vya juu, lakini kaka__"

"Sssshhhs Coletha heshimu uhuru wao, utajua tu bila shaka matokeo ya mazungumzo yao" Li akamsihi Coletha ambaye alitamani kujua nini kiliongelewa ndani ofisini.

Aaaah haya kaka, naomba BB asiharibu jamani, nampenda huyu dada, yule kisirani huko aliko azimie na asiamke ." Coletha akalalama akimuacha Li na kicheko

"Hahhaha mdogo wangu we ni muuaji"

"Wala hata, panzi mwenyewe siwezi kuua daaah"

*********************

"Tangu siku niliyokutana na wewe kwenye Rising Star Show, hisia zangu zilivutiwa sana nawe. Moyo wangu haukuwahi kutulia, nilitamani kukufahamu zaidi. Nilijitahidi sana kuamini kuwa si kitu zile hisia, zilikuwa za kipindi kifupi" Ed akajieleza

"Haikuwa rahisi kukufikia Retha ila ninaamini kuna nguvu ilinivuta kwako kwa msaada wa mazingira" akashusha pumzi na kuendelea

"1Sikuwa namfahamu vya kutosha Joselyn, kama nilivyokwambia kuhusu zile picha. Inavyoonesha anataka kuzisambaza katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, anatumia kila alichonacho kwenda kinyume nami. Retha sio kwamba naogopa ikiwa atafanya la hasha ila kinachonisumbua ni taswira yangu katika jamii. Namna ambavyo jamii yangu imenifahamu itaharibika, atatafuta kuonewa huruma nami nitaonekana mbaya na kila__" kabla ya kuendelea alishtushwa na kitendo ambacho Aretha alifanya, alimkumbatia ghafla akashindwa kuendelea

Katika udogo wa mikono yake alimkumbatia hasa Edrian, hakuwa na nanna zaidi ya kumkumbatia nae, maneno yaliyofuata kutoka kinywani kwa Aretha yakamshtusha

"Am sorry Rian"

Akamshika mabega na kumrudisha nyuma kidogo huku akimwangalia machoni ambapo alikutana na machozi yaliyokuwa yakitiririka usoni kwa Aretha.. akachukua kitambaa na kumfuta. .

"Retha mbona unalia?" Akamuuliza baada ya kumfuta machozi Aretha ambaye hakuweza kuinua macho yake kumuangalia Ed sababu ya kulia na hata maneno yalikwama kooni kwake asiweze kusema..

Edrian akamvuta tena na kumkumbatia, "Retha tafadhali usilie, kwa nini uniombe radhi wakati mwenye makosa ni mimi"

Aliposema hivyo Aretha akajitahidi kuongea "unapata hayo kwa sababu ya mimi Rian__"

"Hapana Retha, hata bila wewe Joselyn angefanya tu ili kunisukuma kufanya kile anataka kitokee" akaweka kidevu chake kichwani kwa Aretha

Baada ya kukaa kwa sekunde kadhaa akiwa amemkumbatia, alipoona hakuna tena dalili za kulia kutoka kwa Aretha akamwachia na kumsogeza mbele kisha akamwangalia usoni

"Rian" Aretha akamuita kwa sauti ya upole

"Naam" akaitika

"Kwa hiyo tutafanyaje?" Akauliza Aretha

Edrian alivyosikia "tutafanyaje" ni kama taa iliwaka kwenye kichwa chake akaamua kumuelezea wazo aliloamua kuendelea nalo kutoka kwa mama yake.

"Kwa hiyo mama anafahamu kuwa mimi aah___"

"Ndio Retha, mama anajua ni kwa kiasi gani nakupenda" Ed akajibu

"Aahm..aa..kwa hiyo unaamini kuwa mtego mtakaomtegea Lyn ataangukia hapo?" Aretha akauliza

Ed akatikisa kichwa kabla ya kusema huku akihisi wepesi katika muelekeo wa mazungumzo yao.

"Ndio Retha, ninahitaji karata moja kama aliyonayo, atakapoicheza nami nitaiweka yangu"

Kimya kifupi kikapita kati yao, Ed akapata wasi wasi ikiwa Aretha angekubaliana na kile alichokiomba au la! Hakujua afanye nini ikiwa angekataa

"Retha kama hautaki niambie tu princess, tutatafuta namna nyingine ya__"

"Rian kama ingekuwepo najua hata usingesubiri niseme" Aretha akajibu kisha akainama akiangalia mikono ya Edrian ambayo ilikuwa imeshika viganja vya mikono yake

"Rian naweza kukubaliana na kila kitu ila niwe muwazi tu kwako...sijui kama itakuwa rahisi kwangu iwapo ataishi hapa kwako" Aretha akamwambia..