"Okay babe, nitakupa muda" Lyn akaongea huku akiwa ameegama kwenye mgongo wa Lyn. Mwili wa Ed ukakakamaa kama aliyepigwa na radi, uso wake ukajikunja na kifua chake kikipanda na kushuka.
Akajisikia usaliti mkuu, "what is this" akijiuliza maana ni kama mtu alipitisha list kikali moyoni mwake. Akamkumbuka Aretha aliyeko nje, akawaza ni jana tu walianza safari ya penzi lao lakini hata kabla ya mwezi amemsaliti na mikono ya Lyn inamgusa sasa.
Akaishika mikono kutoka tumboni akageuka na kumwangalia Lyn moyo wake ukaongea "utalipa kwa kila uchungu unaompa mwanamke ninayempenda"
"Sawa Lyn, sasa nakuomba utulie hapa mama anakuja kuongea nawe kwa muda mfupi. Niko nje" Ed akasema akiwa ameishika mikono ya Lyn ambaye alikuwa na tabasamu lake ovu usoni.
"Okay" Lyn akarudi na kuleti kitandani baada ya Ed kumwachia huku akimgusa begani
Ed akaelekea mlangoni lakini maneno yaliyofuata ya Lyn karibia yaharibu kile alichokianzisha...
"Edrian, sitaki kukuona na Aretha, hilo ni sharti langu"
"Mmmmm"akaguna hakugeuka kumuangalia Lyn akatoka nje mikono yake ikiwa imekunja ngumi. Akatembea mpaka alipoona hawezi kuvumilia tena akapiga ngumi ukuta mara tatu kitendo kilichofanya mama yake aliyekuwa akitoka sebuleni kumuona.
"Aishhsss Ed hebu acha hayo mambo"
"Mama unanifundisha kuongopa wakati unajua nisivyoweza sijui kama nitaendelea" Ed akamlalamikia mama yake aliposogea
"Mwanangu usijali ni kwa muda mfupi tu kabla hajakuharibia taswira tutamuwahi.. haya nenda kwa mkeo mwambie kila kitu akikubali sawa, akikataa tutaacha. Nipigie baadae" Mama akaelekea chumba alichokuwepo Lyn akimuacha Ed aliyeelekea nje.
Huko nje Aretha alimsubiri Ed huku wasi wasi mwingi ukimpata kwa namna alivyoona muda ukienda. Mawazo ya wivu nayo yakaanza kumwingia, akataka kushuka aondoke lakini Ann alifika na kugonga kwenye kioo na kumfanya afungue mlango. Baada ya kupewa juisi na maagizo ya Ed walau akatulia. Akanywa juisi na kuzamisha mawazo yake kwenye simu mpaka mlango ulipofunguliwa na Ed kuingia.
"Rian...umeumizwa na nini?" Aretha akamuuliza Ed mara tu alipoingia na kukaa tayari kuondoa gari.
"Retha samahani sana, nitakwambia ngoja tuondoke kwanza hapa." Akasema na kuondoa gari huku mlinzi akifungua geti Ed aliondoa gari kwa spidi ambayo ilimshtua Aretha ambaye akabaki anamwangalia usoni. Walipoingia barabara kuu Ed akarudisha macho kumwangalia Aretha, akachukua simu kwa mkono mwingine akafungua kioo na kisha akaamuru impigie mama yake Aretha...
Akairudisha na kusubiri simu iliyokuwa ikiita huku akitumia "bluetooth ear pods"
"Hello mama" Edrian akaita kwa sauti ya utulivu,
"Salama mama" akaendelea kuitikia mazungumzo yake na mama ambapo alimuomba kuwa angechelewa kidogo kumrudisha Aretha na atakapofika atampa maelezo ya kwa nini imekuwa hivyo.
Aretha ambaye alimsikiliza Ed huku akikunja na kukunjua mikono yake,
"Rian" Aretha alimuita Ed mara tu alipokata simu, macho yake yakimwangalia kitendo ambacho kilimfanya Ed kujisikia vibaya zaidi na kusababisha kuongeza mwendo akimshtua zaidi aliyekuwa pembeni yake..
"Yes Retha" akaitika
"Unajua sipendi kukuona hivyo, tafadhali ruhusu amani na si machafuko" akasema kwa upole
"Eeehm" Ed hakuelewa kuwa alipigwa na butwaa hata akashtuka mbele kuna gari zimesimama akakanyaga breki kwa haraka...
Aretha akafumba macho mpaka gari iliposimama...
Edrian akageuka na kumuomba samahani Aretha huku akimuuliza kama yuko sawa
"Niko salama Rian and please relax..nitakusikiliza usiache uchungu uendeshe hisia zako" wakati akisema maneno hayo gari ziliruhusiwa kuondoka na Ed akaendesha na sasa alikwenda kwa spidi ya kawaida huku akimtupia jicho Aretha kisha akasema
"Retha, ninataka tuongee na nahisi itachukua muda, nimemuomba mama ruhusa ili asiwe na wasi wasi"
"Nimekusikia Rian, wakati mwingine niamini na unipe nafasi nimwambie mwenyewe"
"Oooh sawa, nilidhani ni rahisi nikimwambia mimi" Ed akajitetea
"Tunaenda wapi Rian?" Akauliza Aretha baada ya kuona mwelekeo ambao haufahamu
"Nyumbani kwangu Retha" Ed akamjibu na kuangalia mwitikio wake ungekuwaje
Aretha akamwangalia kwa mshangao Ed usoni asiamini