Kuongea na Lyn kilikuwa ni kitu cha mwisho angetamani kufanya lakini aliamini mama yake atakuwa ameona mbali zaidi ya hisia zake.
"Okay mama lakini__" kabla Ed hajamaliza mama akamkatisha
"Usihofu mwanangu mengine utajua nini cha kufanya, ana mambo anayoweza yatumia kukuchafua na ikapita muda kujisafisha. Mtulize kwanza halafu tafuta pointi ya udhaifu wake ili atakapojaribu kukuinukia una karata mkononi. Nenda kamtulize"
Ed akainuka kwa kujilazimisha hakujua afanye nini hasa, wiki moja alikosa utulivu akishughulika na visa vya Lyn. "Ngoja nizungumze na huyu binti mgonjwa ananikosesha amani na Aretha" akawaza moyoni mwake huku akipiga hatua kuelekea kwenye chumba cha wageni aliamini Ann atakuwa bado yuko huko ampeleke.
Alikutana na Ann akielekea chumbani kwa Lyn akiwa jagi lenye maji, akamuomba lile jagi ili apeleke, yeye mwenyewe.
"Kaandae juisi kwenye glasi halafu nenda kwenye gari yangu hapo nje kuna mtu mpe mwambie nimekutuma, na mwambie anisubiri."
Ed hakuwa na simu aliiacha kwenye gari kwa kujua kutakuwa kitakuwa kitu cha muda mfupi!
Alipomaliza kumpa maagizo akaelekea chumba alichopumzika Lyn, akasimama mlangoni na kushusha pumzi. Akagonga. Sauti ya Lyn ikasikika akimruhusu kuingia, akafunga mlango taratibu,
"Hauwezi kutumwa kitu ukawahi eeeh" Lyn ambaye alizungumza macho yake yakiwa kwenye kioo cha simu hakujua kama ni Ed aliyeingia mle chumbani,
"Mimina hayo maji unipishe nina kazi ya muhimu" Lyn akaongeza huku akiendelea kugusa kwenye simu yake.
"Mhhh" Ed akaguna kitendo kilichomfanya Lyn kumuangalia na mshtuko mkuu kuonekana usoni mwake, akasimama
"Ed ni wewe?" Akajaribu kujiweka sawa!
Ed akasogea, akaweka jagi la maji mezani, akachukua glasi na kumimina maji kisha akaelekea aliposimama Lyn na kumkabidhi
"Samahani, nimechelewa" maneno yalitoka kati ya meno ya Ed akajitahidi kutoonesha hali ya kujilazimisha.
"Sorry babe, sikujua kama ni wewe...umenishangaza sana"
"Unachoshangaa nini Lyn, uko kwetu, ni jambo la kawaida mwenyeji kuwa mkarimu kwa mgeni wake." Ed akamjibu na kuelekea kukaa kwenye kiti kilichokuwa pembeni. Kabla Lyn hajapata jibu la kufaa Ed akaendelea
"We need to talk Lyn"
"Talk about what Ed?" Lyn akauliza huku alizungusha jicho na kitabasamu cha mbali lilionekana usoni kwake
"Kaa" Lyn akakaa baada ya kusikia maneno ya Ed ambayo yalikuwa na amri ndani yake. Akamwangalia Ed ambaye naye hakuondoa macho yake usoni pake.
"Joselyn, najua kumekuwa na mambo mengi ambayo yameendelea, yametuathiri sote na inawezekana hatutumii utashi wetu vyema. Naomba unipe muda niweke sawa mambo haya ili tuendelee pasipokuwa na tashwishwi iliyopo sasa" Maneno haya yalitoka kinywani kwa Ed kwa shida, alihisi kama kalazimishwa kumeza jiwe.
"Ah haha ha Ed uko sawa au unanitania?" Lyn akamuuliza
"Kama natania kwa nini nipo hapa? Ed akamwangalia kwa ukali..
"Okay...Okay, tuseme hivi unamaanisha hayutaachana?"
Ed akameza mate, "kwa nini niseme kitu ambacho si kweli aaah mama mpango wako unaniumiza sana" Ed akawaza moyoni lakini alijua ukweli kwa wakati huo sio kitu ambacho Lyn anakielewa zaidi.
"Kama mazingira utayamudu tutakuwa pamoja" Ed akajibu
"Unamaanisha nini Ed?" Ed aliposikia Lyn akiuliza hivi akaachia tabasamu na akakumbuka kitu
"Baba yako aiache kampuni yangu na kama mnashirikiana sitaweza kuwa na mtoto wa adui yangu, na pili sitaki hizi drama zako, grow up Lyn"
"Hahahaha Edrian, baba yangu hahusiki, na hizi unazoziita drama ni mapenzi tu"
"Mapenzi gani hayo" akawaza Ed moyoni. Akainuka na kumsogelea Lyn "Zile picha nilikwambia hazitamsumbua Aretha kwa sababu mimi na yeye tunakitu tofauti na wewe unavyodhani."
"Mh, mbona Salim aliwaona leo umemshika kiuno, Ed unadhani mimi ni mjinga, najua unampenda yule binti"
"Kwa hiyo kama nimemshika kiuno inamaanisha ndio nampenda kwako eeeh Lyn"
Lyn akabaki akamwangalia Ed usoni..
"Chagua kuniamini au amini mawazo yako. Au tusirudiane tu" akaanza kuondoka Ed huku usoni akiweka tabasamu akiamini mpango wa mama yake utafeli tu. Lakini kabla ya kufika mlangoni mikono ya Lyn ikazunguka tumboni kwake
"Okay babe, nitakupa muda"