Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 103 - MUIGIAJI MKUU

Chapter 103 - MUIGIAJI MKUU

"Mama" akamuita huku akizuia mguu wake usiendelee mbele kumbusu mama yake kwa sababu adui yake wa sasa aliketi chini huku kichwa chake kikiwa magotini kwa mama yake na Edrian. Macho yake yalimwangalia Lyn ambaye hakugeuka hata kidogo.

"Karibu mwanangu" mama yake akamkaribisha.

"Asante mama" Ed hakukaa akabaki kasimama

Mama yake akamshika mabega na kumsogeza mbele Lyn kisha akaita

"Ann" sauti ya kuitika ilisikika nje. Akaingia Ann, mama yake Edrian akamwambia Lyn "binti yangu hebu nenda kasafishe uso wako, halafu ukiona vyema pumzika mpaka utakapojisikia vyema kwenda nyumbani"

"Mama" Ed akamuita mama yake kwa mshangao wa kile alichomwambia Lyn. Mama yake hakuchukulia maanani sauti ya mwanae.

Ann akaingia na kusogea alipokuwa mama yake Ed, "mpeleke kwenye chumba cha wageni ajiweke vizuri" mama akatoa maelekezo kwa yule binti kisha akainama na kumgusa mabegani Lyn, "ngoja niongee na mwenzio kila kitu kitakaa sawa"

Joselyn akainuka na kwa mara ya kwanza akamwangalia Edrian usoni bila kusema neno akamfuata Ann. Kilichomchosha kabisa Ed ni kuona Joselyn alitumia huruma ya mama yake kumlaghai kwani macho yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia. Walipoondoka Lyn na Ann mama yake Edrian akatabasamu na kumuita mwanae akimuonesha sehemu iliyokuwa wazi ubavuni kwake akae ili waongee. Lakini Ed alimwangalia mama yake kwa mshangao namna alivyobadilika kutoka kwenye ukali na ghafla upole,

"Sasa unapoteza muda kwa kusimama unataka nisimame ili tuongee tukiwa hivyo au la" mama yake akamwambia

"Ah hapana mama" Ed akasogea mpaka alipokaa mamaye, akaketi tayari kumsikiliza..

Mama yake akaongea kwa sauti ya chini, "mwanangu ilikuwaje ukampata msichana huyu eeh?"

"Ah" Ed akashangaa swali la mama yake, akamwangalia usoni

"Assshhh, mbona unanishangaa, mdada mwerevu sana huyu, na ujuzi wake wa kuigiza unakaribia wa kwangu!" Maneno ya mama yake Ed kwa mara nyingine yakamuacha na mshangao

"Aah"

"Mwanangu, najua anachofanya huyu binti, sio kwamba sioni, ila nimekufundisha namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali lakini nilisahau somo kubwa la kukabiliana na sisi wanawake" mama yake akaangalia huku na kule kama kuna mtu alikuwa akiwasikia kisha akaendelea

"Aina hii ya mwanamke Edrian mwanangu anahitaji mpango mkakati kabla ya kumuacha. Huyu hatakubali kushindwa kirahisi ni aidha mkose wote au apate yeye"

Ed ambaye kwanza alikuwa hajaelewa chochote ghafla ni kama taa iliwaka kichwani kwake, akageuka na kumwangalia mama yake akashusha pumzi kidogo huku akitikisa kichwa kwa namna mama yake alivyomshangaza.

"Mama kumbe unaelewa anachofanya?" Akauliza swali ambalo majibu alikuwa nayo, mama yake akatabasamu,

"Sasa nisikie, Aretha anahitaji kujua a hadi z ya kila kinachotokea ili mambo yako yakiguswa asiwe mwepesi kuyumbishwa"

Edrian akakumbuka kuwa Aretha yuko nje, "Mama nimekuja nae ila ameomba asiingie ndani baada ya kuona gari ya Joselyn hapo nje"

"Eehm, binti ana akili oooh, nimeikumbuka na aibu zake! Sasa nataka ufanye kitu kimoja, nenda kaongee na Lyn" mama yake akamwambia huku akimgusa begani

"Mama..sitaki hata___"

"Edrian, nisikie la sivyo atakuchafua sana huyu mwanamke, ni mwerevu nakwambia. Utampata Aretha lakini sura yako itachafuliwa"

"Mama hilo halinisumbu__" mama akamkatisha

"Linaweza lisikusumbue sasa lakini litakusumbua mwanangu, umekaa bila kuwa na mwanamke kwa sababu ulitaka kujenga taswira njema, sasa umepata mwanamke unataka kuibomoa, kwa nini uliijenga mara ya kwanza? Ili uibomoe Edrian? Hapana. Nadhani hata huyo Aretha hatakuacha uibomoe"

Edrian akayatafakari maneno yale kutoka kwa mama yake akakubaliana nae. Kama mwanzo alijenga taswira hiyo si vizuri kile alichokuwa anakiandaa kije kuharibu tena taswira yake. Akajilaumu kwa kutokuwa makini na Joselyn.

"Okay mama, nitaongea nini na Lyn? Amekuja ofisini na picha kunitishia kumpelekea Aretha!" Ed akamuuliza mama yake huku mikono yake akiikunja kifuani

"Aaah kakutishia, assh amekusudia kukuharibia. Ila anachofanya mimi nakielewa zaidi. Mwambie utajaribu kufikiri upya hili swala ila kwa sasa akupe utulivu"

"Mmmhhh" Ed akashusha pumzi