Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 102 - SHE IS CUTE

Chapter 102 - SHE IS CUTE

Nataka watu wote waone kuwa nimependwa na mimi ninaweza kupenda" mikono ya Ed haikumuachia bali aliendelea kumbusu kichwani.

Alipoona ametosheka kwa kumbatio lile Ed akamwachia Aretha kisha akashusha busu kwenye paji la uso la binti yule, akawasha gari kuondoka. Aretha aliibia kumuangalia Ed mara kadhaa akikutana na tabasamu lake usoni.

"She is so cute to love" akawaza Ed, mwisho wa mawazo yake ulileta tabasamu. Muelekeo wa safari yao ulikuwa kwao Aretha kuchukua picha ambayo ilikuwa maalum kwa ajili yake.

Simu yake ikaita wakiwa njiani, alipoangalia aliyepiga ni mama yake, akapokea kisha akaweka sikioni, "Hello mama"

"Edrian, uko wapi?" Sauti ya mama yake ilikuwa tulivu lakini Ed alitambua kuna kitu hakiko sawa.

"Niko barabarani naendesha mama..uko sawa?"

"Unaweza kupata muda ukaja nyumbani sasa?" Maneno haya yalikuja kwa upole lakini kulikuwa kuna amri nyuma yake

"Mmmmm" akaguna Ed

"Edrian Simunge nasema hivi nakuhitaji uje nyumbani mara moja"

"Mama inakuwaje kuhusu ma___?"

"Mwanangu unataka nipige magoti kwa ajili ya kukuomba uje nyumbani? Asssshh yaani mara moja hii nakuomba uje lakini una_____?

"Okay mama nakuja" akakata simu, sura yake ilibeba mashaka

"Kuna shida kwa mama" Aretha akamuuliza taratibu huku akimuangalia usoni

"Mama anataka niende na wakati sio kawaida" Ed akajibu

"Ndio uende Rian, mimi niache tu hapo Vesilisa park, picha yako nitakuletea, lakini ni vizuri kwenda kumuona mama."Aretha akamshauri Edrian na kuangalia begi lake kwenye viti vya nyuma na kuliweka mapajani mwake

Ed alipokaribia Vesilisa Park akaegesha gari akamwangalia Aretha ambaye alimshukuru kwa chakula cha mchana. Aretha akainuka kidogo na kumbusu shavuni Ed akafungua mlango ili atoke lakini mlango ukawa haufunguki, akageuka haraka kumuuliza tabasamu alilokutana nalo likamshangaza huku likifuatiwa na mkono wa Ed ambao ulichukua begi na kulirudisha mahali lililokuwa.

"Tunaenda wote Retha" akasogea na kuvuta mkanda akaufunga tena akimuacha Aretha katika bumbuazi zito. Akaondoa gari kuelekea njia iliyoekea barabara kuu la kuelekea River Estate

"Rian...siwezi kwenda kwa mama hivi" Aretha akamjibu huku akijiangalia

"Retha princess, kama macho yangu yamekukubali basi ujue na ya mama yatakukubali" Ed akamuondoa hofu

"Lakini..Rian mama anaweza kuwa na kitu cha msingi anataka kuongea nawe na mimi___"

"Na wewe utamzuia .... kusema Retha?"

Kuna namna Aretha alihofia, lakini kumwelesha Edrian kwa wakati huo ilikuwa ni kazi bure kwa kuwa mwanaume huyu alikanyaga mafuta kuonesha alichokiamua hakiwezi kubadilika.

Ndani ya dakika kumi na tano Edrian alikuwa alipiga honi mbele ya geti la nyumbani kwa mama yake. Akiwa anamwangalia mlinzi aliyekuwa akifungua taratibu gari, aligundua hali ya wasi wasi aliyokuwa nayo Aretha. Akaweka mkono wake wa kushoto juu ya ule wa Aretha na akaubinya kumpa uhakika

"Hakuna sababu ya kuogopa Retha."

Aretha akatabasamu na kutikisa kichwa kukubaliana na kile Ed alisema. Akashusha pumzi na wakati huo Ed akaendesha kuingia ndani. Mbele yake aliiona gari ambayo aliitambua na sura yake ikabadilika.

"Anafanya nini tena hapa huyu binti" akawaza moyoni, akatafakari kwa namna gani atamlinda Aretha.

"Retha hilo gari hapo ni la Joselyn atakuwa yupo ndani. Utaingia pamoja nami?" Ed akamuuliza huku moyoni akitamani Aretha akubali ili amuoneshe Lyn kuwa hakuna chochote kitakachombadilisha mawazo hata akiwa mama yake mzazi.

"Rian...mh. .nitabaki kwenye gari wewe waweze kwenda.. nakuomba tu usikasirike."

"Retha una uhakika? Kwenda wote ni__"

Kabla ya Edrian kumaliza, mikono ya Aretha ikagusa uso wake, "Rian naamini maamuzi haya ni mazuri..nenda sasa mama anakusubiri" akamuangalia Aretha akiondoa mikono yake usoni kwake akaegemea kwenye kiti kwa utulivu. Ed akashusha vioo vya gari akashuka kuelekea mlango mkubwa wa nyumba. Ann alikuwa nje akamsalimia na kumkaribisha Ed.

Akaingia ndani ambapo picha aliyokutana nayo ikamfanya akunje ngumi kwenye mkono wake.

"Huyu mwanamke hana aibu kaleta hizo picha hadi kwa mama" akawaza moyoni.

"Mama" akamuita huku akizuia mguu wake usiende mbele kumbusu mama yake.