Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 101 - MWENYE BAHATI

Chapter 101 - MWENYE BAHATI

"Retha unaweza kuongeza, don't be shy" Ed akamwambia Aretha baada ya kuona namna alivyokifurahia chakula.

"Aahh hapana nimetosheka Rian..umeniwekea hadi cha kweli aa yatosha" Aretha akamkatalia kwa aibu, ni kweli chakula kilikuwa na ladha nzuri, mara zote Ed alichukua sehemu chakula na kuweka kwenye sahani yake.

"Tuchukue na cha baadae basi princess" kwa kujua Aretha alifurahia chakula kile, Edrian alitamani kumfurahisha.

"Hapana Rian nimekula leo, siku nyingine nitakula pia" Aretha hakuona sababu ya kuchukua kingine maana aliamini ipo siku watakuja tena pale

"Sawa, nitajitahidi kukuleta hapa" Ed akatabasamu, akaingia kwenye simu yake na kufungua ukurasa wa mgahawa ule, akafanya malipo. Wakawa wakisubiri risiti ndipo waondoke..

Wakaingia wanaume wawili ambao walionekana kuwa na hadhi ya juu kwa ule unadhifu waliokuwa nao kwa mavazi na hate muondoko wao. Mmoja alivaa suti safi yenye rangi ya kijivu huku mkononi saa yake ilionesha kuwa ya gharama kubwa. Mwenzie alivaa shati nyeupe ya mikono mifupi na suruali ya kadeti nyeusi. Kwenye shingo yake kulikuwa na mkufu ulioonesha kuwa na thamani ya dhahabu. Wakapiga hatua kuelekea kwenye meza ambayo ilikuwa karibu na ile waliyokaa Edrian na Aretha.

Lakini walipomuona Ed wakasogea kumsalimia ikionesha kuwa walifahamiana. Uso wa Ed ulibadilika kutoka kwenye tabasamu pana lililojaa usoni wakati akiongea na Aretha hadi kwenye uso wa kikazi zaidi..

"Simunge good to see you" akasema yule aliyevaa suti! Akanyoosha mkono ili kumpa Ed ambaye hakuupokea akabaki na uso usio na changamko lolote akimwangalia.."Good to see you Salim"

"Nakuona una mwanafunzi hapa.. unajaribu kuanza darasa au waanzisha chuo" Salim akamwambia Ed akiwa na tabasamu la dhihaka akitoa macho yake kumuelekea Aretha ambaye hakuinua macho kuwaangalia wageni wale

"Hello mwanafunzi" Salim akasalimia kwa dhihaka kisha akamgeukia mwenzake ambaye alikuwa na tabasamu kama lake "Idris, rafiki yetu anapata mawazo kutoka kwa mwanafunzi ya kuwekeza"

"Sure, Mwenye enzi Simunge anapata mawazo kutoka kwa mwanafunzi wa kike mgahawani" Idris akajibu kwa dhihaka

Edrian akawaangalia lakini kabla ya kusema kitu mhudumu akamletea risiti. Akainuka na kumshika mkono Aretha, "twende Retha"

"Hahaha mighty Simunge umemtupilia mbali mwanamke wa hadhi yako ili kuvumbua nini kwa mwanafunzi!" Salim akacheka na kuongea japokuwa sauti yake haikusikika sana

"I wonder bro, unatupa dhahabu unakumbatia mchanga" Idris naye akaongeza maneno huku akicheka

Edrian ambaye alikuwa amepiga hatua chache akageuka kutaka kuwaambia kitu lakini mkono wa Aretha ulimzuia, alipogeuka kumwangalia usoni, macho ha upole na tabasamu laini vikabadilisha hasira iliyoanza kufuka kama moshi kifuani kwake.

Akawaangalia Salim na Idris akatabasamu na kumshika kiunoni Aretha wakaondoka. Baadhi wa watu wachache waliokuwa wakila waligeuka kuangalia. Hawakusikia kilichoongelewa lakini kuondoka kwa Ed kwa namna ile kulivuta hisia zao.

Walipofika garini, Edrian akamwangalia Aretha na kumwambia "Asante princess..samahani kwa maneno ya wapuuzi wale"

Akatabasamu na kumjibu, "usikasirike Rian, watu husema kile wanachotaka kusema, huwezi kuwazuia. Mama husema kuwa " usizuie watu kukurushia mawe, ila unaweza kuamua nini unafanya na mawe unayotupiwa"

"Ahmmm" Ed akamwangalia na furaha yake ilikuwa kuu, "Retha..unanipa kujisikia kwenye bahati sana kuwa nawe"

Aretha akamwangalia Ed usoni kisha akamwambia "mimi ndiye mwenye bahati kwa kuwa nimekubalika nawe na___"

Ed akamvuta na kumkumbatia kwa nguvu Aretha ambaye alishtushwa na kumbatio lile. Akabaki kifuani kwa Ed huku akisikiliza mapigo yake ya moyo yalivyodunda..

"Retha, natamani ningekuona siku ile, kuna mambo yangekuwa tofauti na yalivyo sasa. Wewe umebeba maisha yangu sasa.. please love me this and that much"

"Rian...tuko kwenye gari watu wanaweza kutuona" Aretha akamtahadharisha Rian

"Unajua kitu nachotamani kufanya sasa Retha?" Ed akamuuliza kwa sauti ya utulivu

"Mmmmmh"

"Nataka watu wote waone kuwa nimependwa na mimi ninaweza kupenda" mikono ya Ed haikumuachia bali aliendelea kumbusu kichwani