Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 100 - SURA YA KIRAFIKI

Chapter 100 - SURA YA KIRAFIKI

Karibu asilimia kubwa ya wafanyakazi waliofanya kazi kwenye jengo hili la Ashanti walipata chakula kwenye mgahawa huu. Mchana huu Loy aliketi kwenye meza peke yake akipata chakula cha mchana. Aliwahi kwa kuwa Ed bosi wake aliondoka mapema. Akaamua kuwahi kabla mgahawa haujajaa watu ili kukabiliana na baadhi ya ratiba za Ed ambazo Allan alikabidhiwa kuziendesha.

"Yes, Loyce" akamjibu Renatha ambaye aliketi bila wasi.

"Ooooh lakini nimesikia wakikuita sana Loy" Renatha akamwambia wakati akijiandaa like chakula chake

Loy akamwangalia Renatha kisha akatikisa kichwa kukubali, akaendelea kula chakula chake ambacho kilielekea kumalizika.

"Nami waweze niita Renee" Renatha akaendelea kujaribu bahati yake kuwa karibu na Loy.

"Sawa" Loy akaitikia na akaendelea na chakula. Kimya cha muda mfupi kilipita kati yao mpaka Renatha alipoamua kuuvunja

"Ugh...Loy, samahani, una muda gani tangu uanze kazi na Ed?"

"Ahhmm..muda mrefu kidogo" Loy akamjibu na akainuka kuondoka

"Loy subiri kidogo muda bado" Renatha akamsihi baada ya kuona anataka kuondoka baada ya kumaliza chakula chake.

"Nina kazi sikumaliza nataka nikazimalizie"

"Nitajitahidi nimalize haraka tutoke wote, bado sijawazoea wengine tafadhali" akamwangalia huku akipepesa macho aonewe huruma

Loy akaketi, "sawa fanya haraka, nina kazi bosi atazihitaji akirudi"

"Edrian ametoka? Kaenda wapi?" Renatha akauliza kwa msisitizo ambao ulimshtua Loy akabaki akimwangalia pasi neno lolote

"Oooh...sorry Loy sikupaswa kumrejea bosi hivyo na sikujua kama ningeuliza kwa namna hiyo" akajaribu kuonesha alikuwa kawaida tu! Lakini kwa upande wa Loy alipata maswali kichwani. Amewezaje kumuita bosi kwa kutumia jina lake la kwanza kama mtu wanayefahamiana naye

"Renee unamfahamu bosi?" Loy akamuuliza mshangao ukiwa wazi usoni

"Ooooh no..no simfahamu moja moja zaidi ya kumuona kwenye mikutano ya wafanyabiashara nguli" Renatha akajitetea kwa haraka kuondoa mshangao ulioonekana wazi kwenye uso wa Loy.

"Aaaah sawa" Loy akaitikia huku akiangalia sahani ya Renatha ambayo hata nusu ilikuwa bado haijafika.

"Ngoja nile upesi" akasema alipogundua Loy kweli alikuwa na haraka.

Akaendelea kula kwa haraka, alipomaliza akamshukuru Loy kumsubiri, wakasimama ili kuondoka. Wakapitia maji ya kunywa kisha wakaelekea ilipo lifti wakasubiri iliyopanda juu kuwapeleka kwenye ghorofa walilotumia

"Kwa hiyo Mr Simunge hakupata lunch kukabiliana kutokana na majukumu mengi eeh?" Renatha akamuuliza Loy mara tu walipoingia kwenye lifti. Kwa kuwa watu wengi walielekea kwenye mgahawa muda huo, walikuwa wawili tu ndani ya lifti.

"Hapana hayuko nje sababu ya majukumu mengi." Majibu haya mafupi ya Loy hakujua kwa kiasi gani yalimpa maswali zaidi Renatha ambaye alitaka kutumia ukaribu wake kwa Loy kumsogelea Edrian.

"Unamaanisha katoka kwa ratiba binafsi eeeh?"

Loy ambaye alianza kukereka na maswali haya akamgeukia Renatha, "Unataka nifukuzwe kazi kukushirikisha mambo ya bosi wangu Renee?"

"Oh hapana, samahani sana Loy, masikio tu yaliwasha kujua" Renatha akaomba msamaha baada ya kuona Loy hataki kumuongelea bosi wao.

Mlango wa lifti ulipofunguka wakatoka na Loy akaanza kuelekea ofisini kwake, lakini alishangaa Renee alimfuata.

"Umepotea njia inayoelekea ofisini kwako Renee?" Loy akasimama na kumuuliza

"Usijali Loy naelekea huko ofisini kwako sababu nina kazi pamoja na Allan" Renatha akaongea huku akiendelea kutembea

"Okay" Loy akaitika na kumfuata nyuma

"Loyce, unaniangalia kama mimi ni adui yako" Renatha akamwambia baada ya Loy kumfikia

"Ahm" Loy akaitika, maneno yale ya Renee yalimfanya ajisikie vibaya kwa namna ambavyo hakumuonesha uchangamfu wowote

"It's okay Loy, mimi sio adui. Ni mfanyakazi mpya nayetafuta kupata rafiki kwenye ofisi hii. Nisamehe kama naonekana nakulazimisha" Renatha akamwambia maneno haya wakiwa wamesimama kwenye mlango uliowapeleka kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mkuu.

"Ooh sio hivyo Renee, hatujazoeana tu" Loy akajitahidi kumuonesha sura ya kirafiki. Lakini hakusahau mambo ambayo Ed aliwapa onyo akiwa na bosi Allan japokuwa alimuona Renatha asiye na makuu.