Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 98 - USIPATE WIVU

Chapter 98 - USIPATE WIVU

Ed akaendesha gari kuelekea kwenye maegesho ya magari hapa Capital University, ilikuwa ni dakika tano baada ya Aretha kutoka darasani. Hakutaka kuonekana maeneo yale hivyo akampa maelekezo ya mahali ambapo aliegesha gari na namba ya gari.

Lakini kabla ya Aretha kumuona, yeye alikuwa we kwanza kumuona. Akawasha taa za Volvo XC60 SUV nyeusi kumuonesha kamuona. Aretha akaachia tabasamu na kuelekea ilipokuwa gari, lakini kabla ya kuifikia gari, kijana mmoja wa kiume akamkimbilia na kumfikia.

"Aretha mbona una haraka sana vipi umemaliza vipindi" Yule kijana akamuuliza huku akiangalia usoni kwa Aretha namna alivyokuwa na wasiwasi akiangalia ilipokuwa gari ya Ed kisha kwake

"Aaahm...ndio nimemaliza Charlz, nina haraka aaah kidogo samahani"

"Oooh sawa, nitakutafuta kwenye simu baadae" Charlz akasogea pembeni kumpisha lakini akabaki amesimama kuona wapi Aretha alielekea

Pasipo wasiwasi Aretha akasogea ilipokuwa gari ya Ed na kabla ya kushika mlango Ed akafungua kwa ndani. Akaingia kwenye gari huku begi lake akiliweka mapajani kwake, lakini Ed akalichukua na kuliweka kiti cha nyuma kisha akamwangalia Aretha, uso wake kuna namna ulificha swali lililokuwa na mashaka..

"Hongera aa kwa vipindi" akamwambia Aretha ambaye hapa na pale macho yake yalihama kutoka chini na kumwelekea Ed.

"Aah Asante Rian..!" Akamjibu

Ed akanyamaza huku macho yake yakiendelea kumwangalia Aretha pasipo kuonesha jitihada za kutaka kuwasha gari ili kuondoka. Uvumilivu ukamshinda Ed,

"Retha. Yule kijana ni nani?"

"Aahem" Aretha akashtuka na kuinua uso wake kuangalia macho ya Ed

"Mmh" akainua jicho lake kuonesha alitaka kujua

"Charles?" Aretha akashangaa kuwa Ed alitaka kujua kuhusu Charlz aliyemuona akiongea nae dakika chache zilizopita au mwingine!

"Anaitwa Charles?" Akauliza Ed

Kama vile taa iliwaka kichwani kwa Aretha, akashtuka, akatabasamu akikumbuka mambo ambayo aliyasoma mtandaoni kuhusu vitu vinavyomfanya mwanaume aone wivu

"Rian" akamuita taratibu pasipo kuondoa tabasamu lake usoni na macho yake usoni kwa Ed.

"Mmmh" Ed akaitika macho yake akiangalia yale ya Aretha, kabla ya kusema chochote akahisi kumezwa na hisia za pendo zito zilizoelezeka kwenye macho yaliyomtazama. Hakujua ni kwa nini sasa alijiona mjinga kumuuliza Aretha kuhusu Charles.

"Am sorry princess" akaomba samahani kwa namna harufu ya pendo la Aretha liliufunika moyo wake

"I love you Rian...Yule ni rafiki pekee anayenielewa hapa chuoni.. usipate wivu" Aretha akaongea, tabasamu lake likionekana kwa upana zaidi..

Ed akacheka na kuelekeza mkono wake kuwasha gari, lakini akapokea mshangao mwingine uliompa kucheka zaidi. Aretha akachukua nafasi hiyo kumbusu shavuni kisha akaangalia nje

"Thank you Retha" akarudi nyuma kisha akaondoa gari eneo la chuo, moyo wake ulijaa na furaha. Alifurahia namna ambavyo Aretha aliiba fursa ndogo kama ile kumbusu. "Retha fanya hivyo mara zote"

"Eeeeh" Aretha akashangaa alichosikia amesikia vyema au la! Edrian yeye akishtuka kumbe aliwaza kwa sauti hata mdomo wake ukasema, akaamua kufunika alichosema,

"Nakupenda sana Retha"

"Rian.. asante"

Edrian akaendesha, akitabasamu kwa furaha kwa kuwa mawazo yake hayakusikika vizuri.

**

"Hello kiddo, Mchoraji kaondoka na gari Volvo XC60 muda huu sijui ni nani" Charles aliongea na Derrick kwenye simu

"Safi kiddo, ngoja nicheki na big bro" Derrick akajibu upande wa pili

"Unamaanisha yule ni Big Bro kiddo?" Akauliza Charlz kwa mshangao kuwa msichana kama Aretha amemfahamu vipi Ed.

"Kiddo nimesema nitamuuliza, sijasema ni yeye" Derrick akamjibu huku akicheka

"Unazingua kiddo aiyaa" Charlz akalalamika na kukata simu.

"Big bro na Aretha haaaa nawaza tu" Charlz akawaza na kucheka huku akiondoka eneo lile la maegesho ya magari.

"Derrick alimpa kazi ndogo rafiki yake ya kumwangalia Aretha kama kutakuwa na jambo lisilo la kawaida kwake. Wakati akitoka darasani kwake alimuona Aretha akitembea kwa haraka kuelekea kwenye maegesho ya magari. Akahisi anakimbia mtu, lakini alishangaa alipomjibu kuwa ana haraka, na akaishia kwenye gari. Akaamua kumjulisha Derrick ili kama yuko hatarini asaidiwe..