Lyn hakusema chochote akatoa bahasha nyeupe katika mkoba wake, ilifungwa vyema ikionesha haikuwa ukafunguliwa. Akanyoosha mkono kumkabidhi ile bahasha Ed lakini akasita akarudisha na kumuuliza,
"Babe, bado una msimamo ule ule wa kumpa Aretha nafasi yangu?"
Ed akamwangalia kwa hasira, "Muda wako unakaribia kuisha Lyn, nakusikiliza kisha niache nifanye kazi. Unajua masharti yangu linapokuja suala la kazi"
"Ooooh sijasahau babe, ninakumbuka sababu dunia inajua mimi ni mpenzi wako" Alipomaliza kusema akasukuma bahasha kwa Ed akaegama kwenye kiti..
Ed akamwangalia kumuuliza afanye nini na ile bahasha,
"Fungua babe" Lyn akamuonesha
Ed akachukua ile bahasha na kufungua, akatoa picha ambazo aliziangalia kwa utulivu. Kabla ya kuzimaliza akainua macho na kumwangalia Lyn akamuuliza, "Hizi nazo unazituma mtandaoni?"
"Hahahhaha hapana babe, hizi zitaenda kwa mtu anayetaka kukuiba mikononi, nataka ajue mimi na wewe tumekuwa na safari kwa muda mrefu!"
"Mmmmmm" Ed akaguna
"Ooooooh usikasirike babe, mimi na wewe tunapendana ila nadhani ulipomshika mkono siku ile kwenye show alikuroga"
Mikunjo ilionekana usoni kwa Ed, akamwangalia Lyn kiasi cha kumchoma kwa ukali wa macho yake.
"Babe, mbona unanikasirikia bure! Yeye ndie katuingilia, hizo picha ni ushahidi tu ya kuwa tuko zaidi ya atuonavyo"
Ed akarudisha macho kwenye picha zile, akaziangalia tena. Zilikuwa ni picha zilizoonesha sehemu tofauti walizokuwa pamoja. Lakini chache zilimuonesha akiwa amelala kitandani na Lyn wakiwa wamekumbatiana.
"Okay kama unataka sana..ah Retha azione hizi picha nitakusaidia umfikishie" Ed akasema wakati akizirudisha picha kwenye bahasha na kumrudishia Lyn.
Lyn akabaki akimshangaa kabla ya kucheka kicheko kizito na kuinuka kisha akainama kumuelekea Ed usoni, "Babe najua hautaki ila hatua yoyote ya kuendelea na huyu binti ni gharama ya maisha yako"
"Lyn, unanipotezea muda wangu..nina vitu muhimu vya kufanya kuliko hizi kelele zako. Naomba uondoke" Ed alipomaliza kusema akainuka na kuelekea mlangoni, akamfungulia mlango Lyn
"Hehhehe Ed babe we love each other. Wewe umekusudiwa kuwa wangu." Akachukua mkoba akaelekea aliposimama Ed..
"Umeacha bahasha yako Lyn" Ed akamwambia
"No babe, kaa nayo hiyo na mpatie kama ulivyosema. Nitathibitisha kama imemfikia"
Akamsogelea na kutaka kumbusu, Ed akamzuia kwa mkono wake ambao haukuwa umeshika mlango...
"Tsk. .tsk. .tsk babe I miss you" Lyn akamshika bega na kuondoka..
Ed akaachia mlango uliojifunga taratibu. Akashusha pumzi akarudi kuketi, na kuichukua ile bahasha. Akatafakari ikiwa Lyn atatuma kweli zile picha kwa Aretha inawezekana zikampa mashaka binti yule.
Akaangalia simu yake, muda ulikuwa bado kama dakika arobaini kwa Aretha kuwa ametoka darasani. Akaandika ujumbe mfupi wa simu,
"Retha darlin ukimaliza kipindi nitakuwa karibu na maeneo ya chuo. Usile chakula cha mchana. Tutakula wote. Love you princess."
Akachukua ile bahasha akaitumbukiza kwenye moja ya droo zilizokuwa kwenye meza yake. Akachukua chupa ya maji na kunywa, alipoishusha akacheka sana,
"Mapenzi kumbe huwa yanalazimishwa ha ha ha"
Tik. .tik
Ujumbe ukaingia kwenye simu yake. Akaangalia, "Okay Rian. I love you too" ulikuwa ni ujumbe kutoka Aretha.
Nuru ilionekana usoni kwa Ed baada ya kusoma ujumbe ule. Akaweka simu pembeni na kuinua simu ya mezani
"Allan tunaweza kuendelea na kilichobaki nina dakika chache nitakuwa natoka"
Akarudisha simu mezani huku akiwasubiri Allan na Loy aweze kumaliza alichoanza kueleza kwao. Moyoni alikusudia kuonana na Aretha kwa kuwa alikumbuka kuwa hakuwa amemwambia vile Lyn alimuwekea dawa kwenye kinywaji chake.
"Nahitaji kumwambia mapema, huyu mwanamke ni mgonjwa kweli aweza vuruga mambo zaidi ya ninavyoweza kufikiri" Akawaza Ed.
Mpango ukagongwa. Allan na Loy wakaingia na kuketi tayari kuendelea na mazungumzo waliyoanza na bosi Edrian Simunge.
"Samahani sana kwa muingiliano uliotokea, naamini hautajirudia tena..naomba tuendelee" Ed aliomba radhi kwa Allan na Loy kwa kuwa alijua kama kiongozi lazima akubali kuwa alifanya makosa kwa kuwa Lyn hakuwa mfanyakazi wa SM.