Siku iliendelea vyema kwa upande wa Ed, alifanya majukumu yake kwa furaha sana. Mambo ambayo kuna wakati yalimhitaji kumwagiza Loy, aliamua kuyafanya mwenyewe kwa kuinuka na kumuona mtu husika.
"Boss Allan, kuna nini leo maana sio sawa, au nafukuzwa kazi eeh?" Loy alimuuliza Allan baada ya kuona Ed kaenda mwenyewe ofisi ya Mhasibu mkuu na sio kumuita mhusika ofisini kwake
"Kwa nini uwaze hivyo Loy, umeleta umbea gani hadi ufukuzwe ahh?" Allan akamuuliza huku akiinua jicho lake moja
"Aaah. ..umbea gani tena, mimi nashangaa tu" akajitetea Loy
"Ndio, uache umbea utafukuzwa aisee" Allan akamsukuma kidogo begani Loy kwa kidole chake
"Uwhhh husaidii chochote Allan" Loy akalalamika
"Loyce" sauti ya Ed ambaye aliingia iliwashtua na Allan akainuka kwenye kochi alipokaa karibu na ofisi ya Lot
"Aahm yes..br. .boss" Loy akawa kama mtu aliyekurupushwa akainuka na kusimama
"Nakuomba ofisini sasa hivi" Ed alipomaliza kumwambia akamgeukia Allan na kumpa ishara ya kumtaka pia ofisini kisha akafungua mlango na kuingia
"Uwhhh Allan mbona hukuniambia mapema, nikifukuzwa kazi nitaanzia wapi mimi!" Loy aliendelea kulalamika huku akirudisha mlango wa ofisini kwa na kukutana na Allan ambaye alisimama cheko jepesi lilimtoka..
"Wwhh wewe nani kakuambia unafukuzwa kazi khaaa utakufa kwa umbea! Twende ukajue mbivu na mbichi" akaelekea mlangoni kwa Ed lakini kabla ya mkono wake kushika kitasa, Loy akaushika mkono wake
"Boss Allan nakuomba nitetee, nitajitahidi kufanya kazi zangu vizuri kabisa. Nahitaji hii kazi" Allan akamuangalia Loy alivyoukamata mkono wake,
"Hey Loy acha basi mambo yako ya umbea, hujui sababu ya kuitwa, sasa nini kinakupa mashaka haya ya kufukuzwa eeh" Allan akamwambia huku akitabasamu kumdhihaki
"Haya Boss, lakini uki__!" Allan akafungua mlango wa Ed na kufanya Loy asiendelee kuongea zaidi ya kugeuza muonekano wa sura yake, akapiga hatua za kinyonge kuingia ofisini kwa Ed..
Ed aliyekuwa akiangalia kompyuta yake akainua macho kuwaangalia Allan na Loy waliposimama mbele yake
"Karibuni mketi" akawakaribisha.
Baada yakuketi, Ed akaegama kwenye kiti chake na kusema
"Kuna mabadiliko kidogo nimefanya ambayo naona vyema niwashirikishe kabla ya kuwafikia wakuu wa idara"
Akawaangalia machoni na kuendelea baada ya kuona wamempa usikivu wa kutosha...
"Kuna baadhi ya mafaili ya kampuni mtaweza kuyafikia iwapo nitakuruhusu uuyafikie, nje ya hapo hataweza kufanya chochote mpaka upate kutambuliwa nami"
Uso wa Allan ulionesha kushangazwa lakini kwa upande wa Loy ni kama mwili wake ulikuwa pale ghaflai akili yake ilikuwa haipo
"Kama mlivyopokea taarifa za ujio wa mtu wa wizara, yupo hapa kukagua utendaji watu. Sio busara kumuacha aingie kila kona ya nyumba yetu. Kuna mambo atataka kutoka kwetu mmpatie lakini yale yakiyofungwa ni yetu kujua na sio yeye."
"Allan akashusha pumzi, "Okay brother nimeelewa, tutakapofungua tutaombwa kutumia neno siri ambalo tutalipata kwako?"
"Ndio Allan na itakuwa inabadilika kila baada ya kut___!" Sauti ya mlango ukigongwa ilimkatisha Ed na wote macho yao yakaelekea mlangoni
"Loy hebu angali_!" Mlango ukafunguliwa na aliyeingia alifanya uso wa Ed kubadilika katika sekunde chache
"Oooh mpenzi kumbe mnaendelea na kikao?" Lyn akauliza huku akipiga hatua na kusimama karibu na jokofu..
Ed ambaye alimwangalia Lyn hakujua nini amjibu, Allan na Loy waligeuka kumwangalia
"Joselyn we are in the middle of a meeting and___"
"Am sorry babe lakini najua hawatajali kuniazima dakika chache tuweze kuongea, sio ndio hivyo Allan eeeh?" Lyn akamkatisha Edrian huku akimpa tabasamu la tafadhali nikubalie Allan ambaye alimshangaa
"Oooh Loy how are you? Hautajali dakika chache mnaendelea eeh.." Joselyn akamsalimia Loy huku akimuangalia machoni kuwa akubaliane na alichosema
Kabla ya Ed kusema chochote, Allan na Loy wakasimama
"Sorry brother, tutarejea mkimaliza usijali" Allan akamwambia Ed huku akimpa ishara ya kuwa wako sawa.
"Nashukuru sana Allan kunielewa" Lyn akashukuru na kusogea kwenye moja ya kiti akaketi huku akiweka mkoba wake juu ya meza.
Ed akamtazama Lyn kumuashiria aseme kilichomleta