Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 95 - JAMBO LAKE

Chapter 95 - JAMBO LAKE

Nje kidogo ya A-Town, mwanaume mmoja alisimama kwenye chumba ambacho muonekano wake ulikuwa ni ofisi yenye hadhi yake. Makochi ya ngozi yalikaa upande wa kulia wa meza kubwa ya kiofisi iliyobeba kompyuta na kompyuta mpakato, pembeni kukiwa na mafaili yaliyobebwa kwenye trei. Alisimama kwenye mlango wa kioo ambao ulimpa nafasi ya kutazama nje bila shaka.

Mwanga hafifu wa chumba hiki ulimficha sura yake japokuwa kwa umbile lake ungeweza kutambua ni mwanaume mkakamavu ambaye hata sauti yake ilibeba mrindimo wa mamlaka uliomzunguka.

"Bon, kunileta mahali hapa mida hii hakikisha taarifa unayonipatia inastahili usikivu wangu." Aliongea mwanaume huyo.

"TM samahani kwa muda huu, lakini ni muhimu ukienda kulala ukafahamu kuwa, tumemfuatilia Simunge lakini nimemuona binti wa Emilia akiwa na Simunge"

Akageuka, kwa muonekano usoni kwake ungeweza kujithibitishia kuwa taarifa ile ilimshtua lakini hakusema chochote, Bon akaendelea..

"Wameonekana PVB mchana, jioni alimrudisha nyumbani. Nisamehe kwa kuwa ilibidi nikae kusubiri nje ya geti la Emilia kama kuna namna yoyote ningemuona yule binti tena na__"

"Bon hii ni mara ya mwisho nakukumbusha Emilia asione sura yako, la sivyo sio wewe wala mimi tutakuwa salama"

"Samahani TM" kwa unyenyekevu mkubwa Bon aliomba msamaha

"Sawa, ifanyie kazi taarifa hiyo kujua kwa kiasi gani Simunge anamfahamu Emilia na binti yake na aina gani ya uhusiano uliopo kati yao"

"Sawa, Bosi" akaitika Bon na kuendelea kusimama akimwangalia TM

"Usisahau kumfuatilia Renee, she is so smart, hakikisha unapata taarifa mara kwa mara ya utelekelezaji wa Prop 1..Usiku mwema Bon" alitoa maelezo na kwa maneno hayo alimruhusu Bon kuondoka..

"Sawa TM" Bon akainama na kisha akatoka nje.

***********************

Jumatatu Edrian aliingia kazini mapema kama ilivyo kawaida yake. Uso wake ulibeba tabasamu pana, wakati akiendelea kupitia barua pepe zilizokuwa kwenye akaunti yake.

Loy akaingia na kahawa mkononi, lakini alikutana na kikombe kingine cha kahawa kikiwa tayari mezani..

"Pole Loy nimejihudumia" Ed aliinua kichwa na kumwangalia

"Oooh basi sikujua boss"

"Basi kiache hapa kitapata mtu muda si mrefu" Ed akamwambia Loy.

Kabla hajaendelea na kumsomea ratiba yake leo, "Loy kama kuna ratiba kati ya saa saba hadi saa kumi naomba uzivunje, sitakuwepo ofisini" Ed akarudisha macho kwenye kompyuta mpakato iliyokuwa mbele yake!

"Sawa boss"

Akaendelea na kumsomea ratiba ya asubuhi ile, kabla ya kumaliza mlango uligongwa,

Ed akainua uso na kumwangalia Loy kama ishara ya kumwangalia mtu aliyegonga mlangoni. Loy akaelekea mlangoni na kufungua...

"Hello...Loyce" Renatha akamsalimia akiwa amesimama nje ya mlango..

"Karibu" Loy akamwangalia Renatha kama mtu ashangaaye kitu asichokijua, hakupiga hatua kumpisha.

Renatha akatabasamu na kumwambia Loy, "Naweza kumuona Boss kabla sijaenda kwa HR?"

"Nadhani ungemuona HR kwanza halafu ikawa___?

"Loy?" Edrian akamkatisha Loyce ambaye aligeuka na kumwangali machoni boss wake

"Mruhusu aingie" Ed akamjibu Loy huku macho yake yakiwa kwenye kioo cha kompyuta yake.

Loy akamkaribisha Renatha kisha akarudisha mlango na yeye akatoka.

Ed hakuinua macho yake bali akaendelea kuzungusha kipanya cha kompyuta kilichokuwa mkononi mwake

"Habari ya asubuhi Mr Simunge" Renatha akamsalimia akiwa mita chache kufikia meza alipoketi Ed

"Salama..ungemsikiliza Loy kwa kuwa hakuna sababu ya wewe kuniona mimi kabla ya HR"akainua macho na kumwangalia

Renatha akajiweka vizuri akijaribu kutoonesha kuumizwa na maneno yaliyosemwa na Ed

"Sorry boss, niliona ni vizuri nikushukuru moja kwa moja baada ya kupokea mwito wa kuanza kazi"

"Oooh sawa. Unaweza sasa kuonana na HR ndie anayejua majukumu yako na namna utaingiliana na kila idara. Karibu SM Renatha." Ed akamkaribisha

"Asante sana" Renatha akabaki amesimama akimwangalia Ed kama mtu aliyetaka kusema kitu.

Ed akarudisha macho kwenye kompyuta, Renatha akageuka na kuelekea mlangoni na akatoka huku akiwa na tabasamu la ajabu ajabu usoni mwake. Loy akamwangalia kwa mshangao kwa namna alivyotabasamu

"Huyu naye amekuja na lake jambo"