Gari ya Edrian ilisimama kwenye geti la kuingia nyumbani kwao Aretha ikiwa tayari ni saa moja na nusu usiku. Kwa namna walivyoonekana hawakutamani kuachana kwa wakati huo..
Ed akajikaza na kumwambia Aretha washuke
"Aaah" Aretha aliitika
"Retha twende nisimpe mama wasi wasi" akazima gari na kufungua mlango,
"Rian" Aretha akamuita Ed ambaye aligeuka kushuka lakini akarudi mkono ukiwa umeshika kitasa cha mlango wa gari
"Aaahm" akaitika Ed huku akimuangalia Aretha katika mwanga hafifu uliopenya kwenye gari ukitokea kwenye moja ya taa iliyokuwa pale nje.
"Aaahmm..amm.."Aretha akichezea vidole vyake alipatwa kigugumizi, uso wake ulitazama chini
"Retha unataka kuniambia nini?" Ed akatoa mkono kwenye mlango akamshika Aretha mkono kitendo kilichomfanya amwangilie usoni.
Kitu kilichofuatia kikamshangaza Ed, Aretha akamsogelea kwa haraka na kumkumbatia..
"I love you Rian.."
"I love you so much Retha." Edrian akamjibu na kumkumbatia
Akatabasamu kwa furaha, maana muda wote huo ni yeye ndie alikuwa wa kwanza kwa kila hatua, sasa Aretha amemkumbatia mwenyewe.
"Retha, kesho tutaonana sawa eeh" akamwambia kwa sauti ya chini karibu na sikio lake. Aretha akamuacha na hakumwangalia Ed akashuka kwenye gari na kusimama getini huku akigonga taratibu.
Ed akafuatia nyuma yake, wakasimama wakisubiri geti lifunguliwe. Frans mdogo wake Aretha akafungua na kuwakaribisha ndani. Aretha hakugeuka kabisa nyuma akaingia ndani.
"Frans, asante kutufungulia" Ed akasema akiwa na tabasamu usoni
"Ooh hamna shida karibu bro"
Mama yake Aretha alikaa kwenye veranda ya mbele ya nyumba akamuona binti yake na namna alivyorudi akatabasamu zaidi.
"Mama shikamoo" Aretha akasalimia na kupitiliza hadi ndani uso wake ukionesha tabasamu na soni kwa wakati mmoja.
"Eeeh we Retha unakimbikimbia tu kusalimia gani huko" mama yake akalalamika
"Mamaa aaah"" sauti ya Aretha ikasikika kutokea ndani.
"Mama tumerudi salama, unaendeleaje?" Ed akamsalimia mama akiwa amesimama karibu na ngazi za kuingia pale alipoketi.
"Sawa, mwanangu hongereni naona mwenzio kachoka hataki hata kusalimia" mama akamjibu
"Hahahaha hapana mama" Ed akacheka kidogo
"Karibu ndani mwanangu" mama akinuka kumkaribisha Ed,
"Haaam hapana mama, asante sana naomba nirudi sasa. Wakati mwingine nitakuja tuongee"
"Aaaah basi sawa mwanangu" mama akamkubalia Ed ambaye alirudi kwenye gari ili kuondoka. Akamshukuru sana Frans ambaye alitoka ili kufunga geti.
Edrian akaingia kwenye gari na kuwasha kuanza safari kurudi nyumbani kwake.
"Thank you Retha, ni kama ninaanza kuishi"
Ed akajisemea.
Siku hii ilikuwa na furaha kuu mno kwa Ed, akatamani isiishe lakini asingeweza kukaa na Aretha muda wote.
Wakati akielekea barabara kuu alihisi kuona gari kama ile iliyokuwa ikimfuatilia siku chache nyuma lakini hakutaka kuiharibu siku yake ambayo ilimuacha akiogelea katika furaha ya kipekee. Aliona ni upendeleo wa ajabu kwamba yeye na Aretha wamekubaliana kwa wepesi.
Tabasamu la Ed lilikatishwa na simu iliyoita, na alipoiangalia sura yake ikawa kikazi zaidi.
Akapokea
"Hellow Captain" akaongea
"Umetoka hapo nyumbani kwao Aretha kuna gari imesimama lakini hakuna anayeshuka. Nina mashaka nayo, unaweza kurudi bro" Captain aliongea
Edrian hakusubiri maelezo zaidi akageuza gari wakati huo huo na kuanza kuingia barabara iliymrudisha kwao Aretha.
Akapiga simu yake ambayo ilipokelewa na Aretha, "Rian I am so___? Kabla ya kumaliza Ed akamkatisha
"Retha mwambie Frans asifungue geti endapo kama kuna mtu atagonga getini" Ed alitoa maelekezo kwa sauti ya kawaida ili kutomfanya Aretha ashtuke..
"Rian kuna tatiz__"
"Retha, tafadhali fanya hivyo nitakwambia kwa nini baadae" Ed akamsihi Aretha
"Sawa Rian" Aretha akakata simu kitu kilichompa uhakika Ed kuwa atakuwa ameelekea kutekeleza kile alichomuagiza.
Ed alikuwa katika mwendo ambao magari mengine barabarani ilibidi yampishe. Kwa kuwa ilikuwa jumapili, foleni haikuwa kubwa hivyo ndani ya dakika chache alikata kuingia barabara iliyoingia 'moon street'. Simu yake ikaita alikuwa Captain akaamuru ipokelewe
"Bro imeondoka sasa hivi, inakuja muelekeo wako"