Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 94 - UNGENIKUMBATIA

Chapter 94 - UNGENIKUMBATIA

Ed alikuwa katika mwendo ambao magari mengine barabarani ilibidi yampishe. Kwa kuwa ilikuwa jumapili, foleni haikuwa kubwa hivyo ndani ya dakika chache alikata kuingia barabara iliyoingia 'moon street'. Simu yake ikaita alikuwa Captain akaamuru ipokelewe

"Bro imeondoka sasa hivi na inakuja muelekeo wako"

Ed alipoangalia mbele aliona gari ikiwa katika mwendo mkali na ikampita kwa haraka. Akaangalia mahali pa kugeuzia lakini hakupaona akajua asingeweza kuiwahi ile gari. Akaendesha kurudi barabara kuu taratibu huku akimpigia simu Captain..

"Sikufanikiwa kumuona aliyekuwa akiendesha lakini aina ya gari na namba ninazo. Nikifika nitakutumia. Chochote walichofanya nje hapo"

"Hakuna, hawakushuka kabisa. Lakini namna walivyoondoka ni kama mtu aliwaambia waondoke...worry not tutaanzia kwenye namba" Captain alimpa maelezo Ed

"Okay, Captain" Akakata simu

"Call Aretha" Edrian akaiamuru simu yake ambayo ilikuwa na aplikesheni iliyomwezesha kupiga simu pasipo kuigusa.

Simu ikaita katika "Bluetooth phones" kwa muda, sauti ya Aretha iliposikika Ed akatabasamu

"He..hello Rian" sauti ilisikika kama ya mtu ambaye alikimbia kuiwahi simu

"Ulikuwa mbali?" Edrian akauliza akitabasamu

"Aaah haa nilikuwa naoga..aah sorry nilikuwa nje" Aretha akajishtukia na kujaribu kurekebisha alichosema. .

Edrian anacheka taratibu kwa namna ambavyo Aretha alipatwa na kigugumizi

"Ulikuwa unaoga ah?" Akarudia kile alichosema

"No Rian..nilikuwa nje"

"Okay princess...ulikuwa nje" hakutaka kuendelea kumpa wakati mgumu

"Rian..mbona ulinishtua muda ule?" Aretha akauliza

"Retha, usihofu ni kama aaa. . Nilipatwa na wasiwasi kuhusu usalama wenu. Niliona gari iliyonipa wasi wasi. Lakini usiogope mko salama" Ed akajitahidi kuongea pasipo mashaka ili kutosikika na hofu. Hakutaka kumfanya Aretha kuishi kwa mashaka.

"Gari ipi Rian?" Aretha akazidi kutaka kujua

"Nilipishana nayo maeneo yenu lakini Retha usihofu nimeongea na polisi wamesema watafuatilia" Ed ikambidi amdanganye ili kuepuka kuulizwa zaidi.

"Oooh. Na wewe bado unaendesha gari?"

Ed akajua Aretha atakuwa amesikia sauti as barabarani kwa kuwa alifungua kioo kidogo..

"Sijafika, ila nitafika muda si mrefu" Ed akajibu

"Rian"

"Ahmm" akaitika

"Nisamehe sikukuaga"

"Ha ha sawa Retha....uliogopa ungenikumbat__"

"Rian usiku mwema" Aretha akamkatisha. Kabla Ed hajasema chochote simu ilikatwa. Akatabasamu, "Retha my princess"

*************************

"Lyn kuna nini unafanya mbona umekataa kula?" Martinez akiwa ameketi kwenye kochi chumbani kwa binti yake alimuuliza

"Baba, Ed ameingia PVB na yule binti, ananipuuzia na hataki kuongea nami, ananichukuliaje eeeh?." Lyn akamlalamikia baba yake ambaye alimwangalia akitafakari

"Anadhani mimi kuacha maisha yangu SA kumfuatilia yeye ni bure"

"Hey sweet, usijilaumu hata kidogo, bado una karata mkononi, bado tunaweza kumuweka tunapotaka." Martinez akamfariji binti yake

"Karata ipi baba, huyo binti na mimi ni ulimwengu mbili tofauti lakini bado kampa nafasi yangu mtu asiye na hadhi sawa nami. Ed is so arrogant daddy" Lyn aliyekuwa ameegama kwenye ubao wa kitanda akasema kwa hasira

"Nisikilize binti yangu, Ed anaweza kuwa amekufedhehesha kwa kile alichofanya lakini wewe utatumia hicho hicho kumfedhehesha yeye. Au unaonaje?"

"Baba, nataka huyo binti amkimbie Ed mwenyewe sitaki karata ya kumbembeleza mtu ambaye namfahamu muda wote huo. Nina njia zangu zitamtoa bila hata kumgusa kwa kidole changu" tabasamu ovu likatoka kinywani kwa Lyn ambalo likamfanya baba yake amwangilie kutaka kujua

"Usijeharibu mambo zaidi Joselyn" akampa onyo binti yake

"Unaniamini?" Lyn akauliza

"He he he nitaachaje kumuamini binti yangu" Martinez akaachia tabasamu

"Kaa utulie baba...mwangalie Joselyn wako akimleta Ed kwako?"

"Tukiipata ile ramani alininyima baba yake, tutakuwa tumemaliza mchezo binti yangu.. Almasi itakuwa yetu" Martinez akamuonesha binti yake yuko pamoja nae kwa kila hatua.

"Asante baba, tukipata hiyo ramani maisha yatakuwa murua.." Lyn akatabasamu

"Be ready Aretha, I am coming for you girl"

Baba yake akainuka na kuondoka chumbani