Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 89 - PLEASE LOVE ME

Chapter 89 - PLEASE LOVE ME

Edrian akiwa na umri wa miaka 28 alipata pigo zito la kuondokewa na baba yake. Aliegesha gari sehemu hii ambayo haikuwa na watu kabisa, akasogea mbele akainama na kushika magoti, moyo wake ukiwa mzito baada ya kutoka hospitali mchana huo huku taarifa za kifo cha baba yake sasa zilikuwa wazi kwenye vyombo cha habari. Simu yake iliita kwa muda na hakuhitaji kusikia watu wakimpatia pole, japokuwa ndugu zake pia walimtafuta, hawakujua mahali alipoenda. Ed alipokuja hapa aliamua kuiacha simu ndani gari.

Akapiga kifua chake, akapaza sauti na kulia "Babaaaa....why now!" Akauliza katikati ya kilio chake.

Akapiga magoti kuna kuinama, mikono yale ikagonga chini kwa nguvu hata kusababisha mchubuko kwenye ngozi ya juu ya kiganja chake. Akalia kwa uchungu hakuweza hakuweza kusikia hatua za binti ambaye alisogea kwa kunyata taratibu mpaka alipokuwapo. Akaweka chupa iliyokuwa na maji nusu pembeni yake na kitambaa. Akarudi kwa kunyata mpaka alipokuwa mbali na Ed akaendelea kumwangalia akitamani amfariji lakini aliogopa...

"Baba, nani atasimama kwa ajili ya familia hii, wakati huu ambao ninakuhitaji sana aaaah baba" akapiga tena mikono chini. Kwa sababu eneo hili halikuwa karibu na maji ya ziwa, mchanga wake ulikuwa mgumu, mikono yake iliumia na damu ikaanza kutoka kwenye mikono yake.

Alipoinua uso macho yake yakaona maumivu aliyojisababishia, akaamua kurudi kwenye gari ili kuangalia sanduku la huduma ya kwanza. Alipoinuka akaona pembeni maji na kitambaa, akashtuka na kuangalia kushoto na kulia lakini hakuona mtu yeyote. Akifikiri na kuamua kuhitimisha huenda Mungu alimtumia malaika ili amfariji.

Akachukua yale maji akanawa mikono yake vyema, akainua macho kuangalia juu kisha akasema "Baba huko uliko unajua sababu kwa nini umeniacha, inawezekana sababu yako ni nzuri kuliko malalamiko yangu. Sasa natambua kuwa hata kama hauko pamoja nami najua ninayo sababu ya kuendelea kuishi, nitaishi hata kama itanibidi kuteseka lakini kile umeweka ndani yangu ni mbegu ambayo nitaitunza isiharibike.. Daima Simunge ataishi ndani yangu"

Alipomaliza kusema maneno haya akaiangalia ile chupa na kile kitambaa, taratibu akageuka na kurudi garini huku akiangaza kuona kama kuna mtu alikuwa karibu na pale!.

*******************

"Nilipoyasikia maneno hayo Rian, nilipenda uthabiti wako. Sikujua kama ulikuwa umefiwa nilihisi nawe ulikuwa katika hali kama yangu. Nikaamua kutoendelea kumtafuta baba, nikasema nitaishi na kutimiza kusudi langu kama Aretha." Aretha akajitoa mikononi kwa Ed akachukua chupa ya maji akanywa.

Alipotaka kusogea pembeni aendelee kumsimulia Ed, mikono ya Ed ikamvuta na kumrudisha kifuani. Aretha akafumba macho kwa aibu

"Ulitaka kufanya nini Retha?" Ed akamuuliza uso wa ukiwa umeinamishwa kumuangalia Aretha..

"Haamh" akashtuka Aretha

"Umesema nilikuzuia kufanya maamuzi mabaya kwa maneno yangu. Maamuzi gani ulikuwa nayo wakati huo Retha?"

"Rian..ai. aaa...nilipotoka PVB nilikusudia kutafuta sumu yoyote ninywe nitakapofika nyumbani. Nilikasirika sana. Lakini nilipokuona na kukusikia, nikaamua kuishi na nikabadilika hadi huyu Aretha unayeniona". Alimaliza Aretha huku akichezea kifuniko cha chupa

Ed akatabasamu na kuuliza, "Ulinifahamu uliponiona hapa?"

"Haaa nilimuona sura yako uliporudi kwenye gari. Sikufahamu chochote kuhusu wewe zaidi ya vile nilivyokusikia ukisema "Simunge ataishi ndani yako". Niliporudi nyumbani nilikutana na taarifa ya kifo cha aaah baba yako" Aretha akaongea taratibu na akajaribu kumuangalia Ed ili amuoneshe hakupenda kuongelea hilo, lakini Ed akamkumbatia kumzuia asimwangalie..

"Am sorry..Rian" akaomba radhi

"It's okay" Ed akamjibu akiendelea kuzilaza nywele za Aretha

"Niliposikia ni Simunge nikawa nimeelewa sababu ya huzuni. Bado nikakuona ukiwa unajibu maswali ya waandishi wa habari.. ndipo nikakufahamu."

Ed ambaye muda wote huu alijizuia kuonesha furaha yake, akamuinua Aretha ili amwangile vyema usoni. Hakuweza kujizuia akamshika kidevu akikikiinua kwa vidole vyake...

"Retha, I love you more. Please love me" alipomaliza kusema maneno haya aliinama na kubusu midomo ya Aretha taratibu