Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 84 - UNAWAZA NINI

Chapter 84 - UNAWAZA NINI

Eeeh 'sorry' hiyo ni ya nani binti yangu" sauti ilimkatisha kwenye mawazo yake na kumfanya ainuke kwa ghafla

"Mama aaaah.." Aretha akalalamika baada ya kusikia sauti ya mama yake

"Aiyaaa nijibu basi nimesikia unaomba samahani, na hapa sioni mtu zaidi ha hiyo picha....aaaaah ni ya___" kabla ya mama kusogea ilipo picha Aretha akavuta kitambaa na kuifunika huku akisimama mbele yake

"Mama jamani nilikwambia huku ni kwangu peke yangu" Aretha akaendelea kumlalamikia mama yake ambaye uso wake ulibeba tabasamu la kumtania binti yake..

"Unaomba sorry picha ya Simunge eeeeh" akamtania Aretha ambaye macho yake yalijawa na aibu akijaribu kuyakwepa yale ya mama yake..

"Aaah mama niache nataka kuchora"

"Unataka kuchora au kuomba msamaha, umekosea nini binti yangu?" uchokozi wa mama sasa ulikuwa wazi..

Aretha akarudi kukaa pasipo kumjibu mama yake na sura yake ikawa na huzuni ghafla. Mama yake akamsogelea na kumkumbatia kwa nyuma

"Binti yangu, huwa tunaomba msamaha kwa mtu na sio picha yake. Kuomba picha msamaha ni kiburi kuwa huwezi kumwambia uliyemkosea ukweli. Usimwambie ulichokosea ila kabiliana nacho katika uhalisia" mama aliongea kwa sauti ya upole na kabla Aretha hajamwambia akamuachia na kusogea kando.

"Mama hmmm" Aretha akajaribu kuongea lakini akakatishwa na mkono wa mama yake.

"Retha, ongea na mtu sio picha yake" alipomaliza kusema akaondoka ndani akimuacha Aretha ameinama akiangalia kioo cha simu yake..

"Mmmmhhh" akashusha pumzi na kumpigia Ed.

***********************

Ed alipowasili nyumbani, akamkuta Li amekaa sebuleni akiangalia mpira akiwa tayari amevaa pajama zake.

"Bro" akamuita mara baada ya kumuona alipoingia ndani!

"Li", Ed akaelekea kuketi kochi lililokaa pembeni ya ukumbi huu. Akafungua vifungo vya mwanzo wa shati.

"Uchovu eeh" Li akamuuliza kaka yake!

"Yeeah, leo imekuwa ya kuchosha sana. Ila niko okay" wakati anamalizia kusema kuna tabasamu fulani lilipita haraka mdomoni kwa Ed ambalo Li aliliona. .

"So how are you going to handle the news" Li akamuuliza kaka yake huku akitafakari lile tabasamu aliloliona...

"Sitafanya chochote. Let them say whatever they want to believe" Ed alijibu na kushusha pumzi

"Okay bro" Li akakubaliana na kaka yake..

"About Aretha___"

"Worry not, nitalimaliza kesho. Asante sana Li" kulikuwa na chumba ya farijiko katika maneno ya Ed yalipofika masikioni kwa Li. Akahisi kuna kitu kitakuwa kimetokea kwa kaka yake lakini asingeweza muuliza sana maana alimfahamu asivyopenda kuzungumzia mambo hayo.

"Sawa brother" Li akarudisha macho yake kwenye runinga kutazama mechi iliyoendelea..

Ed, akainuka na kuelekea juu, akageuka tena na kumwambia Li, "Asante sana"

Li akamwangalia kaka yake ambaye alishageuka kuendelea kupanda ngazi.

"Sijui nini kasikia" Li akawaza

Hakuelewa ghafla kutoka kwenye hasira aliyoiona walipokutana na kubadilishana magari, hadi hili tabasamu analoliona nini kilikuwa kimetokea.

Akawaza huenda kuna habari njema ameipata alipoenda kwa Captain. Akashusha pumzi na kuamua kuingia katika furaha ya kaka yake.

Wakati Edrian alipoingia chumbani mlio wa meseji uliingia kwenye simu yake..

"Rian. .umelala?"

Tabasamu la Ed sasa lilikuwa zaidi ya lile alilokuwa nalo wakati akiingia

"Hapana Retha. Ndio nimefika nyumbani. Mbona hujalala?" Akaandika na kutuma,

Akavua nguo akijiandaa kuoga lakini akakaa kwenye kochi..

Aliposikia ujumbe umeingia kwenye simu yake akaangalia "Sina usingizi" Retha aliandika.

Ed akacheka taratibu na kuandika "Kwa nini?"

Akasubiri.

"Sijui" akajibu Aretha

"Unawaza nini?" akaandika Ed, meseji ikajibiwa haraka

"Nothing Rian"

"Okay, basi lala sasa" akaandika Ed

Kabla ya kusubiri jibu akaongeza "Kesho ni siku ndefu. Unahitaji kupumzika"

Akainuka na kuelekea bafuni huku akihisi joto likiongezeka kwenye mwili wake.

"I need cold water right now" akasema alipofunga mlango wa bafuni. Mlango ulipofungwa ujumbe ukaingia kwenye simu. Ukafuatiwa na mwingine wa pili.

Bafuni Ed aliruhusu maji ya kutosha yatiririke kwenye mwili wake. Maji yalikuwa na ubaridi ambao ulimfanya Ed kutamani kukaa kwenye "shower".