Chapter 83 - MSAMAHA

Edrian akiwa ofisini kwa Captain, "The base" alikaa kwenye kiti cha kiofisi kilichokuwa nyuma ya meza ambayo pia ilibeba kompyuta mbili. Mikono ya Captain iliendelea kubofya kompyuta huku maongezi yakiendelea kati yao.

"Najaribu kujua nani anabeba hisa kubwa za Kussah Investment, siamini Martinez anaweza kubeba 60% yote kama inavyoonesha. Kwa hiyo rekodi hapo, inaonesha kumekuwa na hamisho la hisa ambazo mwenyewe bado hajulikani." Captain akimuelezea Ed

"Nitamuondolea umiliki huo. Nitaiona njia naamini" Ed akamwambia huku mikono yake ikiwa kwenye kompyuta moja kati ya mbili zilizokuwepo

"Kwa hili ambalo liko mtandaoni, usijibu chochote. Ukishajibu wataibua maswali mengine zaidi. Tutapata kitu cha kuivuta hadhira na itasahau." Akashauri Captain

"Hhmmm"

Mazungumzo yao yalikatishwa na muito wa simu ya Ed, alipoangalia alikuwa ni Linus

"Niambie Li" Ed akaitikia

"Nimemfikisha Aretha. Nakuja huko!" Li akamjulisha

"Asante sana Li, tukutane tu nyumbani hapa namaliza sasa hivi."

"Okay Bro." Li akamkubalia kaka yake na kukata simu.

Ed akamalizia kuangalia faili chache kisha akaamua kumuaga Captain kwa kuwa mara nyingi yeye hulala hapo Base kwenye chumba cha ziada ambacho kiliandaliwa iwapo kazi zikiwatinga.

"Sawa Bro, worry not we will find a way." Captain akamfariji Ed,

"Barak na Edwin wakirudi nadhani wataifanya kazi kwa urahisi"

Barak, Edwin, Ismail na Captain waliunda timu ya 4D..

Edrian akatikisa kichwa, "see you Captain"

Akaelekea kwenye gari, lakini kabla ya kuingia simu yake ikaita. Akaamua kuingia kwanza ndio apokee. Baada ya kufanya hivyo, macho ya Ed yalipoona nani alikuwa akimpigia simu muda ule, mikono yake ikawahi kuteleza kupokea akihisi inaweza kukata

"Retha" Ed akaita

Upande wa pili Retha alikuwa kimya kwa sekunde, sauti ya pumzi yake akihema ilisikika vyema masikioni kwa Ed ambaye aliegama kwenye kiti

"Rian. . Am sorry" Aretha akajibu kwa sauti ya utulivu

"Aaahm" Ed akashtuka, Aretha anaomba msamaha wa nini wakati yeye ndie alitakiwa kufanya hivyo.. kimya kingine kikafuata

"Retha...are you___?" Kabla ya kumaliza Aretha akamkatisha

"Nilizima simu sababu nilihisi umenidanganya. .n..na.na aa..sikutaka kukusikiliza kwanza" Aretha sasa sauti yake ilibeba majuto kiasi kumfanya Ed kuhisi kama alikuwa akilia

"Retha..don't feel bad, mimi sikujua kama aaaam.. angekuwepo. Sikufanya hivyo kusudi. Na kuhusu yanayoendelea Insta na__?"

"R..Rian, aaamh ...tutaonana kesho?" Aretha akamkatisha Ed

"Kama hauna shida na hilo Retha, I will love to" Kuna raha ya ghafla iliujaza moyo wa Ed baada ya kusikia Aretha mwenyewe akiomba wakutane.

"Sawa, naaa..amh....tunaweza kuonana mapema Rian?" Aretha akauliza

"Yes Retha. Niambie tu muda gani nije nikuchukue"

"Aaaamhhh saa sita mchana, Itafaa?" Aretha akapendekeza

"Sawa" Edrian akamjibu uso wake ukiachia tabasamu murua

"Asante kwa usafiri"

"Ooooh...sawa Retha" Ed akamsikia Aretha akishusha pumzi kama mtu aliyeshusha mzigo

"Retha" akaita

"Goodnight Rian" kabla Ed hajaitikia simu ikakatwa.

"Eewhhhh" Ed akashusha pumzi, hakuamini imekuwa rahisi sana kwa kitu ambacho alihisi kingemchukua muda kukiweka sawa. Akatafakari ushauri wa Brian, akashukuru kuwa umefanya kazi.

"Retha how I wish hiyo kesho ije haraka" Ed akajisemea moyoni mwake. Akitafakari siku ilivyokuwa ndefu na nzito lakini simu hii kutoka kwa Retha ilifukia mashimo mengi ya uchovu kwake.

"Kesho ni nafasi pekee ambayo nitaitumia kusema kile nakitaka." Akawaza wakati huo akaondoa gari kuelekea nyumbani huku taratibu akiburudishwa na "Perfect" wa Ed Sheeran.

"Ilikuwaje Aretha amebadilika.."

*******************

Baada ya Li kumshusha Aretha getini kwao, akamsubiri mpaka alipoingia ndani akaondoa gari. Aretha alipitiliza hadi chumba chake cha kuchora, akakaa kwenye moja ya picha iliyokuwa kwenye ubao wa kutundikia.

Akavuta kitambaa kilichofunika ile picha. Akaiangalia "oooh Rian" mikono yake ikakumbatia simu yake kifuani.

"Am sorry" akasema taratibu

"Eeeh 'sorry' hiyo ni ya nani binti yangu" sauti ilimkatisha kwenye mawazo yake na kumfanya ainuke kwa ghafla

"Mama aaaah.."