Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 70 - SHE IS WICKED

Chapter 70 - SHE IS WICKED

Walifika nyumbani majira ya saa saba na nusu usiku. Kwa uchovu aliokuwa nao Ed hakumsubiri Li aliyekuwa akimaliza kuegesha gari vyema.

"Usiku mwema Li" akaelekea ndani. Alipofika chumbani kwake hakuchelewa kuelekea bafuni na kujiweka sawa kulala. Wakati akijitupa kitandani simu yake iliita, na kwa sababu alipofika aliiacha mezani ikabidi ainuke kuichukua

"Aaaaargh!" Alilalama Ed na kuinuka. Alipoangalia ni nani aliyekuwa akimpigia simu mida ile macho yake yaliwaka kwa mng'ao wa ajabu na ghafla akapata wasi wasi. Akapokea kwa haraka...

"Retha uko salama?" Swali la kwanza aliuliza baada ya kupokea simu

"Mh. ..aaah niko salama" upande wa pili Aretha aliitikia.

Ed akashusha pumzi kwa nguvu kiasi kwamba Aretha akashtuka

"Rian" akaita kwa sauti ya chini

"Sorry, nilishtuka kuona simu yako, nikahisi kuna shida..Mbona hujalala" akauliza Ed wakati huo akilala kitandani..

"Ijumaa natumia muda mwingi kuchora. Nilikuwa nakamilisha picha moja" Aretha akajieleza

"Ya kwangu Retha?" Edrian aliuliza huku tabasamu likiwa dhahiri kwenye midomo yake... akakumbuka kwenye Show alipokutana na Aretha, jinsi alivyokuwa akiyakwepa macho yake...

Kimya kilipita hadi akaita "Retha"

"Mmmh" Aretha akaguna

"Asante" Ed akasema huku akiendelea kutabasamu. Kichwani akili yake mwenyewe ilimshangaa "unatabasamu haumuoni...Ed you are crazy"

"Eeeeh?" Aretha akashangaa

Ed akaamua kumchokoza Aretha.."mbona umenipigia muda huu Retha..ulijuaje nitakuwa macho?"

"Oooh ...aaah sorry..aaah Rian. .I.." kigugumizi cha maelezo kilimshika Aretha

"Retha, usijali. Nilihitaji sana call yako sikujua kwamba unaweza kuwa hujalala..asante"

"Mmhh. ..aaah Rian nina...sorry nilitaka aah kukwambia naomba kesho nisiende kwa mama. Naomba uongee na Derrick asije, mimi hatanielewa."

Edrian tabasamu lake likazidi zaidi " kwa nini hutaki kwenda Retha?....unamuogopa?" Akauliza

"Ooh hapana...hapana Rian sio hivyo" Retha akajitetea

"Then why Retha? Mama ndie alikualika labda nikutumie namba yake umwambie mwenyewe" Ed alifurahia maongezi haya maana alihisi yanapunguza uchovu uliokuwa kwenye mwili wake...

"What!!....Ooooh no Rian no ninakuomba"

Aretha alimsihi Ed

"Okay...Tell me the truth nitakusaidia Retha."

Aretha akanyamaza kwa sekunde kisha akasema "nitakuwa na usingizi sababu muda wa kulala umeenda sana"

"Then lala sasa halafu nitamwambia mama utachelewa na Derrick asiwahi kukuchukua" Edrian alitaka sana mama yake apate muda na Aretha ili baadae apate maoni yake. Aliamini hii itakuwa nafasi nzuri ya Aretha kuwa karibu na familia yake.

"No..oh Rian sorry... amhhh" Aretha akasema kwa haraka...

"Retha, kama unataka usiende makusudi niambie nitamwambia mama hauko tayari sio______"

"Sio hivyo Rian please" Aretha akamkatisha Ed

"Then niambie ukweli" Ed akamwambia taratibu alihisi kuna kitu nyuma ya kile anachokisema Aretha

"Mmmhhhhh..."akashusha pumzi Aretha kisha akaendelea, "Rian aaahm ...sidhani aaah ni vizuri tukutane kwa mama hmmmm ..na yule dada.. mchumba wako" Aretha aliongea kwa shida kiasi kwamba Ed aligundua

"Retha, mama alikualika wewe. Usiwaze habari ya mtu mwingine. Na huyo unayemuwaza hatakuwepo. Please usimhuzunishe mama!" Ed aliyasema maneno yale kwa uchungu maana alihisi labda kuna kitu Lyn alimwambia Aretha hata anaogopa kuwa pamoja nae sehemu moja...

"Hapana...Rian. .sitamhuzunisha mama. Basi hamna shida. Samahani nikuache ulale..Us____"

"Retha" Edrian akamuita kwa upole...

"Abeee"

"Utaniruhusu nije nikupeleke badala ya D?"

"Eeeh. Aaaah.Rian na kazi?" Akauliza Retha

"Retha, Jumamosi ninaweza kupata nafasi. Naomba nikupeleke nikuondoe na wasi wasi. Halafu nitaondoka na nitakuijia baadae"

"Sawa Rian. Usiku mwema"

"Nawe pia Retha?" Ed akatabasamu wakati akiiweka simu kwenye meza ndogo pembeni ya kitanda.

"Thank you Retha" akasema taratibu akajigeuza na kulala moyoni akiwa na furaha ya kuwa jumamosi na jumapili atakuwa na muda wa kuwa karibu na Aretha kwa urahisi zaidi. Akakumbuka Aretha alivyokaribia kuahirisha sababu ya Lyn akaazimu kushughulika na suala la Lyn.

"She is wicked"akajisemea moyoni huku akilala taratibu