Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 71 - ADUI ASIYEFAHAMIKA

Chapter 71 - ADUI ASIYEFAHAMIKA

"Joselyn mwanangu naomba unisikilize, huwezi kumlazimisha mwanaume akupende, na wala usijaribu sababu utavuna maumivu na huzuni" mama yake Lyn alimwambia binti yake ambaye muda huu wa asubuhi alikuwapo nyumbani baada ya kuruhusiwa na daktari pale Embassy Hospital.

"Mama, naheshimu sana mawazo yako lakini katika hili naomba uniache, mimi simlazimishi Edrian bali namsaidia kujua kile ambacho anakitaka" alijibu huku akiwa ameegemea kwenye ubao wa kitanda baada ya kupata supu ya asubuhi aliyoandaliwa na mama yake..

"Mwanangu, kama humlazimishi kwa nini ulikunywa vidonge wakati unajua hutakiwi kabisa kunywa antidepressants na..."

"Ma..niache, ninajua nachofanya, haukikubali usiongee chochote, wewe mbona ulimng'ang'ania baba hadi sasa umebaki nae halafu un__"

"Joselyn" sauti ya mama yake iliita kwa ukali huku akimwangalia

"Nini mama! Hutaki nikukumbushe yale uliyofanya eeeh?"

"Mhmhhh" mama yake akashusha pumzi kwa nguvu kisha akamjibu binti yake

"Chochote mnachofanya na baba yako kwa yule kijana kiache"

"Kwa hiyo huyo kijana ni bora kuliko mimi eeeh" Lyn alimuuliza mama yake huku usoni tayari alionesha kukerwa

"Kwa sababu wewe ni bora ndio maana nataka uache__"

"Sikia mama, nataka kulala maana jioni naelekea kumuona mama yake huyo kijana na usijaribu kunizuia au kunifuata" Lyn akamwambia mama yake huku akishusha vyema mwili wake kulala

"Unaendaje huko wakati bado unahitaji kupumzika Joselyn!" Mama yake akashangaa

"Ndio utoke nipumzike au hujaelewa mama" Lyn akageukia upande wa pili.

"Mwanangu..bado unaweza kubadilika. Nitakusaidia tafadhali nipe nafasi nifanye___"

"Mama" Lyn akaita kwa hasira.

Mama yake akamwangalia binti yake na kutikisa kichwa akisikitika " Sawa mwanangu" akavuta shuka iliyoachwa pembeni akamfunika binti yake.

Akachukua vyombo alivyotumia binti yake na kuondoka mle chumbani. Moyoni aliendelea kujilaumu "kama ningemchukua asingekuwa hivi, Mungu nisaidie"

************************

Edrian alikuwa katika majukumu mazito tangu asubuhi alipoingia ofisini. Linus, Allan, Beno, Ganeteu na wanasheria wengine wawili waliendelea kupitia mafaili ya wafanyakazi wa SGC - Mining yaliyotumwa kutoka miji minne. Loyce alikaa pembeni kidogo ya meza ambapo kikao kiliendelea Bado ripoti za maendeleo ya kila mgodi zilikuwa mezani zikisubiri kuwekwa vyema, kompyuta mpakato zilijaa kwenye meza na sauti ya kubofya ilisikika vyema kwenye chumba hiki cha mikutano.

Simu ya Ed iliita akapokea, baada ya kusikia sauti ya Captain, akainuka na kutoka nje ya chumba kile ambacho hakikuwa mbali na ofisi yake. Akaingia

"Kwa hiyo hakuna historia yoyote ya Renatha ambayo inatia mashaka yoyote?" Akauliza Ed!

"Hakuna historia niliyopata mkuu, mashaka yangu yako hapa, ana mwezi mmoja tu tangu aajiriwe na Wizara kama mtafiti. Kwa nini wizara ilete mtu ambaye si mzoefu sana kwenye kampuni inayomiliki migodi minne?"

"Unashaurije Captain?" Ed akauliza huku akichua paji lake la uso

"Take her in but be cautious, kuwa mwangalifu na taarifa za muhimu za ndani ya kampuni. Nitaendelea kuangalia zaidi. Chanzo changu kimoja wizarani ameniambia alipangwa mtu mwingine kuja hapo lakini mabadiliko ya ghafla yalifanywa dakika za mwisho."

"Okay Captain!" Ed akajibu huku akiegama kwenye kiti

"And one more thing!" Captain alimuwahi Ed kabla hajakata simu..

"Mmm" akaitika Ed

"Kuhusu ile gari uliyosema kufuatilia, inamilikiwa na mtu anaitwa TM. Bado natafuta kirefu cha hili jina. Hakuna picha yake tuliyopata zaidi ya biashara anazojihusisha nazo. Ni mtu wa madini pia. Tumejaribu kumuunganisha na Martinez lakini hawana connection. Tunaendelea kushughulikia." Captain alimueleza Ed

"Sawa. Let's work Captain" Ed alisema na kisha akakata simu, akainuka na kujinyoosha.

Akarudi kwenye chumba cha mkutano, huku mara kwa mara akiangalia saa iliyokuwa ukutani. Alikusudia kumaliza saa saba, kisha safari ya kumchukua Aretha ingefuata baada ya kupata chakula. Asubuhi ile alimpigia Derrick na kumfahamisha mabadiliko ya yeye kumpeleka Aretha nyumbani ambayo alihisi yalimfurahisha sana mdogo wake. Haikuwa uongo maana Derrick alifurahi mno.