"Karibu," Edrian alirudia makusudi ili kumshtua mgeni wake ambae alisahau kujitambulisha
"Oh...Samahani nimevutiwa na mandhari ya humu ndani hata nikasahau hunifahamu, Naitwa Renatha Musoti, natokea Wizara ya Madini na Nishati..." akamkazia macho Ed ambaye aliachia tabasamu
"Edrian Simunge ... Karibu Renatha!"
"Call me Renee" akampa ishara kwa mkono
Edrian akatabasamu "Sawa Renee nitegemee nini kutoka wizarani?"
"Oh....kuhusiana na ukaguzi uliofanyika kwenye moja ya migodi ya SGC.. wakati tunasubiri ukaguzi wa pili ndani ya siku 14, kuna maagizo maalum yametolewa kwa makampuni yote yanayojihusisha na uchimbaji madini. Katika maagizo hayo mtahitajika kufanya kazi na mtu mmoja kutoka wizarani. Kwa SGC mimi ndie nimepewa jukumu la kufanya kazi na nyie" Renatha akapumzika kidogo huku akimwangalia Ed ambaye aliegama kichwa chake kwenye kiti akimsikiliza kwa makini
Akaendelea "hivyo nitaanza rasmi jumatatu na hii hapa ni barua yangu pamoja na maelekezo ya mambo nitakayoyafanyia kazi." Akainuka kidogo na kunyoosha mkono kumkabidhi faili na bahasha alivyokuwa navyo mkononi.
Ed akapokea na kuweka mezani wala hakutaka kufungua akaendelea kumsikiliza na kusababisha Renatha kushangaa
"Haufungui kuangalia kama nachosema ni kweli?"akauliza
Edrian akaachia tabasamu "kwani unaweza kuwa unadanganya?"
Renatha akakohoa kidogo, akapeleka macho yake pembeni asimwangalie Ed ambaye alikuwa na tabasamu laini huku akimwangalia machoni...
"Ahh...hapana... ok, ni kwa sababu hapa ndio sehemu ya kwanza bosi hasumbuki kuthibitisha nachosema" akazungusha macho na kumwangalia Ed
"Nitaangalia bila shaka. Bosi mpumbavu pekee ndiye ataamini maneno anayosikia tu bila uthibitisho wowote" Ed akamwambia huku akirudi na kuegama kwenye kiti!
Renatha akabaki anamuangalia kwa mshangao aliposema maneno haya..
Kimya kifupi kikapita kati yao...Edrian akamuangalia sana binti huyu kuna namna alikuwa anamfanania kidogo Aretha. Muonekano wake tangu alipokuwa akiingia ungeweza kuhisi ana undugu na Aretha. Lakini Ed hakutaka kuingiza hisia zake kwenye majukumu yake ya kazi. .
"Sawa Renatha tutaangalia vielelezo vyako vyote na utapokea barua ya kuitwa na HR. Kaa karibu na e-mail yako leo na kesho."
Edrian akampa maelekezo
"Kwani manataka kunifanyia usaili Mr Simunge?...haya ni maelekezo ya makao makuu" akaongea kwa ujasiri Renatha akirudi kumwangalia Ed ambaye naye akampa jibu kali..
"Na mimi sipokei mtu kufanya kazi hapa kabla sijajiridhisha na uwepo wake hapa, una wasi wasi tukifanye usaili hautakuwa na vigezo vya kuwa SGC aaah?" Tabasamu la mzaha likamtoka Edrian ambaye aliinama mbele kumwangalia Renatha..
"I hate the way he looks at me as if am naked..nitamuonesha" Renatha aliwaza moyoni, akamjibu
"Kwa nini niogope usaili ninajua hii kazi ni maagizo ya wizara na hayana mjadala wa usaili, lakini kama unataka kunifanyia usaili be my guest" akamjibu kwa ujasiri na kuangalia macho ya Edrian asiye na hofu
"Okay.. kama nilivyosema, e-mail itatumwa kwako leo au kesho na maelekezo ndani yake. Karibu SGC Renatha Musoti" Edrian aliyasema haya huku akiinuka na kumpa mkono Renatha ambaye aliinuka na kurudisha kitendo kile kilichoonesha makubaliano yao. Renatha akakamata pochi yake na kuanza kuelekea mlangoni akifuatiwa na Edrian aliyekuwa nyuma.
Edrian alimuangalia alivyotembea kwa kujiamini, kichwani akitafakari mambo mawili, kwa nini maagizo ya haraka pasipo kushirikishwa na wizara. La pili ni mfanano wa huyu dada na Aretha kama wenye undugu kati yao..
Baada ya mgeni kutoka, akafunga mlango akarudi kukaa na kufungua bahasha na kuisoma barua iliyomtambulisha Renatha kisha akafungua faili na kulisoma...akainua simu yake na kupiga
"Hellow Captain"
"Kuna faili nakutumia nikimaliza kui-scan, tafadhali check taarifa za huyu mtu."
"Okay"
Edrian akamaliza kuongea na simu. .. Akatuma ujumbe kwa Lyn wapi wakutane jioni ile ili waweze kuongea. Alijua nyumbani kwake sio hapafai kwa kile alikusudia kumwambia Lyn.
Akaendelea na kazi zilizokuwa mbele yake mwishoni mwa wiki. Hapa na pale hakuacha kumfikiria Aretha japokuwa alijizuia asimtumie ujumbe mida hii